Usalama na Ustawi wa Vijana Mtandaoni

Somo 1: Zana za Usimamizi wa Muda katika Instagram

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na mawasilisho ya moduli.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Mjadala

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Ni kwa namna gani unapata usawa kati ya shughuli zako za mtandaoni na shughuli zisizo za mtandaoni? Je, una mikakati yoyote ya kuzuia kutumia muda mwingi kupita kiasi ukitazama vifaa vyenye skrini?
  • Ni zipi baadhi ya ishara zinazokuonya kwamba huenda unatumia muda mwingi sana mtandaoni, na unazishughulikia vipi?
  • Ni kwa namna gani unakabiliana na msukumo unaoletwa na watu wa rika lako au woga wa kukosa jambo fulani (FOMO) unaohusiana na shughuli za mtandaoni? Je, unahisi msukumo wa kuwa mtandaoni kila mara?

Sehemu ya 1: Tazama Dashibodi ya Shughuli

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Dashibodi ya Shughuli hukuonyesha kiwango cha muda uliotumia katika Instagram kila siku na kila juma. Kwa kugonga na kushikilia miambaa ya rangi ya buluu, unaweza kuona kiasi cha muda ulichotumia katika Instagram siku fulani. Pia kuna chaguo la kutazama muda wako kwa kiwango cha wastani.

Ni rahisi kusahau kutilia maanani muda unapoangalia maudhui katika Instagram. Kwa kutilia maanani kiasi cha muda unachotumia katika Instagram, utakuwa na uwezo zaidi wa kusimamia muda wako vyema zaidi kutoka sasa na kuendelea.

Sehemu ya 2: Weka Kikumbusho cha Kila Siku

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kuweka Kikumbusho cha Kila Siku ni zana nzuri ya kukuarifu unapofikia kikomo cha muda ambao wewe ungetaka kutumia katika Instagram. Unaweza kutumia Dashibodi yako ya Shughuli ili ikuongoze katika kuweka kikomo chako cha wakati cha kila siku. Kuweka kikomo cha kila siku kunaweza kufanya matumizi yako ya Instagram yawe ya kimantiki na yenye maana zaidi.

Sehemu ya 3: Hali Nyamavu

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Hali Nyamavu ni zana katika Instagram inayokuruhusu kunyamazisha arifa kwa kiasi mahususi cha muda uliowekwa. Unaweza kuamua kunyamazisha arifa zako wakati ambapo unasoma, kufanya mazoezi ya masomo yanayofanyiwa nyumbani au wakati unapotaka kutulia saa za usiku.

Wakati muda uliowekwa unapoisha, mipangilio ya arifa zako itarudia hali ya kawaida bila kukuhitaji kuiweka tena mwenyewe.

Sehemu ya 4: Chukua Muda wa Mapumziko

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Chukua Muda wa Mapumziko ni zana inayokuhimiza kuchukua muda wa mapumziko kutoka Instagram ikiwa umekuwa ukitazama maudhui ya mtandao huo kwa muda mrefu. Hii ni tofauti na Vikumbusho vya Kila Siku kwa kuwa kipengele cha Chukua Muda wa Mapumziko huangazia kipindi kimoja tu cha matumizi ya Instagram.

Sehemu ya 5: Miguso

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Miguso ni kipengele kinachokuhimiza kuhakikisha kwamba unatumia muda wako katika Instagram kwa njia yenye manufaa na ya makusudi zaidi. Mguso ni arifa inayoibuka wakati ambapo umekuwa ukirudiarudia kutazama maudhui ya aina moja. Maana ya miguso ni kukusaidia kutazama maudhui mengine mapya. Unaweza kuteua chapisho lililopendekezwa au kutotilia maanani mguso huo. Ikiwa utaamua kuzingatia mguso huo, utaonyeshwa miraba fito mbadala ya machapisho yanayopendekezwa.

Chanzo

familycenter.meta.com/

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy