Kuchangamana Kidijitali

Somo 6: Mtu Mwema Zaidi Unayeweza Kuwa

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Mtafanya zoezi litakalowaruhusu kuwa wabunifu kiasi mnachotaka: Mtafikiria kuhusu jinsi maisha yenu yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Anza kwa kuwaomba wanafunzi wafumbe macho yao au waangalie sehemu ya sakafu iliyo mbele yao kisha wavute pumzi kwa nguvu mara chache.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO

Tumieni muda kufikiria kuhusu jinsi maisha yenu yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa. Mambo yametokea jinsi tu mlivyotumaini. Kimyakimya, fikiria kuhusu majibu yako ya maswali yafuatayo.

  • Utakuwa ukifanya nini?
  • Ni nani atakuwa katika maisha yako?
  • Ni nini kitakuwa muhimu zaidi kwako?
MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wape wanafunzi kitini cha "Mtu Mwema Zaidi Unayeweza Kuwa" kisha uwaombe wakijaze peke yao. Baada ya wanafunzi kumaliza, wape wanafunzi fursa ya kuzungumza kuhusu mambo waliyoandika au mawazo yao kuhusu mchakato huu baina yao au na darasa zima, ikiwa hakuna tatizo kwao kufanya hivyo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Waambie wanafunzi wafikirie kama zoezi hili lilithibitisha msukumo wao maishani, au ikiwa hawana hakika kuhusu msukumo wao, je, shughuli hii iliwapa kidokezo cha kufahamu msukumo wao unaweza kuwa upi?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kuelewa msukumo wetu maishani hakutatusaidia tu katika maisha yetu ya kila siku, lakini pia kunaweza kuhakikisha kwamba tunawasiliana vizuri mtandaoni kwa namna inayoonesha watu bora zaidi tunaoweza kuwa pamoja na kutuelekeza kwenye msukumo wetu katika maisha.

Zoezi

(la kufanyiwa darasani au nyumbani)

Masuala ya Kufikiria Baada ya Zoezi
  • Je, wanafunzi walilichukulia vipi zoezi hili? Je, waliliona ni muhimu katika kuamua lengo lao liwe lipi?

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Somo hili linatolewa kwa ushirikiano na kituo cha Greater Good Science Center katika UC Berkeley. The Purpose Challenge Toolkit (Mkusanyiko wa Zana za Zoezi la Msukumo wa Maisha) ulitengenezwa na Dkt. Kendall Cotton-Bronk akishirikiana na mashirika ya Greater Good Science Center na Prosocial. kendallcottonbronk.com. Kwa maelezo zaidi, tembelea: purposechallenge.org & ggie.berkeley.edu/practice/best-possible-self

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy