Usalama na Ustawi wa Vijana Mtandaoni

Somo 3: Maingiliano Yanayofaa Umri Fulani

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na mawasilisho ya moduli.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Mjadala

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Ni kwa namna gani mitandao ya kijamii inaweza kutengeneza mazingara salama na yanayolingana na umri fulani kwa ajili ya vijana ili waweze kuingiliana baina yao mtandaoni na kushiriki mambo wanayopendelea na waliyopitia?
 • Ni jukumu gani ambalo wazazi au walezi wako wanafaa kuchukua ili kukuongoza katika matumizi yako ya mtandaoni, na ni nyenzo au zana gani ambazo zinaweza kuwasaidia katika jukumu hili?
 • Ni hatua gani zinazoweza kuchukuliwa ili kulinda usalama wako unapotumia mtandao huku bado ukitukuza uhuru wako?

Sehemu ya 1: Zana za Usimamizi wa Wazazi

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tulitambulisha Kituo cha Familia, ambacho ni nyenzo inayowapa wazazi na walezi mwongozo wa kitaalamu, zana za usimamizi na maagizo ya mazungumzo kupitia makala za kutaarifu. Kituvo hiki cha elimu kimeundwa ili kusaidia wazazi au walezi wako kuongoza hali ya sasa ya mtandaoni na kuwasaidia kuhakikisha muda wenu mtandaoni ni chanya na wenye msaada zaidi.

Zana za usimamizi wa wazazi huruhusu wazazi na walezi:

 • Kuangalia kiasi cha muda unaotumia katika Instagram na kuweka vikomo vya muda.
 • Kupata arifa ikiwa utaamua kushiriki ripoti fulani.
 • Kufuatilia akaunti unazofuata na zile zinazokufuata.

Tumeongeza vipengele vingi zaidi, ili:

 • Wazazi na walezi waweze kukualika ili uwe sehemu ya usimamizi kupitia mipangilio ya programu. Bado chaguo ni lako wewe, na wewe pamoja na wazazi au walezi wako sharti mkubaliane.
 • Wewe na wazazi au walezi wako mnaweza kuratibu vipindi vya mapumziko ambapo huwezi kutumia Instagram. Wazazi au walezi wako wanaweza kuchagua saa mahususi na kupanga wakati wa mapumziko wa kila siku ya juma. Pia tutakujulisha wakati ambapo kipindi cha mapumziko kinawadia.
 • Tumeboresha mchakato wa kuripoti. Unapotoa ripoti kuhusu jambo fulani, sasa unaweza kuongeza maelezo zaidi, kama vile ni nani uliyeripoti na ni katika kategoria gani. Bado utachagua wewe kama utashiriki taarifa hizi na wazazi au walezi wako ama hapana.
 • Wewe na wazazi au walezi wako mnaweza kuwa na mazungumzo ya kimantiki zaidi kuhusu kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwajibika.
  • Wazazi wako wanaweza kuangalia mipangilio ya akaunti yako, kama vile ufaragha, vidhibiti vya maudhui nyeti, na mapendeleo ya kipengele cha jumbe.
  • Wanaweza kuona akaunti ambazo umezuia katika Instagram. Kabla ya mabadaliko haya kufanyika, utapata notisi ya saa 72. Hii inakupa nafasi ya kuzungumza na wazazi wako kisha uamue kama unataka kujiondoa.

Sehemu ya 2: Kuwekwa Kiotomatiki Katika Akaunti za Faragha kwa Walio Chini ya Miaka 16

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tunaamini kwamba kuwa na akaunti za faragha ndiyo njia bora zaidi ya kukaa salama. Kwa kutumia akaunti za faragha, sharti watu watume ombi la kukufuata au kuona au kutoa maoni kwenye maudhui yako — na sharti ukubali maombi hayo kwanza. Ujumbe wowote watakaotuma utaenda kwenye folda yako ya maombi ya jumbe za faragha.

Ikiwa hujatimiza miaka 16 na wewe ni mgeni katika Instagram,chaguomsingi litakuweka kiotomatiki katika akaunti ya faragha. Ikiwa hujatimizamiaka 16 na tayari uko Instagram, tutakutumia (au tayari tumekutumia) arifa ya kukukumbusha kuhusu manufaa ya akaunti ya faragha na kukuhimiza kubadilisha aina ya akaunti yako.

Ni muhimu sana kufikiri kuhusu ufaragha kwa mantiki, hata ikiwa utaamua kutumia akaunti iliyo wazi kwa umma.

Chanzo

familycenter.meta.com/education

End Module

Hongera!
Umekamilisha Moduli


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy