Moduli za Mafunzo

Moduli zetu za mafunzo zimetengenezwa ili kuwawezesha watu kupata maarifa ya kutafakari kwa kina kuhusu tabia zao za kidijitali. Mpango wa Ulimwengu Wangu wa Kidijitali umetengenezwa ili kuwasilishwa kama mtalaa kamili au somo moja moja katika mazingira ya teknolojia ya juu au teknolojia ya chini. Masomo hayo yameandikwa kikamilifu na yanatoa mwongozo kuhusu jinsi unavyoweza kujiandaa kwa ajili ya masomo hayo na kuyafundisha katika mazingira rasmi na yasiyo rasmi. Masomo hayo yako wazi kiasi kwamba unaweza kuyarekebisha ili yaendane na mahitaji ya wanafunzi wako.

Utangulizi wa Mafunzo ya Kidijitali

Masomo na mazoezi katika sehemu hii yanawasaidia wanafunzi kuelewa maana ya intaneti, taarifa ya utambulisho inayoweza kusambazwa kwenye intaneti, kutambua njia tofauti za kupata taarifa mtandaoni na kuyajua manufaa, majukumu na wajibu wa uraia wa kidijitali.

Jifunze Zaidi

Misingi ya Kidijitali

Masomo na mazoezi katika sehemu hii yanawasaidia wanafunzi kuelewa jinsi ya kuunganishwa na kutumia intaneti na majukwaa mengine vizuri. Masomo hayo pia yanawasaidia wanafunzi walinde data na taarifa zao (na za wengine), na vilevile vifaa na mali zao za kidijitali.

Jifunze Zaidi

Ustawi wa Kidijitali

Masomo na mazoezi katika sehemu hii yanawasaidia wanafunzi wachunguze utambulisho wao, washirikiane (watu binafsi na pia makundi makubwa) mtandaoni kwa njia za huruma, kimaadili na chanya, na kukabiliana na hatari zinazoweza kuletwa na ulimwengu wa kidijitali ili kulinda afya zao za mwili na kiakili.

Jifunze Zaidi

Kuchangamana Kidijitali

Masomo na mazoezi katika sehemu hii yanawasaidia wanafunzi kufasiri tofauti za kitamaduni na kijamii, wajibu na kushirikiana kwa heshima, na wachanganue, waunde na kushiriki aina tofauti za maudhui ya vyombo vya habari. Ujuzi unaoshughulikiwa: muktadha, ubora wa taarifa na elimu ya vyombo vya habari.

Jifunze Zaidi

Uwezeshaji wa Kidijitali

Masomo na mazoezi katika sehemu hii yanawasaidia wanafunzi kushiriki katika masuala ya umma na utetezi unaohusu mambo muhimu kwao. Ujuzi unaoshughulikiwa: maamiliano ya kiraia na uzalishaji wa maudhui.

Jifunze Zaidi

Fursa za Kidijitali

Masomo na mazoezi katika sehemu hii yanawasaidia wanafunzi wajifunze ujuzi wanaohitaji kuutumia kikamilifu fursa zinazoweza kupatikana katika ulimwengu wa kidijitali.

Jifunze Zaidi

Uraia wa Kidijitali

Washiriki wataelewa wajibu wao wanaposhiriki katika majukwaa ya kidijitali. Washiriki wataelewa jinsi ya kutengeneza mazingira chanya wanapotumia mitandao, na jinsi ya kulinda ustawi wao wanapokuwa mtandaoni. Washiriki watatambua michango ya wengine kama watengezaji wa maudhui na kushiriki katika jumuiya za mtandaoni ipasavyo.

Jifunze Zaidi

Ujuzi wa Vyombo vya Habari

Washiriki wataweza kutambua na kutathmini uaminifu wa vyanzo vya dijitali (ikiwa ni pamoja na vyanzo vya kuthibitisha, kutambua upendeleo, habari potofu, vyombo vya habari vilivyodanganywa na kutathmini utafutaji). Washiriki wataweza kueleza jinsi shughuli zao za mtandaoni na maudhui wanayosambaza yanavyoathiri sifa na utambulisho wao mtandaoni. Washiriki watajua jinsi ya kuongeza ufahamu na/au kuripoti habari zinazoshukiwa […]

Jifunze Zaidi

Faragha

Washiriki watajifunza jinsi ya kulinda faragha yao binafsi na jinsi ya kulinda faragha na usalama wa wengine. Washiriki watajifunza jinsi maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu binafsi yanavyosambaa kwenye mtandao. Washiriki wataelewa kuwa wanaweza kukuza na kudhibiti sifa na utambulisho wao mtandaoni kwa kuchukua hatua muhimu za faragha.

Jifunze Zaidi

Epuka Kutapeliwa

Washiriki watajifunza jinsi ya kutambua utapeli na ulaghai wa kawaida mtandaoni, ikiwa ni pamoja na viashiria vya utapeli, Hadaa Mtandaoni na ulaghai mwingine wa mtandaoni. Washiriki wataelewa hatari za kuposti taarifa zao binafsi kwenye tovuti zisizo na ulinzi na wanapotumia Wi-Fi za umma. Pia watajifunza jinsi ya kulinda taarifa zao za benki wakati wa manunuzi […]

Jifunze Zaidi

Usalama Mtandaoni

Washiriki watajua jinsi ya kudhibiti usalama wa vifaa vyao, programu na manenosiri. Washiriki wataweza kutumia vipengele vya Ukaguzi wa Usalama ili kudhibiti akaunti zao mtandaoni. Washiriki watatambua wakati akaunti zao au za watu wengine zinaweza kuathiriwa na kujua hatua za kuchukua.

Jifunze Zaidi

Usalama na Ustawi wa Vijana Mtandaoni

Masomo katika sehemu hii huwasaidia wanafunzi kujifundisha kuhusu zana na vidokezo mbalimbali vya kuwalinda vijana wao wanapokuwa mtandaoni na kuangazia namna tofauti za kuwasaidia kusimamia muda wao mtandaoni kwa njia chanya.

Jifunze Zaidi

Usalama na Ustawi wa Vijana Mtandaoni

Masomo katika sehemu hii huwasaidia wanafunzi kujifundisha kuhusu zana na vidokezo mbalimbali vya kuwalinda wanapokuwa mtandaoni na kuangazia namna tofauti za kusimamia muda wao mtandaoni kwa njia chanya.

Jifunze Zaidi

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy