Uwezeshaji wa Kidijitali

Somo 3: Kufanya Uhamasishaji Kupitia Vyombo vya Habari

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Kutumia Vyombo vya Habari ili Kuleta Mabadiliko

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Vyombo vya habari ni njia nzuri za kushirikishana mawazo na watu wengine. Kwa watu wengi, majukwaa ya vyombo vya habari vya kidijitali huwa njia wanayopenda zaidi ya kutoa ujumbe wao. Kwa mfano, Taaooma na Elsa Majimbo hutumia Instagram na YouTube kusambaza visa vya kuchekesha na watu barani Afrika na dunia nzima. Kwa upande wake Natasha Mwansa hutumia Twitter kutetea haki za wanawake na vijana.

DONDOO ZA MWALIMU

Toa mifano ya watu wa eneo lako wenye ushawishi katika ulimwengu wa kidijitali ambao wanasambaza ujumbe wao katika majukwaa ya kidijitali. Mfano huu unalenga kuwaonesha wanafunzi jinsi watu wengine wanavyotumia intaneti katika utetezi wa mambo wanayojali. Mifano ni kama:

 • Ethiopia: Yared Shumete hutumia Facebook kuwasaidia wakimbizi wa ndani na waathiriwa wa ghasia wanaohitaji chakula, makazi, na mavazi.
 • Kenya: 'Churchil' Daniel Ndambuki anayetumia YouTube, Facebook, na Instagram kusambaza visa vya kuchekesha na watu kutoka kote ulimwenguni, na Julie Gichuru anayetumia Twitter kutetea haki na kushiriki fursa za kuimarisha uchumi wa vijana waliotengwa.
 • Nigeria: Taaooma na Elsa MaJimbo hutumia Instagram na YouTube kusambaza visa vya kuchekesha na watu kote barani Afrika na dunia nzima, huku Malala Yousafzai akitumia Twitter kutetea haki za wanawake na vijana.
 • Zambia: Steffan Phiri hutumia TikTok kusambaza visa vya kuchekesha na watu kote barani Afrika huku Natasha Mwansa akitumia Twitter kuwawezesha vijana barani Afrika.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Wakati mwingine, watetezi hutumia vyombo vya habari vya kidijitali kulenga matatizo mahususi.

DONDOO KWA MWALIMU

Toa mifano ya watetezi wa eneo lako ambao wanasambaza ujumbe wao katika majukwaa ya kidijitali. Mfano huu unalenga kuwaonesha wanafunzi jinsi watu wengine wanavyotumia intaneti katika utetezi wa mambo wanayojali. Mifano ni kama:

 • Kenya: Digital Farmers Kenya, ni kundi katika Facebook lenye wanachama 434,694 ambalo huhimiza wanachama wake kubadilishana mawazo ya kilimo na teknolojia mpya zaidi za kilimo ambazo wakulima wanaweza kuanza kuzitumia ili kuboresha mazao yao.
 • Nigeria: Zuriel Oduwole ni kijana anayetengeneza filamu na mwanaharakati aliyeanzisha mradi unaojulikana kama “Dream Up, Speak Up, Stand Up,” ambao ni kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayopigania kuboreshwa kwa elimu ya mtoto wa kike barani Afrika.
 • Zambia: Buumba Malamba ni mtetezi wa haki za mwanaharakati mtoto nchini Zambia. Alitumia mitandao ya kijamii kama jukwaa la kuanzisha shirika lake linalozungumzia unyanyasaji wa watoto na kuwasaidia watoto walionyanyaswa.

DONDOO ZA MWALIMU

Kwenye skrini ya projekta mbele ya darasa, onesha mfano wa video inayoendana na maudhui ya eneo/mkoa wa wanafunzi wako ili kuonesha jinsi vyombo vya habari vinavyoweza kutumika kuhamasisha na kutetea masuala fulani.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tunapoendeleza jitihada za utetezi, vyombo vya habari vya aina zote vinaweza kuwa zana nzuri sana katika kutimiza malengo yetu. Katika zoezi linalofuata, mtaangalia wazo hilo kwa kutengeneza ujumbe na kuusambaza kupitia vyombo vya habari mbalimbali ili kuwafikia watu wengi.

Zoezi

Sehemu ya 1

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tafuta mfano wa vyombo vya habari (mfano, video ya YouTube, chapisho la Facebook, au picha) ambayo inaleta msukumo na ambayo huenda ikawa njia nzuri ya kusambaza ujumbe kuhusu suala fulani unalojali. Mna dakika 15 za kutafuta maudhui hayo. Baadaye, wanafunzi watalionesha kundi zima maudhui waliyopata na kuelezea kwa nini wanadhani yanaleta msukumo.

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wape wanafunzi dakika 15 ili watafute mfano wa vyombo vya habari ambavyo wanaamini vinasambaza ujumbe kuhusu suala fulani kwa njia nzuri. Baadaye, chukua dakika 15 na umuombe kila mwanafunzi aeleze kwa kifupi na/au aoneshe hivyo vyombo vya habari kwa kundi zima huku akizungumzia kwa nini anadhani vinaleta msukumo.

Sehemu ya pili ya zoezi hili inaweza kukamilishwa wakati wa mkutano wa sasa wa kundi au wa pili, ikitegemea na muda uliotolewa.

Sehemu ya 2

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Sasa kwa kuwa mmepata na kuzungumzia mfano wa vyombo vya habari vyenye kuleta msukumo na vinavyoweza kutumika kutangaza suala fulani, hivi sasa ni wakati wa kutengeneza maudhui yenu wenyewe kuhusu masuala mnayojali.

Katika muda wa dakika 20 zijazo, fikiria kuhusu suala lenye umuhimu kwako kisha uandike wazo lako kuhusu aina mahususi ya vyombo vya habari ili kuhamasisha watu kuhusu suala hilo. Inaweza kuwa:

 • Chapisho la maandishi litakalozungumzia jitihada unayotaka kufanya na kwa nini watu wanafaa kuchukua hatua
 • Wazo la picha au mchoro (au picha/mchoro wenyewe) utakaoeleza sababu na jinsi watu wanavyoweza kuunga mkono jitihada hiyo
 • Wazo la video ya kuhamasisha watu na kuwahimiza kuchukua hatua kuhusu suala hilo

Mbali na wazo hili, tafadhali andika:

 • Angalau njia mbili unazoweza kutumia kusambaza ujumbe wako wa kwenye vyombo vya habari ili kuongeza uonekanaji na kuhamasisha watu zaidi kuhusu jitihada zako
MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wape wanafunzi dakika 20 ili waandike mawazo yao. Baadaye, waombe wanafunzi wazungumzie mawazo waliyoandika katika kundi zima. Jadilianeni kwa dakika 15.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa
Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy