Uwezeshaji wa Kidijitali

Somo 5: Ni Wakati wa Kuchukua Hatua!

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Mpango wa Kuleta Mabadiliko!

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika baadhi ya mafunzo mengine yanayohusiana na masuala ya kiraia na kisiasa ambayo tumekamilisha pamoja, tuliangalia mbinu na mawazo tofauti yanayoweza kutusaidia kuwa watetezi wa kuleta mabadiliko.

Tumetambua masuala yanayoathiri jamii zenu na kujifunza kuhusu zana mahususi ya kujenga mitandao ya watu na maudhui yatakayotumiwa kuleta mabadiliko chanya.
Sasa, ni wakati wa kuleta mawazo haya pamoja na kupanga kampeni yako ya utetezi kutoka mwanzo hadi mwisho!

DONDOO KWA MWALIMU

Hiari: Toa wasilisho kuhusu kampeni ya utetezi inayoendelea sasa hivi na inayohusisha masuala ya vijana ambayo inalingana na muktadha wa eneo lako/la wanafunzi wako. Tovuti za Sauti za Vijana (kwa Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, na Kiarabu) na Sauti za Ulimwengu (kama itasaidia, ndani ya tovuti hiyo, tafuta neno "vijana") huenda zikawa vyanzo vya kuwapa msukumo ikiwa hamna hakika kuhusu kampeni mtakayochagua. Jisikie huru kuonesha tovuti ya kampeni hiyo kwenye skrini ya maonesho huku ukizungumzia kampeni hiyo. Lengo la kampeni hii ni kuwaonesha wanafunzi jinsi kampeni ya utetezi inavyokuwa.

Zoezi

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Andika muhtasari wa kampeni ya utetezi ambayo ungependa kuendesha katika jamii yako. Unaweza kuongeza maandishi uliyoandika katika mafunzo ya hapo awali. Kwa mfano, unaweza kuweka maelezo kuhusu suala hilo unalotaka kulishughulikia au kueleza kwa nini mtu maarufu ambaye umechagua kwa ajili ya kuendesha kampeni yako analingana na malengo ya utetezi unaotaka kufanya. Shirikianeni katika makundi madogo ili kutoa hoja na kubuni mpango wa kampeni yenu. Mtakuwa na dakika 45 za kubuni kampeni zenu.

Tafadhali jibu maswali yafuatayo:

  • Ni tatizo gani unalotaka kusuluhisha?
  • Tatizo hili linaathiri jamii gani?
  • Ni kwa vipi ungependa kulishughulikia tatizo hili?
  • Ni vyombo gani vya habari ambavyo utatumia kukuza uhamasishaji kuhusu jitihada unayoendesha? Kwa njia zipi?
  • Kuna mtu maarufu ambaye ungependa kumtumia ili kusaidia kuendesha kampeni yako? Vipi?
  • Ni nani atakayekuwa katika mtandao wa watu wanaokusaidia?
  • Ni alama ya reli ipi utakayotengeneza kwa ajili ya kampeni yako?
  • Kampeni yako itadumu kwa muda gani?

Jisikie huru kubuni mawazo yako kwenye Hati ya "Kampeni ya Utetezi" au kwenye karatasi nyingine.

Wape wanafunzi Hati za "Kampeni ya Utetezi".

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Sasa katika makundi ya watu wawili wawili, mtazungumzia mipango yenu ya kampeni za utetezi mliyoandika. Zungumza na mwenzako kuhusu kipengele cha kampeni yako kinachokusisimua zaidi!

Wape wanafunzi dakika 20 ili kuzungumzia kampeni zao.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa
Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy