Usalama na Ustawi wa Vijana Mtandaoni

Somo 2: Machaguo ya Kudhibiti Matumizi yako ya Facebook, Messenger, Instagram na WhatsApp

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na mawasilisho ya moduli.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Mjadala

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Ni hatua gani unazochukua ili kuhakikisha kwamba taarifa zako binafsi na ufaragha wako umelindwa wakati unapotumia mtandao na mitandao ya kijamii?
  • Ni tahadhari gani unazochukua unapotengeneza marafiki mtandaoni?
  • Je, umewahi kuzungumza na wazazi au walezi wako kuhusu usalama wa mtandaoni? Ulijifunza nini kutoka kwenye majadiliano hayo?

Sehemu ya 1: Ripoti

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Ukiona kitu unachodhani kwamba hakifai kuwa hapo, iwe umekiona Facebook, Messenger, Instagram au WhatsApp, tungependa kujua kukihusu ili tuchukue hatua. Hiyo ndiyo sababu tumebuni zana za kukuwezesha kuripoti chochote kwa urahisi, kama vile akaunti, chapisho, Hadithi au ujumbe wa faragha. Kipengele cha kuripoti hupatikana katika teknolojia zetu zote na hakimtambulishi anayeripoti.

Sehemu ya 2: Zuia

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Unaweza kumzuia mtu yeyote anayekuudhi katika Facebook na Instagram. Baada ya kufanya hivyo, mtu huyo hataweza tena kutazama picha au video zako au kutafuta wasifu wako. Watu hawajulishwi unapowazuia. Na sasa, unapomzuia mtu, kabla aweze kukuchukiza tena unaweza kuzuia akaunti zozote mpya ambazo mtu huyo anaweza kutengeneza.

Sehemu ya 3: Nyamazisha

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kipengele cha Nyamazisha kilibuniwa ili kukupa fursa ya kupata kipindi cha mapumziko kutoka kwa akaunti unayofuata. Kuna sababu nyingi zinazoweza kukusababisha kuhitaji muda wa mapumziko kutoka kwa akaunti fulani. Unaweza kutumia kipengele cha Nyamazisha ili kuficha machapisho ya Mlisho na Hadithi katika akaunti iliyoteuliwa. Ukiwa tayari, unaweza kulemaza kipengele hicho cha kunyamazisha akaunti hiyo.

Akaunti unayochagua kunyamazisha haitataarifiwa. Chaguo hili la kudhibiti muda wako mtandaoni pia linapatikana katika Facebook kama chaguo la Acha Kufuata/Ficha. Katika WhatsApp, unaweza kunyamazisha gumzo zima.

Sehemu ya 4: Kuzuia

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Zana ya Kuzuia ilibuniwa ili kusaidia kupambana na kudhibiti unyanyasaji wa mtandaoni. Unapomzuia mtu, ni wewe tu na mtu uliyemzuia anayeweza kuona maoni yake mapya katika machapisho yako. Mtu aliyezuiwa pia hataweza kuona ukiwa mtandaoni au kufahamu utakaposoma jumbe zake za faragha.

Kwa kutumia kipengele cha Kuzuia, pia unaweza kudhibiti ni nani anayeweza kukutambulisha katika picha, kukutaja katika Hadithi na kutoa maoni kwenye machapisho yako. Machaguo haya yameundwa ili kukuwezesha kudhibiti jinsi watu wanavyoweza kuingiliana na wewe katika Instagram.

Sehemu ya 5: Ondoa Urafiki

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika Facebook, una chaguo la kuondoa urafiki wa mtu fulani bila mtu huyo kutaarifiwa.

Sehemu ya 6: Taarifa za Usalama

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Taarifa za Usalama katika jumbe zako za faragha zitakutaarifu ikiwa mtu mzima ambaye ana tabia ya kutiliwa shaka anajaribu kuwasiliana na wewe. Kipengele hiki kitakulinda dhidi ya mawasiliano usiyotaka kutoka kwa watu wazima na kukupa uwezo wa kujilinda mwenyewe kwa kukupa chaguo la kuhitimisha mazungumzo, kuzuia, kuripoti au kudhibiti mtu huyo mzima.

Sehemu ya 7: Vidhibiti vya Maudhui Nyeti

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Udhibiti wa Maudhui Nyeti hukusaidia kuchagua wingi au udogo wa maudhui nyeti utakayoona katika chaguo la Tazama Maudhui la akaunti ambazo hufuati. Udhibiti wa Machaguo Nyeti una machaguo 2: Kawaida na Chini. Ikiwa hujatimiza miaka 16 na wewe ni mgeni katika Instagram, chaguomsingi litakuweka kwenye chaguo la Chini.

Ikiwa tayari uko Instagram na hujatimiza miaka 16, tutakutumia arifa ya kukuhimiza uchague chaguo la Chini.

Sehemu ya 8: Vitambulisho na Mitajo

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kando na kuwekwa kiotomatiki katika akaunti ya faragha unapojiandikisha katika Instagram na kuzuia watu wazima usiowafuata wasiweze kukutumia jumbe za faragha, pia unaweza kulemaza uwezo wa watu wa kukutambulisha au kukutaja ikiwa huwafuati. Pia, kwa chaguomsingi, unapojiandikisha kwa mara ya kwanza, watu usiowafuata hawataweza kukujumuisha katika maudhui yao katika Matoleo Mapya ya Video Fupi au Miongozo.

Sehemu ya 9: Dhibiti Anayeweza Kukutumia Jumbe za Faragha

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO
  • Katika Instagram, kila mtu ana uwezo wa kudhibiti ni nani anayeweza kumtumia ujumbe wa faragha. Una chaguo la kuamua ikiwa unaweza kupokea ujumbe kutoka kwa kila mtu au kutoka kwa watu unaowafuata tu. Pia unaweza kuchagua ni nani anayeweza kukuongeza katika gumzo za makundi na ikiwa jumbe za watu usiofuata zitaingia katika folda ya maombi au jumbe hizo zisiwasilishwe kwako kamwe.
  • Katika Messenger, unaweza kuamua ni nani anayeweza kukutumia jumbe na jumbe hizo zitaenda wapi (Orodha ya Gumzo, folda ya Maombi ya Jumbe au jumbe hizo zisiwasilishwe kamwe). Pia unaweza kuchagua kupokea au kutopokea jumbe kutoka kwa watu walio na nambari yako ya simu, marafiki za marafiki zako katika Facebook, akaunti unazofuata au ambazo umeingiliana nazo katika Instagram au wafuasi wako wa Instagram.
  • Katika WhatsApp, unaweza kuamua ni nani anayeweza kukuongeza katika makundi ya WhatsApp. Tumeongeza mipangilio ya ufaragha na mfumo wa mialiko ili kukusaidia kuamua ni nani anayeweza kukuongeza katika makundi. Waasiliani Wangu ni chaguo linalomaanisha kwamba watu waliohifadhiwa kwenye orodha yako ya waasiliani tu ndio wanaoweza kukuongeza katika makundi yao. Waasiliani Wangu Isipokuwa ni chaguo linalokupa udhibiti wa ziada ili kuchagua ni nani kati ya waasiliani anayeweza kukuongeza katika kundi.
    • Ili kuwezesha machaguo haya, unafaa kwenda kwenye kwa Mipangilio, kisha ubofye Akaunti > Ufaragha > Makundi na uteue moja kati ya machaguo haya 3: Kila Mtu, Waasiliani Wangu au Waasiliani Wangu Isipokuwa.
    • Msimamizi wa kundi ambaye hawezi kukuongeza katika kundi kwa sababu ya mipangilio yako atapokea agizo la kukutumia mwaliko wa faragha kupitia gumzo binafsi, na kukupa chaguo la kujiunga na kundi hilo.

Sehemu ya 10: Maneno Fiche

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Maneno Fiche ni kipengele ambacho kimeundwa ili kusaidia kukulinda dhidi ya kupokea jumbe za faragha zinazochukiza. Kipengele hiki kinapowezeshwa, ombi lolote la ujumbe wa faragha lililo na maneno, fungu la maneno au emoji ya kuchukiza litatumwa kiotomatiki kwenye folda ya Maombi Fiche, ili usiwahi kuliona.

Unaweza kutumia orodha yetu ya maneno, fungu la maneno au emoji za kuchukiza ambayo tayari imewekwa au unaweza kutengeneza orodha yako — kwa kuwa tunaelewa kwamba jambo linalomchukiza mtu fulani linaweza kuchukuliwa kwa namna tofauti sana na mtu mwingine. Kipengele hiki pia hufanya kazi kwa maoni, kwa kuficha maoni yanayotumia maneno, fungu la maneno au emoji za kuchukiza.

Sehemu ya 11: Maoni Yaliyobanwa

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Huku tukichukulia kwa uzito jukumu la kusimamia visa hasi mtandaoni, pia tunafikiri kwamba ni muhimu kuangazia visa chanya. Maoni Yaliyobanwa ni kipengele kinachokuruhusu kuchagua maoni chanya kwenye chapisho lako na kulibana ili likae juu ya maoni mengine, na kuweka mfano wa maoni utakaofuatwa na wengine.

Chanzo

familycenter.meta.com

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy