Muhtasari wa Somo
Washiriki watajifunza kuhusu jinsi vijana wanaweza kusimamia muda wao mtandaoni na kutumia zana zinazowahimiza kutumia muda wao kwa njia chanya na za kimakusudi zaidi katika mitandao ya kijamii.
Washiriki watajifunza kuhusu jinsi vijana wanaweza kusimamia muda wao mtandaoni na kutumia zana zinazowahimiza kutumia muda wao kwa njia chanya na za kimakusudi zaidi katika mitandao ya kijamii.
Tayari?
Anza Somo
Dashibodi ya Shughuli hukuonyesha kiwango cha muda uliotumia katika Instagram kila siku na kila juma. Kwa kugonga na kushikilia miambaa ya rangi ya buluu, wanaweza kuona kiasi cha muda ulichotumia katika Instagram siku fulani. Pia kuna chaguo la kutazama muda wao kwa kiwango cha wastani.
Ni rahisi kusahau kutilia maanani muda unapoangalia maudhui katika Instagram. Kwa kuwafahamisha kiasi cha muda ambao vijana wanatumia katika Instagram, watakuwa na uwezo zaidi wa kusimamia muda wao vyema zaidi kutoka sasa na kuendelea.
Kuweka Kikumbusho cha Kila Siku ni zana nzuri ya kuarifu vijana wanapofikia kikomo cha muda ambao wangetaka kutumia katika Instagram. Unaweza kuzungumza na kijana wako kuhusu umuhimu wa kuweka mipaka na jinsi wanavyoweza kutumia Dashibodi ya Shughuli ili kuweka kikomo chao cha muda cha kila siku. Kuweka kikomo cha kila siku kunaweza kufanya matumizi yao ya Instagram yawe ya kimantiki na yenye maana zaidi.
Hali Nyamavu ni zana katika Instagram inayokuruhusu kunyamazisha arifa kwa kiasi mahususi cha muda uliowekwa. Vijana wanaweza kuamua kunyamazisha arifa zao wakati ambapo wanasoma, kufanya mazoezi ya masomo yanayofanyiwa nyumbani au wakati wanapotaka kutulia saa za usiku.
Wakati muda uliowekwa unapoisha, mipangilio ya arifa zao itarudia hali ya kawaida bila kuwahitaji kuiweka tena wenyewe.
Chukua Muda wa Mapumziko ni zana inayohimiza vijana kuchukua muda wa mapumziko kutoka Instagram ikiwa wamekuwa wakitazama maudhui ya mtandao huo kwa muda mrefu. Hii ni tofauti na Vikumbusho vya Kila Siku kwa kuwa kipengele cha Chukua Muda wa Mapumziko huangazia kipindi kimoja tu cha matumizi ya Instagram.
Miguso ni kipengele kinachohimiza vijana kuhakikisha kwamba wanatumia muda wao katika Instagram kwa njia yenye manufaa na ya makusudi zaidi. Mguso ni arifa inayoibuka wakati ambapo wamekuwa wakirudiarudia kutazama maudhui ya aina moja. Maana ya miguso ni kuwasaidia kutazama maudhui mengine mapya. Vijana wanaweza kuteua chapisho lililopendekezwa au kutotilia maanani mguso huo. Ikiwa wataamua kuzingatia mguso huo, wataonyeshwa miraba fito mbadala ya machapisho yanayopendekezwa.
Hongera!
Umekamilisha Somo
Wanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.

Tazama Ukurasa