Epuka Kutapeliwa

Muhtasari

Washiriki watajifunza jinsi ya kutambua utapeli na ulaghai wa kawaida mtandaoni, ikiwa ni pamoja na viashiria vya utapeli, Hadaa Mtandaoni na ulaghai mwingine wa mtandaoni. Washiriki wataelewa hatari za kuposti taarifa zao binafsi kwenye tovuti zisizo na ulinzi na wanapotumia Wi-Fi za umma. Pia watajifunza jinsi ya kulinda taarifa zao za benki wakati wa manunuzi mtandaoni na tahadhari za kuchukua wanapokamilisha miamala ana kwa ana. Washiriki watajua jinsi ya kuripoti utapeli au uhalifu mwingine wa mtandaoni unaoshukiwa.