Pakua Mwongozo wa Muwezeshaji

Karibu

Mpendwa Mwezeshaji,

Karibu  kwenye  Ulimwengu Wangu wa Kidijitali. Hii ni programu ya kidigitali ya Facebook na huduma za mtandaoni kwa watu wazima waojua kusoma na kuandika. Mwongozo huu umepangiliwa kuongoza na kusaidia wawezeshaji ulimwenguni kufanikisha utekelezaji wa programu kwa watu wazima wanaojifunza.

Faragha: Somo hili litawasaidia washiriki kujua jinsi ya kutunza siri zao na siri za watu wengine. Pia litawasaidia kukuza utambulisho na sifa yao mtandaoni pamoja na kusimamia taarifa zao binafsi.

Usalama: Somo hili litawasaidia washiriki kujua jinsi ya kusimamia ulinzi wa vifaa vyao vya mawasiliano, programu na nenosiri.  Pia litawapa ujuzi wa kutumia program za uangalizi ili kuongeza usalama wa akaunti zao mtandaoni. Mwisho, litawasaidia washiriki kujua jinsi ya kutambua na kuchukua hatua iwapo akaunti zao zitadukuliwa.

Kuepuka ulaghai: Somo hili litawasaidia washiriki kutambua aina za uwongo, kuelewa juu ya hatari ya kusambaza taarifa binafsi zinazo julikana mtandaoni na kujua njia salama ya kuripoti kashfa.

Ujuzi wa vyombo vya habari: Somo hili litawasaidia washiriki kutambua na kufanya maamuzi kuhusu uaminifu wa vyanzo vya kidijitali, kuelewa uhusiano kati ya ujuzi wa vyombo vya habari na utambulisho na sifa yao mtandaoni, na kuelewa jinsi ya kukabiliana na taarifa potofu.

Uraia wa kidigitali na Mahusiano Mazuri: Somo hili litawasaidia washiriki kutambua na kufanya maamuzi kuhusu uaminifu wa vyanzo vya kidijitali, kuelewa uhusiano kati ya ujuzi wa vyombo vya habari na utambulisho na sifa yao mtandaoni, na kuelewa jinsi ya kukabiliana na taarifa potofu.

Ulimwengu Wangu wa Kidijitali umetengenezwa ili kuwasilishwa kama mtaala kamili au kama masomo yanayo jitegemea kufundishwa darasani uso kwa uso, au kufundishwa kwa njia ya mtandao.

Kila somo lina mafunzo matatu muhimu. Mafunzo katika kila somo husaidia washiriki kujifunza ujuzi kwa ajili ya matumizi chanya na salama wanapowasiliana na wengine katika mitandao ya kijamii. Kila somo limeandikwa kikamilifu na hutoa mwongozo kuhusu jinsi ya kubadilisha maudhui na mazoezi husika ili yaendane na muktadha wa eneo husika pamoja na mahitaji ya wawezeshaji na washiriki.

Kila somo pia linajumuisha viungo vya nyenzo za ziada, zoezi moja au zaidi ili kuchagiza majadiliano na kujifunza pamoja na maswali yanachunguza uelewa wa washiriki (k.m., chagua jibu sahihi, ukweli au uongo n.k). Masomo yanaweza kutumika katika mazingira yasiyo kupitia jukwaa shirikishi la kujifunza au mazingira rasmi ya kujifunzia (iwe ana kwa ana au kwa njia ya mtandao).

Mwongozo ufuatao unapaswa kusomwa na kuzingatiwa kwa makini kabla ya kutumia mtaala huu. Mwongozo unatoa mapendekezo ya jinsi ya kuanza, kuelewa masomo na muundo wake pamoja na mambo muhimu ya kuongoza uwezeshaji. Mwongozo huu pia unatoa muhtasari wa kila somo la kujifunza ili kuangazia mawazo makuu kwa mwezeshaji, ukijumuisha maelezo, malengo ya kujifunza, mada za somo na istilahi muhimu.

Ahsante kwa kuwezesha  Ulimwengu Wangu wa Kidijitalina kusaidia watu wazima kwenye jamii  kuwa tayari na  kuwa wananchi wawajibikaji wa kisasa.

Wako Mwaminifu,

Antigone Davis

Mkuu wa Kimataifa wa Idara ya Usalama, Meta