Muhtasari wa Somo
Washiriki wataelewa jinsi ya kuunda hali nzuri ya utumiaji mtandaoni na kulinda ustawi wao wanapokuwa mtandaoni.
Washiriki wataelewa jinsi ya kuunda hali nzuri ya utumiaji mtandaoni na kulinda ustawi wao wanapokuwa mtandaoni.
Tayari?
Anza Somo
Unaweza kuchukua jukumu kubwa katika kukuza mazingira chanya mtandaoni kwa ajili yako na kwa wengine kwa kufanya mambo yafuatayo:
Kabla ya kuchapisha au kusambaza chochote mtandaoni, fikiria jinsi maudhui yako yataathiri sifa yako mtandaoni na kwa wale unaowataja au kuwatambulisha.
Usifikirie tu juu ya matokeo ya haraka lakini pia athari za muda mrefu za kile unachosambaza. Labda unagombana na mtu mtandaoni na unataka kuchapisha maoni ya uchochezi au hasi kuwahusu, lakini fikiria ni nini mwajiri wa siku zijazo anaweza kufikiria ikiwa ataona aina hii ya maudhui kutoka kwako baadaye.
Kama vile ulivyo na mategemeo kuhusu faragha yako, vivyo hivyo na wengine. Watu wengine pia hufanya kazi kukuza na kudumisha umiliki wa utambulisho na sifa zao mtandaoni.
Kwa sababu watu wana uelewa tofauti wa faragha ya kibinafsi na viwango vya faraja wakati wa kusambaza taarifa za kibinafsi mtandaoni, ni muhimu kuzingatia faragha ya watu wengine kabla ya kuchapisha au kusambaza kitu.
Panua mtazamo wako wa ulimwengu kwa kuchunguza mitazamo mbalimbali kuhusu suala au mada, na uepuke kuchapisha au kuchapisha kwa mara nyingine maudhui bila kufikiria athari zake kwa wengine.
Anayekebehi ni mtu kwenye mtandao ambaye anachapisha ujumbe wa uchochezi kimakusudi ili kuanzisha mabishano, mizozo au kuwaudhi wengine. Mkebehi hujaribu kutatiza majadiliano katika maeneo kama vile vyumba vya mazungumzo, sehemu za maoni za makala au tovuti, bodi za majadiliano au machapisho ya mitandao ya kijamii.
Iwapo mtu mwingine ana maoni hasi au ni mkebehi,” usichangamane naye.
Badala yake, tumia zana zinazofaa ndani ya jukwaa kwa ajili ya kuripoti tabia au maudhui yasiyofaa. Tazama Sehemu ya 2: Kushiriki katika majukwaa ya kidijitali kwa maelezo zaidi kuhusu zana mahsusi za kuripoti kwenye jukwaa.
Kuna mambo mengi mazuri ya kujichanganya na wengine mtandaoni. Mitandao ya kijamii inaweza kutuunganisha na watu na vikundi mbalimbali duniani, kutusaidia kuwasiliana na familia, hutusaidia kuendelea kujumuika na jumuiya yetu, ikiwa ni pamoja na kuunda au kutoa maonyo yanayohusu jamii ya karibu, na kujifunza kuhusu mada mpya.
Hata hivyo, ni muhimu kufikiria kuhusu kiasi na ustawi mzuri ili kuhakikisha kuwa una uhusiano mzuri na mitandao ya kijamii na zana zingine za kidijitali.
Kusimamia muda wa kutumia kifaa cha kidijitali
Kusimamia muda wa kutumia kifaa kunaweza kukusaidia kuwa na ustawi mzuri na kuhakikisha kuwa una uhusiano mzuri na teknolojia.
Kuunda mahusiano chanya mtandaoni kunaweza kufanya muda wako mtandaoni kuwa wa maana zaidi. Mifumo mingi ya mtandaoni hutoa zana na nyenzo za kukusaidia katika kufanya hivi.
Programu za mahusiano mtandaoni na majukwaa ya mitandao ya kijamii hurahisisha watu kuungana na kukuza mahusiano. Hakikisha kutengeneza mahusiano chanya. Tumia zana ambazo umejifunza katika Somo la 1 ili kujiweka salama au kukomesha mahusiano kabla hayajawa na matatizo.
Vifaa vya kidijitali huturuhusu sisi kupata taarifa mara kwa mara na kupata kuridhika papo kwa papo. Ni vyema nyakati unazotumia mtandaoni ziwe za kukusudia, chanya na zenye kuhamasisha. Hata hivyo, uwezo wa kujipoteza kabisa katika skrini wakati mwingine unaweza kutuondoa kutoka kwenye wakati uliopo na inaweza kuwa tatizo ikiwa haitatumiwa kwa kiasi.
FOMO ni "woga wa kukosa kitu" Hii ni aina ya wasiwasi wa kijamii unaoweza kutokea unapohisi kuachwa au kuwa na wasiwasi unapoona watu wengine wakichapisha kuhusu matukio ya kusisimua au ya kuvutia kwenye mitandao ya kijamii. Ili kupambana na FOMO, kumbuka kuwa wasifu wa watu kwenye mitandao ya kijamii mara nyingi huratibiwa vyema ili kuwasilisha mambo muhimu kutoka kwenye maisha yao. Unaona sehemu bora zaidi za maisha ya mtu mwingine, sio picha kamili ya maisha yao ya kila siku.
Katika somo la ujuzi wa Vyombo vya Habari, ulijifunza kuhusu watoa maudhui wanaotumia ubadilifu ili kueneza habari potofu. Watu binafsi wanaweza pia kutumia ubadilifu ili kujipa kile kinachoonekana kuwa mabadiliko ya papo kwa papo kidijitali. Hata hivyo, kuona picha zilizohaririwa kunaweza kuathiri hali yetu ya kiakili. Ikiwa unaona kila mara picha zisizo na dosari zinazowasilishwa kama ukweli, zinaweza kusababisha mawazo yenye madhara na kukupa matarajio yasiyo ya kweli kuhusu uzuri wako na taswira yako binafsi.
Mara nyingi mitandao ya jamii hujumuisha vichujio vya kinachoonekana ambavyo hukuruhusu kubadilisha au kuboresha mwonekano wako. Vichujio vinaweza kutumika kwa madhumuni ya kisanii, kujieleza au kujifurahisha. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kutotegemea vichujio ili kujisikia vizuri kuhusu wewe mwenyewe.
Pia kumbuka kuwa watu wengine wanaweza kuwa wakitumia vichujio kila mara ili kuwasilisha taswira yao mahususi. Usijaribu kulinganisha hali yako halisi na hali ya mtu mwingine iliyoratibiwa au iliochujwa.
Hongera!
Umekamilisha Somo
Wanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama Ukurasa