Kuchangamana Kidijitali

Somo 5: Aina za Matini za Vyombovya Habari

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Hapo nyuma mlijifunza kuhusu orodha ya ukaguzi yenye hatua tano za uthibitishaji ambazo wanahabari wataalamu huzitumia wanapohitaji kuthibitisha picha au video. (Pamoja na wanafunzi, pitia kwa haraka vile vipengele vitano vya Orodha ya Ukaguzi ya Uthibitishaji.)

  • Chanzo: Je, unaangalia chanzo cha maudhui?
  • Chanzo: Ni nani aliyetengeneza maudhui hayo?
  • Tarehe: Maudhui hayo yalichukuliwa/yalirekodiwa lini?
  • Eneo: Maudhui hayo yalichukuliwa/yalirekodiwa wapi?
  • Ari: Maudhui hayo yalichukuliwa/yalirekodiwa kwa sababu gani?

Leo, tutazungumza kuhusu vipengele viwili vya kwanza vya orodha hiyo ya ukaguzi: asili na chanzo. Katika mazingira ya sasa ya ubadilishanaji wa habari, watu wanabuni, wanasambaza na kuyafanyia maudhui mabadiliko kila wakati, hasa katika mitandao ya kijamii. Wanahabari na watu wanaopokea habari hizo wanaweza kutumia zana mbalimbali ili kuthibitisha uhalisia wa picha au video na kubaini ikiwa imetumiwa katika muktadha unaofaa. Hii ndiyo sababu tunachukulia uthibitishaji kuwa mchakato — kwa sababu kuthibitisha uhalisia wa maudhui huhusisha hatua nyingi na wakati mwingine huchukua muda mrefu kukamilisha. Changamoto moja ambayo watu hupitia wanapothibitisha uhalisia wa maudhui ni kwamba picha na video huenea kutoka tovuti moja hadi nyingine na kwa urahisi, yanaweza kufanyiwa mabadiliko, kunakiliwa na kueleweka vibaya.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Je, mmewahi kunakili picha au video kutoka kwenye tovuti moja na kuisambaza katika tovuti nyingine?
  • Je, mmewahi kuchapisha maudhui ambayo marafiki zenu walishiriki nanyi, katika tovuti tofauti?
  • Je, mmewahi kufuta maudhui fulani kisha mkayachapisha tena baadaye?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Nakala za maudhui ni maudhui ambayo hunakiliwa kutoka kwenye maudhui halisi na wakati mwingine zinahamishwa kutoka kwenye mfumo mmoja hadi mwingine. Neno hilo linatokana na kitendo cha "kunakili" na maana yake ni maudhui yanayonakiliwa na mtumiaji ili kubuni toleo jipya la maudhui hayo.

(Nakala pia hujulikana kama matoleo ya aina za matini za vyombo vya habari. Ikiwa wewe/wanafunzi wako wangependa kupata nyenzo zaidi kuhusu nakala za maudhui mtandaoni, mnaweza kutumia maneno haya mengine. Kwingineko katika mafunzo haya, tumeamua kuita nakala kwa jina "nakala (matoleo)" ili kuonesha wingi wa maneno hayo.

Fikiria kwamba unasambaza picha uliyopiga kwenye mfumo wa kutuma ujumbe binafsi, kama Snapchat au WhatsApp, kisha mmoja wa marafiki zako aichukue picha hiyo kisha aichapishe katika mtandao ulio wazi kwa umma kama Twitter. Hebu tuseme kwamba mwanahabari ameiona picha iliyochukuliwa na rafiki yako na angependa kujua aliyepiga picha halisi.

Hiari: Waombe wanafunzi wawageukie watu waliokaa karibu yao ili wayajadili maswali haya katika makundi ya watu wawili wawili.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mwanahabari huyo anaweza kujua vipi kwamba wewe ndiye uliyepiga picha halisi?
  • Vipi kama chapisho la rafiki yako litakuwa maarufu zaidi na lisambazwe na watu wengine 50? Mwanahabari huyo atajua vipi mtu aliyepiga picha halisi? (Mwanahabari huyo anaweza kuwasiliana na rafiki yako na kumuuliza kama ndiye aliyeipiga picha hiyo. Ikiwa mwanahabari huyo amepata nakala (matoleo) nyingi za picha hiyo, anaweza kuangalia tarehe ambayo kila nakala ilichapishwa na kujaribu kuwasiliana na mtu aliyechapisha nakala ya kwanza.)
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Nakala (matoleo) zinaweza kuleta matatizo wakati wa habari za hivi punde kwa sababu taarifa zinaweza kuenea kwa kasi sana na inaweza kuwa vigumu kufahamu ni nani aliyetengeneza taarifa halisi na wakati ilipotengenezwa. Katika tovuti kama YouTube, watu wengine watapakua video halisi ya habari fulani kisha kuipakia tena haraka wakitumia jina tofauti la mtumiaji, huku wakitumaini kuchuma pesa (First Draft). "Wakati mwingine unaweza kuona mamia ya (matoleo) video ileile katika saa chache baada ya habari za hivi punde" (First Draft).

Unapoona maudhui fulani kwa mara ya kwanza, huwezi kuchukulia tu kwamba ndiyo halisi. Tafuta vidokezo kama hivi vinavyofuata ambavyo vinaweza kukufahamisha kama picha au video hiyo ndiyo halisi:

  • Nakala (matoleo) kwa kawaida huwa na ubora wa chini wa picha au video ikilinganishwa na picha au video halisi. Pia zinaweza kuwa na faili zenye ukubwa mdogo au vipimo visivyo vya kawaida (jambo linaloashiria kwamba maudhui hayo huenda yamebadilishwa kutoka katika maudhui halisi).
  • Angalia akaunti ya mtu aliyechapisha picha au video hiyo. Je, huwa wanasambaza nakala (matoleo) mengine ya habari za hivi punde? Hiyo inamaanisha kwamba kuna uwezekano kuwa yeye siye aliyechukua picha/video hiyo.
  • Je, picha au video hiyo imetoka katika tovuti ya shirika? Mashirika "wakati mwingine yanaweza kusambaza upya maudhui ambayo yalisambazwa na mtu aliyeshuhudia tukio fulani" (First Draft).
  • Mwisho, zingatia silika yako. Je, kuna uwezekano kwamba mtu huyu alikuwa katika eneo la tukio hilo na anasambaza video halisi?

Zoezi

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Ingia mtandaoni kisha utafute picha ya habari za hivi sasa inayokuvutia. Tafiti chanzo cha picha hiyo. Tengeneza nakala ya picha hiyo kisha uisambaze kwenye mojawapo ya akaunti zako za mitandao ya kijamii. Unapochapisha picha hiyo, unaweza kuifanyia mabadiliko kwa namna yoyote (mfano, kuhariri, kukata, kuongeza matini) kabla ya kuisambaza.

Unapochapisha picha hiyo, hakikisha umebaini chanzo chake halisi.

Baadaye, andika aya fupi inayojibu maswali yafuatayo:

  • Je, ni picha gani uliyoamua kusambaza na kwa nini?
  • Wapi na nani ambaye ulisambaziana naye picha?
  • Je, uliamua kuifanyia mabadiliko (mfano, kuhariri, kukata, kuongeza matini) picha hiyo kwa namna yoyote kabla ya kuisambaza? Je, ulikuwa na nia gani kufanya/kutofanya mabadiliko kwenye picha hiyo?
  • Je, unadhani chapisho lako lingepokelewa kwa njia tofauti kama usingesema chanzo halisi cha picha hiyo? Kwa nini au kwa nini siyo?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Mgeukie mtu aliye karibu yako. Mwoneshe picha uliyochapisha na umpe maelezo mafupi kuhusu sababu yako ya kuchagua picha hiyo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Je, ni zipi baadhi ya sababu ambazo zinazoweza kuwafanya watu waamue kusambaza tena maudhui mtandaoni?
  • Fikiria kuhusu nakala (matoleo) nyingine maarufu ambazo umeona watu wamezisambaza mtandaoni. Je, kuna hali ambapo kutambua chanzo cha maudhui ni muhimu zaidi/kidogo kuliko hali nyingine? Zungumzia mifano kadhaa na darasa zima na mjadili ikiwa ina madhara au la.

Mjadala

MAZUNGUMZO YA DARASANI YA VIDEO

Katika mazingira ya sasa ya upashanaji wa habari, picha au video yoyote inaweza kuchukuliwa, kufanyiwa mabadiliko au kusambazwa na mtu yeyote anayeweza kuipata intaneti na kompyuta au simu ya mkononi. Katika hali nyingine, maudhui husika yanaweza kuonwa na watu wengi sana na kufanyiwa mabadiliko tena na tena kiasi kwamba inakuwa vigumu sana kutambua picha halisi. Hali hii inaweza kuonekana hasa wakati ambapo nakala (matoleo) zinakuwa picha maarufu za kuchekesha.

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Angalia picha ya mwendeshaji kayaki na papa iliyo katika kiunganishi kilicho hapa chini: https://www.nationalgeographic.com/animals/article/great-white-shark-meme-news-photography-animals-peschak

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Picha za mwendeshaji kayaki na papa zilienea sana baada ya kuchapishwa kwa mara ya kwanza na magazeti ya Afrika Kusini. Matoleo mengine ya picha hiyo yamesambazwa tena mtandaoni, wakati mwingine hata bila kutambulisha chanzo halisi.

Baadhi ya nakala (matoleo) hizi zimegeuzwa kuwa picha maarufu za kuchekesha ambazo zimetumiwa katika machapisho makuu. Hata hivyo, mara nyingi picha hizi za kuchekesha zinahitaji uelewa wa kiasi fulani wa muktadha halisi. Kwa sababu hii, watu wanaoona picha za kuchekesha za mwendeshaji kayaki na papa huenda wazisielewe kikamilifu ikiwa hawajui muktadha wa picha halisi.

DONDOO KWA MWALIMU

Mfano huu unalenga kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi ya kuthibitisha nakala za picha kwa kufuata hatua za uthibitishaji. Ingawa mfano wa papa kutoka Afrika Kusini unafaa sana kwa kuonesha mfano wa nakala, tunakuhimiza utumie picha au video ambayo inatambulika na wanafunzi wako. Ikiwa kuna mfano wa eneo lenu ambao wanafunzi wako wanautambua zaidi, tunapendekeza kwamba utumie mfano huo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Fikiria kuhusu nakala (matoleo) maarufu ambazo zimekuwa picha za kuchekesha. Je, una zozote unazopenda?
  • Unafahamu chanzo halisi cha picha hiyo ya kuchekesha? Vipi kuhusu muktadha halisi?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Taarifa za picha, kuliko maandishi tu, zimebuniwa ili kuwavutia watu kwenye mitandao ya kijamii. Kama mpokezi wa habari mwenye kuwajibika, unaweza kuamua jinsi unavyotaka kuingiliana, kusambaza au kuyafanyia maudhui mabadiliko vizuri zaidi, ambayo unaona marafiki, jamaa na watu wengine wakichapisha mtandaoni.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Kwa mujibu wa mambo mliyojifunza leo kuhusu nakala (matoleo), mtachukulia vipi nakala na picha za kuchekesha mtakazoona katika siku zijazo?
NYENZO

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy