Sisi Ni akina Nani
Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na wataalamu walioko Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ulimwengu Wangu wa Kidijitali hutoa moduli za mafunzo na vifaa ili kujenga ujuzi kwa ajili ya ulimwengu wa kidijitali. Kupitia Ulimwengu Wangu wa Kidijitali, Meta inawafikia wanafunzi kote katika ukanda huu na kuitengeneza jumuiya ya kidijitali ya Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa bora.
Masomo haya yametengenezwa kwa ajili ya wanafunzi wenye umri wa miaka 13-17 wa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mtalaa umetengenezwa na maelekezo ya hatua kwa hatua kwa ajili ya walimu wa wanafunzi wenye umri huu. Masomo haya yametolewa kwenye vifaa vya washirika kadhaa wataalamu wenye uzoefu wa kusanifu maudhui na mitalaa. Tafadhali angalia ukurasa wa Kuhusu Sisi kwenye tovuti ili kujifunza zaidi kuhusu washirika wetu wa maudhui.