Muhtasari wa Somo
Washiriki wataweza kutumia vipengele vya ukaguzi wa usalama kusimamia akaunti zao za mtanådaoni.
Washiriki wataweza kutumia vipengele vya ukaguzi wa usalama kusimamia akaunti zao za mtanådaoni.
Tayari?
Anza Somo
Kitunza nenosiri ni hifadhi ya kidijitali iliyosimbwa kwa njia fiche ambayo huhifadhi taarifa za kuingia kwenye akaunti zako zote za kidijitali. Hii ni Pamoja na programu, wasifu wa mitandao ya kijamii na tovuti zingine. Ili kuongeza usalama zaidi, baadhi ya vitunza nenosiri huwa na vitengeneza nenosiri ili kukusaidia kuunda nenosiri jipya kwa kila akaunti.
Kitengeneza nenosiri ni programu au huduma ambayo huunda kiotomatiki manenosiri madhubuti ili kuhakikisha kuwa unatumia manenosiri ya kipekee kwa kila akaunti. Vitunza nenosiri vingi huwa na kitengeneza nenosiri iliyo ndani ili kukusaidi kuunda nenosiri jipya kwa kila akaunti.
Unapotumia programu ya kutunza nenosiri, bado utahitaji kukariri nenosiri kuu moja ili kuingia kwenye akaunti ya kitunza nenosiri. Hakikisha kuwa unachagua nenosiri kuu ambalo lina nguvu, lakini pia hakikisha umelikariri.
Kumbuka, ikiwa mtu atakisia au kupata nenosiri kuu la akaunti yako ya kitunza nenosiri, basi ataweza kupata manenosiri mengine yote na taarifa binafsi zilizohifadhiwa ndani ya akaunti hiyo.
Kuna baadhi ya hatua ambazo unaweza kuchukua ili kuwa makini katika kudhibiti akaunti zako za mtandaoni. Vifuatavyo, ni vidokezo vya kukusaidia kukaa salama mtandaoni, ikijumuisha udhibiti wa nenosiri, kuwa mwangalifu kuwasiliana na watu usiowajua, kudhibiti maelezo yako binafsi na ukaguzi wa usalama wa akaunti zako za mtandaoni.
Kwa kila akaunti ya mtandaoni, fahamu jinsi ya kubadilisha manenosiri yako na uhakikishe kuwa umeyabadilisha baada ya tukio lolote ambapo yanaweza kuwa yameathirika, ama kwenye akaunti hiyo au nyingine ambayo umetumia taarifa sawa kuingia. Baadhi ya vivinjari vya tovuti vina zana za kukagua nenosiri ili kukusaidia kujua wakati anwani zako za barua pepe na manenosiri yako yameingiliwa katika wizi wa data.
Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kupelekea kuhitaji au kutaka kuwasiliana na watu usiowajua mtandaoni. Kwa mfano, unaweza kutaka kupanga mkutano wa biashara na wateja watarajiwa, kuuza bidhaa, kujifunza kitu kipya kutoka kwa mtaalamu au kuuliza wanajamii wa karibu mapendekezo yao. Unapowasiliana na mtu mpya mtandaoni, ni muhimu kutafuta ishara kwamba akaunti yake ni halali. Wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kutambua kama ni mtu kweli na maelezo yao, hasa kama hamfahamiani moja kwa moja.
Amini hisia zako:
Kusambaza taarifa kupita kiasi ni ufichuaji wa kiasi kisichofaa cha maelezo kuhusu maisha binafsi ya mtu. Ingawa unaweza kutaka kutengeneza utambulisho na sifa chanya mtandaoni, kusambaza taarifa zako kupita kiasi kunaweza kuwa hatari kwa usalama wako mtandaoni na nje ya mtandao.
Ndani ya kila programu au tovuti unayotumia, fahamu ni taarifa gani inaonekana na wengine (kama vile huduma za eneo au programu za watu wengine) na ni nani anayeweza kuona wasifu na machapisho yako.
Kuna zana zinazopatikana kwenye mifumo mingi ya kuripoti mambo kama vile machapisho, wasifu, picha na video.
Baadhi ya mitandao ya kijamii kuhupa uwezo wa kukagua usalama ili kukusaidia katika kuongeza baadhi ya hatua za usalama tulizojifunza katika somo hili, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa kuingia, ulinzi wa nenosiri na uthibitishaji wa njia mbili.
Hongera!
Umekamilisha Somo
Wanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama Ukurasa