Sisi Ni akina Nani

Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na wataalamu walioko Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ulimwengu Wangu wa Kidijitali hutoa moduli za mafunzo na vifaa ili kujenga ujuzi kwa ajili ya ulimwengu wa kidijitali. Kupitia Ulimwengu Wangu wa Kidijitali, Meta inawafikia wanafunzi kote katika ukanda huu na kuitengeneza jumuiya ya kidijitali ya Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa bora.

Masomo haya yametengenezwa kwa ajili ya wanafunzi wenye umri wa miaka 13-17 wa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mtalaa umetengenezwa na maelekezo ya hatua kwa hatua kwa ajili ya walimu wa wanafunzi wenye umri huu. Masomo haya yametolewa kwenye vifaa vya washirika kadhaa wataalamu wenye uzoefu wa kusanifu maudhui na mitalaa. Tafadhali angalia ukurasa wa Kuhusu Sisi kwenye tovuti ili kujifunza zaidi kuhusu washirika wetu wa maudhui.

Mtaala wa Vijana (umri wa miaka 13 - 17)

Ulimwengu Wangu wa Kidijitali ilishirikiana na mashirika yote ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kutengeneza mdouli za mafunzo na vifaa katika mtalaa. Jifunze zaidi kuhusu washirika wetu katika eneo letu na jinsi wanavyotengeneza mustakabali wa uraia wa kidijitali katika ukanda uliopo hapa chini:

  • Asikana Network

    Asikana Network ni shirika linaloshughulika na masuala ya kijamii nchini Zambia ambalo linajikita katika kuongeza ushiriki hai na wenye manufaa wa wanawake na wasichana katika kozi zinazohusiana na masuala ya kiufundi. Mpango huu unajikita katika ukuzaji wa mbinu kupitia kutoa mafunzo, ushauri na kuwaweka katika mafunzo kwa vitendo ili kuwakuza vijana wa kike.

    Visit Asikana Network Tembelea
  • Chama cha Amani & Maendeleo Afrika

    Chama cha Amani & Maendeleo Afrika ni shirika la asasi za kiraia linalohusika katika kutekeleza na kufuatilia masuala ya sera za mtandaoni za watoto nchini Kameruni na katika eneo la Afrika ya kati kwa ujumla. Kutokana na mwelekeo huu, tunashirikiana kwa karibu na mashirika mengi ya umma, binafsi na ya kimataifa yanayohusika katika ukuzaji na udhibiti wa mawasiliano ya kutumia simu, redio na televisheni katika jamii yetu.

  • Authentic Africa Group

    Authentic Africa Group ni shirika linalotoa huduma anuwai kwa biashara zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambalo linatoa usimamizi kamili wa mipango na huduma za ushauri ili kusaidia biashara kukua haraka zaidi.

    Visit Authentic Africa Group Tembelea
  • BS Corp

    BS Corp ni shirika la Wasenegal lililobobea katika kutoa mafunzo ya masuala ya kidijitali kwa watu waliotelekezwa zaidi. Tangu 2019, shirika la BS Corp limekuwa likitofa mafunzo ya elimu ya kidijitali huku zaidi ya watu 7,000 wakipokea mafunzo tangu lilipoanzishwa.

  • Center for Africa Leadership Studies

    Shirika la Center for African Leadership Studies (CALS) lilianzishwa mwaka 2012. CALS ni mojawapo ya makampuni yanayoongoza kutoa ushauri na mafunzo nchini Ethiopia yanayoangazia uongozi na masuluhisho ya ujasiriamali ili kujenga viongozi waliobadilika na wanaowajibika. xHub Addis ni mpango wa CALS ulioanzishwa mwaka wa 2014 ambao unakuza, kuharakisha ukuaji, kushauri, na kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wachanga ili wageuze mawazo yao bunifu kuwa biashara na huduma.

    Visit Center for Africa Leadership Studies Tembelea
  • Child Online Africa

    Child Online Africa (COA) ni shirika lisilo la kiserikali lililojikita katika utafiti na utetezi wa masuala ya watoto ambalo hufanya utetezi wa/na watoto na vijana pamoja na familia zao ili kushajihisha sera na kubadilisha taratibu zinazoathiri ustawi wa watoto nchini Ghana na Afrika nzima. Tuko tayari kushirikiana na wengine ili kutengeneza maudhui kwa ajili ya mtoto wa Afrika.

    Visit Child Online Africa Tembelea
  • Cybersafe Foundation

    Cybersafe Foundation ni shirika lisilo la kiserikali lililo katika sekta ya usalama wa taarifa ambalo linalenga kufanya juhudi za kuleta mabadiliko yatakayohakikisha kwamba intaneti ni salama kwa kila mtu barani Afrika anayeweza kupata teknolojia za kidijitali. Wanafanya kazi bila kuchoka ili kuboresha usalama wa intaneti barani Afrika, hasa kwa watu walio katika hatari kubwa zaidi katika jamii yetu, kupitia jitihada za shirika hilo.

    Visit Cybersafe Foundation Tembelea
  • Digify Africa

    Shirika la Digify Africa mwanzoni lilianza kama Live Magazine South Africa wakati ambapo mwanzilishi wake Gavin Weale alihamia Afrika Kusini kutoka Uingereza ili kuzindua gazeti hilo la vijana ambalo alikuwa akiliendesha jijini London, Uingereza tangu mwaka 2002. Live Magazine likawa gazeti la vijana lililosambaa sana nchini Afrika Kusini, huku maudhui yake yote yakizalishwa na vijana wasio na ajira wakifanya kazi chini ya washauri wataalamu. Kiini chake kilikuwa mradi wa kuleta mabadiliko kwenye jamii, huku wito wake ukiwa kufikia vijana wenye rasilimali finyu kupitia jumbe muhimu na kutengeneza ajira kupitia mchakato wake wa uzalishaji. Jambo hili lilifanya gazeti hilo kubuni mipango mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kampeni ya miaka minne ya shughuli za demokrasia, iliyojulikana kama kampeni ya VIP, pamoja na rudio la kwanza zaidi la Digify Pro lililozinduliwa mwaka wa 2014. Mwaka 2016, shirika la Digify Afrika lilianza shughuli zake nchini Kenya na Nigeria, na likapitia kipindi cha maendeleo makuu, likitoa mpango mkubwa wa mbinu za kidijitali kwa ushirikiano na Google, Wakfu wa Rockefeller na Baraza la Uingereza.

    Visit Digify Africa Tembelea
  • Eveminet

    Shirika la Eveminet linaongoza katika kuelimishana kuhusu masuala ya kidijitali na kudumisha usalama katika mtandao, hasa kwa familia, watoto, na mazingira yao. Wanapigania teknolojia jumuishi kwa watu wote kupitia mpango wao wa Light It Up Blue Initiative kwa ajili ya watoto wenye Usonji. Wanatengeneza watetezi wa kimataifa wa masuala ya kidijitali kwa kuleta mabadiliko wanayotaka kuona katika jamii.

    Visit Eveminet Tembelea
  • International Education and Resource Network

    International Education And Resource Network (iEARN- Kenya) ni mtandao wa wakufunzi wanaofundisha, kushauri na kuwasaidia wakufunzi na vijana kutoka kote ulimwenguni ili waweze kutumia teknolojia katika mafunzo wakiwa kazini na pia wakiendesha miradi kwa pamoja na wenzao kutoka ulimwenguni kote na kuchukua hatua zinazoshirikisha ulimwengu mzima katika jamii zao ili kuleta mabadiliko.

    Visit International Education and Resource Network Tembelea
  • Mtoto News

    Mtoto News ni kampuni ya vyombo vya habari inayotumia teknolojia kuboresha maisha ya watoto kwa kuhakikisha sauti zao zinasikika. Mtoto News hutengeneza majukwaa yanayowezesha kuwajulisha watoto sera, programu na taratibu. Majukwaa haya huwezesha kupangwa, kutengenezwa na kusambazwa kwa maudhui na watoto na kuhusu watoto, huku pia ikihimiza watungaji sera watumie tafiti sahihi na zinazoongozwa na watoto.

    Visit Mtoto News Tembelea
  • Bodi ya Kitaifa ya Viwango vya Mafunzo ya Kitaalamu

    Wito wa mwanzo wa Bodi ya Kitaifa ya Viwango vya Mafunzo ya Kitaalamu ni kuboresha viwango vya mafunzo kwa kudumisha vipimo vya juu na kamilifu ambavyo walimu weledi wanafaa kujua na kuweza kufanya, kutoa mfumo wa hiari wa kitaifa wa kuidhinisha walimu wanaotimiza viwango hivi, na kupigania mabadiliko katika sekta ya elimu ili kuijumuisha Bodi ya Kitaifa ya Uidhinishaji katika elimu ya Marekani na kutumia kikamilifu weledi wa Walimu Walioidhinishwa na Bodi ya Kitaifa. Bodi ya Kitaifa ambayo inatambulika kama "kiongozi katika uidhinishaji" wa walimu, inaamini kwamba kuboresha viwango vya walimu kutasababisha mafunzo bora zaidi kwa wanafunzi.

    Visit Bodi ya Kitaifa ya Viwango vya Mafunzo ya Kitaalamu Tembelea
  • Phambano Technology Development Centre NPC

    Phambano Technology Development Centre NPC ni shirika linaloendeshwa kwa lengo la kujulikana kama suluhisho la kujenga uwezo wa kiteknolojia kwa mashirika ya asasi za kiraia Kusini mwa bara la Afrika. Mipango yao ya kukuza teknolojia inawawezesha kuyapatia mashirika mengine yasiyokuwa ya kibiashara uwezo wa kuwafikia wanufaika wengi katika ngazi ya kawaida na ya kimataifa.

    Visit Phambano Technology Development Centre NPC Tembelea
  • Plan International

    Shirika la Plan International lililoanzishwa mwaka wa 1937 ni shirika la kibinadamu la maendeleo linalowalenga watoto ambalo halina mafungamano ya kidini au kisiasa na linalopigania haki za watoto na usawa kwa wasichana. Linajitahidi kuhakikisha kuna haki ulimwenguni, huku likishirikiana na watoto, vijana, wafadhili, na washirika. Shirika la Plan International huunga mkono maendeleo ya watoto yaliyo salama na yenye ufanisi kutoka wakati wa kuzaliwa hadi katika utu uzima.

    Visit Plan International Tembelea
  • re:learn

    re:learn by CcHUB, ambao ndio mpango wa Elimu wa Co-Creation Hub Limited, linajikita katika kutumia teknolojia kuwasaidia walimu, wanafunzi na shule ili kuboresha matokeo ya mafunzo, hasa katika Elimu ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Linapanga na kutengeneza maudhui yanayoshirikisha na kuhusisha watu, huku likitumia mbinu bunifu za kutoa mafunzo na kusaidia jamii yake ya maelfu ya walimu ili kubadilisha mafunzo katika madarasa yao.

    Visit re:learn Tembelea
  • Watoto Watch Network

    Watoto Watch Network (WWN) ni shirika lisilokuwa la kibiashara la nchini Kenya linaloshughulikia masuala ya watoto ambalo linaongoza katika kuhamasishana katika ulinzi wa watoto mtandaoni kwa kutekeleza mipango ya kufahamishana na kuhamasishana kuhusu usalama wa intaneti.

    Visit Watoto Watch Network Tembelea

Mtaala wa Watu Wazima (miaka 18+)

Ulimwengu Wangu wa Kidijitali ilishirikiana na mashirika yote ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kutengeneza mdouli za mafunzo na vifaa katika mtalaa. Jifunze zaidi kuhusu washirika wetu katika eneo letu na jinsi wanavyotengeneza mustakabali wa uraia wa kidijitali katika ukanda uliopo hapa chini:

  • Get Safe Online

    Kuwa Salama Mtandaoni ni tovuti iliyoidhinishwa na inayoheshimiwa sana iliyoundwa mahsusi kusaidia watu binafsi na biashara ndogo ndogo kuwa salama na kujiamini wanapotumia intaneti. Taarifa na ushauri unaotolewa – upo kwenye tovuti yake ya Uingereza www.getsafeonline.org, akaunti zake za mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, sehemu za uhamasishaji na kupitia chaneli za washirika wake. Mtaala umeundwa kutopendelea, kujifunza kwa vitendo na rahisi kufuatwa na hadhira inayolengwa. Kuwa Salama Mtandaoni pia hufanya kazi kwa karibu na idadi ya vikosi vya polisi na mashirika ya MOD, na pia, kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, imeanzisha mtandao wa tovuti na uwakilishi katika nchi 24 za Jumuiya ya Madola na kwingineko. Kuwa Salama Mtandaoni ilianzishwa mwaka wa 2006 na ni shirika lisilo la faida. Mtaala huu unafadhiliwa na Ofisi ya Uingereza ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO).

    Visit Get Safe Online Tembelea
  • Digital Promise

    Digital Promise ni shirika lisilo la faida la kimataifa linalofanya kazi kupanua fursa kwa kila kila mtumiaji wa mtandao. Tunafanya kazi na waelimishaji, watafiti, viongozi wa teknolojia na jumuiya ili kubuni, kuchunguza na kuongeza ubunifu unaosaidia watumiaji wa mtandao, hasa wale ambao wametengwa kihistoria na kimfumo.

    Visit Digital Promise Tembelea

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy