Somo 2: Zana za vijana za Kudhibiti Matumizi yao ya Facebook, Messenger, Instagram na WhatsApp
Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na mawasilisho ya moduli.
Muhtasari wa Somo
Katika muda wa miaka michache iliyopita, tumeunda vipengele vingi vilivyobuniwa ili kusaidia watu wote — ikiwa ni pamoja na vijana — ili waweze kupata udhibiti zaidi wa matumizi yao. Hii ni pamoja na kudhibiti ni nani anayeweza kuwasiliana nao au kutoa maoni kwenye machapisho yao na aina ya lugha ambayo wangependa kuona. Zana nyingi kati ya hizi zilibuniwa kutokana na maoni ya moja kwa moja ya vijana.
Sehemu ya 1: Ripoti
Kijana akiona kitu anachodhani kwamba hakifai kuwa hapo, iwe amekiona Facebook, Messenger, Instagram au WhatsApp, tungependa kujua kukihusu ili tuchukue hatua. Hiyo ndiyo sababu tumebuni zana za kuwezesha mtu yeyote kuripoti chochote kwa urahisi, kama vile akaunti, chapisho, Hadithi au ujumbe wa faragha. Kipengele cha kuripoti hupatikana katika teknolojia zetu zote na hakimtambulishi anayeripoti.
Sehemu ya 2: Zuia
Vijana wanaweza kuzuia mtu yeyote anayewaudhi katika Facebook na Instagram. Baada ya kufanya hivyo, mtu huyo hataweza tena kutazama picha au video zao au kutafuta wasifu wao. Watu hawajulishwi wakati vijana wanawazuia. Na sasa, vijana wanapomzuia mtu, kabla aweze kuwachukiza tena wanaweza kuzuia akaunti zozote mpya ambazo mtu huyo anaweza kutengeneza.
Sehemu ya 3: Nyamazisha
Kipengele cha Nyamazisha kilibuniwa ili kuwapa vijana fursa ya kupata kipindi cha mapumziko kutoka kwa akaunti wanayofuata. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha vijana kuhitaji muda wa mapumziko kutoka kwa akaunti fulani. Wannaweza kutumia kipengele cha Nyamazisha ili kuficha machapisho ya Mlisho na Hadithi katika akaunti iliyoteuliwa. Wakiwa tayari, wanaweza kulemaza kipengele hicho cha kunyamazisha akaunti hiyo.
Akaunti wanayochagua kunyamazisha haitataarifiwa. Chaguo hili la kudhibiti muda wao mtandaoni pia linapatikana katika Facebook kama chaguo la Acha Kufuata/Ficha. Katika WhatsApp, wanaweza kunyamazisha gumzo zima.
Sehemu ya 4: Kuzuia
Zana ya Kuzuia ilibuniwa ili kusaidia kupambana na kudhibiti unyanyasaji wa mtandaoni. Vijana wanapomzuia mtu, ni wao tu na mtu waliyemzuia anayeweza kuona maoni yake mapya katika machapisho yao. Mtu aliyezuiwa pia hataweza kuona wakiwa mtandaoni au kufahamu watakaposoma jumbe zake za faragha.
Kwa kutumia kipengele cha Kuzuia, pia vijana wanaweza kudhibiti ni nani anayeweza kuwatambulisha katika picha, kuwataja katika Hadithi na kutoa maoni kwenye machapisho yao. Machaguo haya yameundwa ili kuwezesha vijana kudhibiti jinsi watu wanavyoweza kuingiliana nao katika Instagram.
Sehemu ya 5: Ondoa Urafiki
Katika Facebook, vijana wana chaguo la kuondoa urafiki wa mtu fulani bila mtu huyo kutaarifiwa.
Sehemu ya 6: Taarifa za Usalama
Taarifa za Usalama katika jumbe za faragha zitataarifu vijana ikiwa mtu mzima ambaye ana tabia ya kutiliwa shaka anajaribu kuwasiliana nao. Kipengele hiki kitawalinda vijana dhidi ya mawasiliano wasiyotaka kutoka kwa watu wazima na kuwapa uwezo wa kujilinda wenyewe kwa kuwapa chaguo la kuhitimisha mazungumzo, kuzuia kuripoti au kumzuia mtu huyo mzima.
Sehemu ya 7: Vidhibiti vya Maudhui Nyeti
Udhibiti wa Maudhui Nyeti huwasaidia vijana kuchagua wingi au udogo wa maudhui nyeti watakayoona katika chaguo la Tazama Maudhui la akaunti ambazo hawafuati. Udhibiti wa Machaguo Nyeti una machaguo 2: Kawaida na Chini.
Ikiwa kijana wako hajatimiza miaka 16 na ni mgeni katika Instagram, chaguomsingi litamweka kwenye chaguo la Chini kiotomatiki. Ikiwa tayari yuko katika Instagrama na hajatimiza miaka 16, atapokea agizo linalomhimiza kuteua chaguo la Chini.
Sehemu ya 8: Vitambulisho na Mitajo
Kando na kuweka vijana kiotomatiki katika akaunti za faragha wanapojiandikisha katika Instagram na kuzuia watu wazima wasiowafuata wasiweze kuwatumia jumbe za faragha, pia wanaweza kulemaza uwezo wa watu wa kuwatambulisha au kuwataja ikiwa hawawafuati. Pia, kwa chaguomsingi, wanapojiandikisha kwa mara ya kwanza, watu wasiwaofuata hawataweza kuwajumuisha katika maudhui yao katika Matoleo Mapya ya Video Fupi au Miongozo.
Sehemu ya 9: Dhibiti Anayeweza Kutumia Vijana Jumbe za Faragha
- Katika Instagram, kila mtu ana uwezo wa kudhibiti ni nani anayeweza kumtumia ujumbe wa faragha. Kila mtu ana chaguo la kuamua ikiwa angependa kupokea jumbe za faragha kutoka kwa kila mtu au watu anaowafuata tu. Pia wanaweza kuchagua ni nani anayeweza kuwaongeza katika gumzo za makundi na ikiwa jumbe za watu wasiowafuata zitaingia katika folda ya maombi au kamwe jumbe hizo zisiwasilishwe kwao.
- Katika Messenger, vijana wanaweza kuamua ni nani anayeweza kuwatumia jumbe na jumbe hizo zitaenda wapi (Orodha ya Gumzo, folda ya Maombi ya Jumbe au jumbe hizo zisiwasilishwe kamwe). Pia wanaweza kuchagua kupokea au kutopokea jumbe kutoka kwa watu walio na nambari zao za simu, marafiki za marafiki zao katika Facebook, akaunti wanazofuata au ambazo wameingiliana nazo katika Instagram au wafuasi wao wa Instagram.
- Katika WhatsApp, wanaweza kuamua ni nani anayeweza kuwaongeza katika makundi ya WhatsApp. Tumeongeza mipangilio ya ufaragha na mfumo wa mialiko ili kuwasaidia kuamua ni nani anayeweza kuwaongeza katika makundi. Waasiliani Wangu ni chaguo linalomaanisha kwamba watu waliohifadhiwa kwenye orodha yao ya waasiliani tu ndio wanaoweza kuwaongeza katika makundi yao. Waasiliani Wangu Isipokuwa ni chaguo linalokupa udhibiti wa ziada ili kuchagua ni nani kati ya waasiliani anayeweza kuwaongeza katika kundi.
-
- Ili kuwezesha machaguo haya, vijana wanafaa kwenda kwenye kwa Mipangilio, kisha wabofye Akaunti > Ufaragha > Makundi na wateua moja kati ya machaguo haya 3: Kila Mtu, Waasiliani Wangu au Waasiliani Wangu Isipokuwa.
- Msimamizi wa kundi ambaye hawezi kuwaongeza katika kundi kwa sababu ya mipangilio yao atapokea agizo la kuwatumia mwaliko wa faragha kupitia gumzo binafsi, na kuwapa chaguo la kujiunga na kundi hilo. Sehemu ya 10: Maneno Fiche
Sehemu ya 10: Maneno Fiche
Maneno Fiche ni kipengele ambacho kimeundwa ili kusaidia kulinda vijana dhidi ya kupokea ujumbe wa faragha unaochukiza. Kipengele hiki kinapowezeshwa, ombi lolote la ujumbe wa faragha lililo na maneno, fungu la maneno au emoji ya kuchukiza litatumwa kiotomatiki kwenye folda ya Maombi Fiche, ili vijana wasiwahi kuliona.
Wanaweza kutumia orodha yetu ya maneno, fungu la maneno au emoji za kuchukiza ambayo tayari imewekwa au wanaweza kutengeneza orodha yao — kwa kuwa tunaelewa kwamba jambo linalomchukiza mtu fulani linaweza kuchukuliwa kwa namna tofauti sana na mtu mwingine. Kipengele hiki pia hufanya kazi kwa maoni, kwa kuficha maoni yanayotumia maneno, fungu la maneno au emoji za kuchukiza.
Sehemu ya 11: Maoni Yaliyobanwa
Huku tukichukulia kwa uzito jukumu la kusimamia visa hasi mtandaoni, pia tunafikiri kwamba ni muhimu kuangazia visa chanya. Maoni Yaliyobanwa ni kipengele kinachoruhusu vijana kuchagua maoni chanya kwenye chapisho lao na kulibana ili likae juu ya maoni mengine, na kuweka mfano wa maoni utakaofuatwa na wengine.
Chanzo
familycenter.meta.com
Hongera!
Umekamilisha Somo
Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Get Safe Online and Digital Promise chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0.