Uwezeshaji wa Kidijitali

Somo 6: Kuangalia Maadili Yako Binafsi

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Maadili yako binafsi ni muhimu sana kwa lengo lako la maisha. Mambo unayoamini na kuthamini sana maishani huenda yakachangia mwelekeo wa malengo yanayokupa lengo lako la maisha. Huku ukitilia mambo hayo maanani, tumia dakika chache kujaza kitini kinachokuomba kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wa maadili hayo kwako.

Mpe kila mwanafunzi kitini na umuombe akijaze peke yake.

Baada ya wanafunzi kumaliza zoezi hilo, waombe waandike majibu ya maswali yafuatayo kuhusu mambo waliyoweka namba "1" karibu yake (maswali haya pia yameorodheshwa chini ya kitini):

  • Kwa nini maadili haya ni muhimu sana kwako?  Yanaashiria kwamba wewe ni mtu wa aina gani?
  • Yanachangia vipi jinsi unavyoendesha maisha yako ya kila siku?
  • Yanahusiana vipi na mipango yako ya muda mrefu? Je, yanachangia jinsi ambavyo ungependa maisha yako yakumbukwe? Kama ndiyo, kwa njia gani? Kama siyo, kwa nini siyo?
MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wape wanafunzi fursa ya kuzungumza kuhusu mambo waliyoandika au mawazo yao kuhusu mchakato huu baina yao au na darasa zima, ikiwa sio tatizo kwao kufanya hivyo.

Zoezi

(la kufanyiwa darasani au nyumbani)

Waambie wanafunzi watafakari kama zoezi hili lilithibitisha lengo lao la maisha au kama hawana uhakika na lengo lao, je, limewapa vidokezo au mwanga kuhusu lengo lao liweje?

MASUALA YA KUTAFAKARI BAADA YA ZOEZI
  • Ni kwa vipi wanafunzi walilichukulia zoezi hili? Je, waliona ni muhimu kwao katika kuwasaidia kuamua lengo lao liwe lipi?

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Kituo cha The Greater Good Science Center hufanya utafiti wa saikolojia, sosiolojia na sayansi ya nyurolojia na kufunza stadi zinazokuza ustawi, ustahimilivu na huruma katika jamii. Kituo cha GGSC kimejitolea kwa namna ya kipekee katika masuala ya sayansi na taaluma: Hatufadhili tu michakato bunifu ya utafiti wa kisayansi kuhusu ustawi wa kijamii na kihisia, bali pia tunawasaidia watu kutumia utafiti huu katika maisha yao binafsi na taaluma zao. Jifunze zaidi: https://greatergood.berkeley.edu/

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy