Kuchangamana Kidijitali

Somo 7: Utafutaji Unaotumia Picha

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo

Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo


WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Picha na video mnazopata mtandaoni huenda zisiwe za kweli kwa sababu pengine zimefanyiwa mabadiliko kwa njia za kidijitali. Hata hivyo, maudhui ambayo hayajabadilishwa kwa namna za kidijitali pia yanaweza kupotosha ikiwa yameeleweka katika muktadha usiofaa (mfano, yamenaswa katika wakati na/au eneo tofauti na kisa cha habari kinachohusika). Kwa sababu hii, kuthibitisha chanzo cha picha unayoona katika mitandao ya kijamii huhusisha kubaini ikiwa ni sahihi na katika muktadha unaofaa.

Njia muhimu za kuthibitisha asili na pengine chanzo, tarehe na eneo ambalo picha ilipigwa inafahamika kama Injini ya Utafutaji Unaotumia Picha.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mnadhani injini ya utafutaji unaotumia picha hufanya kazi vipi?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Injini ya Utafutaji Unaotumia Picha huwawezesha watumiaji kutafuta taarifa mtandaoni wakitumia picha badala ya maneno muhimu.

Injini ya utafutaji huanza kwa kukusanya mabilioni ya picha zilizo mtandaoni katika hifadhidata yake. Kwa kutazama taarifa kama vile jina la faili ya picha na metadata, hifadhidata ya injini ya utafutaji inaweza kupanga picha katika kielezo kikubwa, sawia na kielezo kilicho kwenye upande wa nyuma wa kitabu cha kisa halisi. Unapopakia faili ya picha au kuweka URL ya picha, injini ya utafutaji huchambua picha zilizo kwenye kielelezo ili kukupa matokeo yanayolingana zaidi na utafutaji wako. Injini ya utafutaji hulinganisha picha yako na mabilioni ya picha zingine zilizo katika hifadhidata yake, ili uweze kutambua ikiwa kuna picha zinazofanana nayo kwenye mtandao na lini na pahali ambapo picha hiyo imechapishwa.

Wanahabari wakati mwingine hutumia injini ya utafutaji unaotumia picha kama huduma ya Utafutaji wa Google Unaotumia Picha [https://images.google.com/] au TinEye [https://www.tineye.com/] kama hatua ya kwanza kabisa katika mchakato wa uthibitishaji. Kuthibitisha chanzo ukitumia injini ya utafutaji unaotumia picha huenda kukafichua kwamba picha unayotazama ilipakiwa kabla ya kutokea kwa kisa fulani, au kwamba picha hiyo tayari ilikuwa imehusishwa na muktadha tofauti. Injini tofauti za utafutaji huenda zikatoa matokeo tofauti, lakini utafutaji mzuri unaotumia picha huenda ukapata chanzo halisi cha picha. Sio picha zote za uongo au zilizochukuliwa katika muktadha usiofaa zinaweza kupatikana na injini ya utafutaji unaotumia picha, lakini bado injini za aina hiyo ni zana nzuri sana za uthibitishaji.

DONDOO ZA MWALIMU

Onesha video ya Common Sense Education ya "Jinsi ya Kutumia Utafutaji wa Google Unaotumia Picha ili Kuhakiki Uhalisia wa Picha" ili kuonesha jinsi ya kutumia Utafutaji wa Google Unaotumia Picha. Wajulishe washiriki kwamba pia wanaweza kupakia picha katika injini za utafutaji unaotumia picha. Pia wanaweza kuchuja matokeo ya utafutaji kwa kubofya Njia (chini ya mwambaa wa utafutaji kwenye upande wa kulia), kubofya Wakati, na kuchagua muda mahususi uliowekwa au kuweka kipindi cha wakati kwa tarehe.

Kwa picha za kurejelea, tafadhali angalia hapa chini:
pbs.org/newshour/extra/daily-videos/why-is-itimportant-for-news-sources-to-be-trustworthy

PICHA YA MAZUNGUMZO YA DARASANI

Sasa, utakuwa na nafasi ya kuona jinsi injini ya utafutaji unaotumia picha inavyofanya kazi kwa kutumia picha utakayotumia. Tumia kompyuta au simu yako ya mkononi kupiga picha. Tafadhali zingatia masuala ya siri: tunapendekeza upige picha ya chombo au eneo ambalo halioneshi maelezo yako binafsi au ya mtu mwingine.

Pakia picha hii katika huduma ya Utafutaji wa Google Unaotumia Picha au TinEye kisha ukague matokeo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Umepata matokeo gani?
  • Matokeo yalikuwa kama ulivyotarajia?
  • Kwa nini au kwa nini siyo?

Zoezi 

Sehemu ya 1

DONDOO KWA MWALIMU
Onesha video ya First Draft ya "Kufanya Utafutaji Unaotumia Picha kwa Kutumia TinEye" ili kuonyesha jinsi ya kutumia TinEye
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Wanahabari wataalamu hukumbana na changamoto za kipekee za uthibitishaji wanaposhughulika na hali zinazoibua habari za hivi punde kama ajali, majanga ya asili, na matukio yanayoendelea ambayo yanavutia sana vyombo vya habari.

Picha na video zinazohusiana na matukio haya huenea kwa kasi na inaweza kuwa vigumu kufikia na kuwasiliana na vyanzo vyake, hasa vile ambavyo hubaki katika eneo lililoathiriwa. Msukumo mkubwa wa kuripoti haraka kuhusu matukio yanayoibuka, pia uwepo mkubwa wa zana za kuhariri picha, ambao unaweza kufanya wapokezi wa habari, na hata wanahabari wataalamu, kuchapisha au kusambaza taarifa zisizokuwa sahihi.

Sehemu ya 2

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tumia injini ya utafutaji unaotumia picha ya TinEye kupitia tineye.com ili kutambua chanzo cha picha iliyo kwenye kiunganishi kilicho katika slaidi. Chunguza ikiwa kuna picha zinazofanana na picha ya papa wa Afrika Kusini na uangalie kama zinalingana na kipindi ambacho picha halisi ilipopigwa.

Baada ya kuthibitisha chanzo cha picha hiyo, andika aya ukieleza kwa nini ni muhimu kuthibitisha uhalisia wa picha zinazosambazwa mtandaoni.

Washiriki wanaweza kuichukua picha ya papa wa Afrika Kusini na kuipakia katika TinEye. Kuchuja matokeo kwa tarehe ya zamani zaidi kunaweza kuonesha kwamba picha hiyo ilichapishwa katika machapisho mengi. Cha kusikitisha ni kuwa, tovuti za mitandao ya kijamii huondoa metadata za picha halisi na hivyo basi hatuwezi kuweka picha hii katika kitazamaji cha data za EXIF ili kuchunguza kama ndiyo picha halisi. Mwanahabari anaweza kuamua kuwasiliana na watu wanaochapisha picha katika mitandao ya kijamii ili kuthibitisha ikiwa picha hii kweli ndiyo picha halisi.

DONDOO KWA MWALIMU

Mfano huu unalenga kuwawezesha wanafunzi kufikiria kwa makini kuhusu picha wanazoona na kujifunza kuhusu jinsi ya kuthibitisha kama ni za kweli au la. Ingawa mfano wa papa kutoka Afrika Kusini unafaa sana kwa kuonesha mfano wa nakala, tunakuhimiza utumie picha au video ambayo inatambulika na wanafunzi wako. Ikiwa kuna mfano wa eneo lenu ambao wanafunzi wako wanautambua zaidi, tunapendekeza kwamba utumie mfano huo.

Mjadala

Sehemu ya 1

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Waombe washiriki wawageukie watu waliokaa karibu yao ili wajadili maswali haya katika makundi ya watu wawili wawili.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mlitumia mbinu gani kupata picha halisi iliyochapishwa na chanzo cha picha hiyo?
  • Ni kwa kiasi gani mlikaribia kufanikiwa kufanya hivyo? Mna uhakika gani kwamba picha mliyopata ndiyo halisi?
  • Chanzo chake ni nani?

Sehemu ya 2

DONDOO ZA MWALIMU

Kusanyikeni nyote katika kundi kubwa na uwaombe washiriki wateue wenzao waliotumia mbinu nzuri au zisizo za kawaida kupata asili na chanzo cha picha hiyo. Jadilianeni katika kundi zima.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mnapotumia injini ya utafutaji unaotumia picha, mnafahamu vipi ikiwa matokeo ya zamani zaidi katika injini ya utafutaji ndiyo yanayoonesha picha halisi?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Hamuwezi kuchukulia tu kwamba matokeo ya zamani zaidi ya injini ya utafutaji unaotumia picha ndiyo yanayoonesha picha halisi ya tukio fulani. Matokeo huenda yakawa tofauti kati ya injini moja ya utafutaji na nyingine, na matokeo ya zamani na/au picha yenyewe halisi huenda isiwe katika matokeo hayo ya utafutaji. Njia bora zaidi ya kuthibitisha uhalisia wa picha ni kutumia mbinu za utafutaji unaotumia picha kwa pamoja na mbinu zingine za uthibitishaji. Kwa mfano, unaweza kurejelea machapisho mengine ambapo picha hiyo imechapishwa ili kukusaidia kupata na kuwasiliana na chanzo halisi. Kupata njia mbalimbali za kuthibitisha uhalisia wa picha ya tukio fulani na asili na chanzo chake kunaweza kukusaidia kuhakikisha kwamba unaendesha mchakato wa uthibitishaji vizuri zaidi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Hivi sasa hakuna injini za utafutaji unaotumia video. Unawezaje kutumia injini ya utafutaji unaotumia picha ili kukusaidia kuthibitisha uhalisia wa video? Kwa sasa, unaweza kuchukua picha ya sehemu ya video hiyo yenye upekee na kuweka picha hiyo katika injini ya utafutaji unaotumia picha ili kuona ikiwa kuna picha zingine za nyuma zinazofanana na picha hiyo.

Cha kusikitisha ni kwamba mbinu hii hutegemea sana picha ya skrini ya sehemu ya video hiyo ambayo utaamua kuitumia. Video ni mkusanyiko wa picha zinazooneshwa kwa mfululizo wa kasi (mfano, fremu 24 kwa kila sekunde). Kwa sababu hii, faili za video zina data nyingi, ambazo injini za utafutaji unaotumia picha haziwezi kuchakata kwa sasa.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mnadhani ni kwa nini picha za ajabu kama hizi husambazwa sana wakati wa habari za hivi punde?
  • Je, mmesambaza aina hizi za picha au video hapo kabla? Kwa nini/kwa nini siyo?
  • Je, kwa nini mnadhani ni muhimu kuthibitisha uhalisia wa picha na video zinazosambazwaa katika mitandao ya kijamii wakati wa habari za hivi punde?
DONDOO ZA MWALIMU

Jadilianeni katika kundi zima.

NYENZO

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy