Kuchangamana Kidijitali

Somo 1: Heshima na Mipaka

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Kuelewa na Kushiriki Hisiaza Wengine

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Waambie wanafunzi wajigawe katika makundi ya watu wawili wawili kisha umpe kila mwanafunzi nakala ya kitini cha "Kuelewa na Kuheshimu Hisia za Wengine". Wape wanafunzi dakika 15 ili wasome na kujadili matukio hayo. Zunguka katika darasa hilo na uwasaidie wanafunzi kwa kutumia nyenzo za ziada za mwalimu zilizo kwenye kitini.

DONDOO ZA MWALIMU
Kitini hiki kinalenga kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kutafakari kwa kina kuhusu tabia zao za mtandaoni na namna matendo yao huwagusa wengine. Majina yaliyo kwenye vitini yanaweza kubadilishwa ili yaendane na majina yanayotumika sana katika eneo unalofundisha. Kwa mfano:

  • Ethiopia: Dawitt, Yacob au Hiwot
  • Kenya: Cherono, Mwita au Masese
  • Zambia: Abigail, Mary au Yonah

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Matukio haya yanafanana kwa vitu gani?
  • Ni tukio lipi lililokuwa gumu zaidi kuzungumzia? Ni lipi lilikuwa rahisi zaidi? Kwa nini?
  • Ungelishughulikia vipi kila tukio kama lingekutokea wewe?
  • Unaweza kujilinda vipi na aina nyingine za uvamizi wa siri?
MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wajulishe wanafunzi kwamba aina nyingine za kupeleleza taarifa ni haramu na karibu katika matukio yote, huenda kupeleleza taarifa ni kinyume na maadili. Katika mahusiano ya aina tofauti, watu hutaka kupata/kuona aina mbalimbali za taarifa zinazowahusu. Aina hii ya kutafuta taarifa inakubalika na ni ya kawaida. Pia ni jambo sawa na la kawaida kwa mtu mmoja kufikiria kuwa hatua fulani inafaa lakini kwa mtu mwingine haifurahii.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Hivi sasa tutatazama kwa kina matukio ambayo tumeyazungumzia. Kwenye karatasi yako, chora mistari miwili tofauti ya vichekesho (ikiwa wanafunzi hawfurahii wazo la mfululizo wa michoro ya hadithi nzuri, pendekeza kwamba badala yake waandike kisa kifupi), inayoonesha:

  • Tukio ambalo unahisi kwamba mipaka yako au ya mtu mwingine haikuheshimiwa na jinsi ambavyo unatumaini watu wengine wangelichukulia suala hilo
  • Tukio ambalo unahisi kwamba mipaka yako au ya mtu mwingine iliheshimiwa na jinsi ambavyo watu wengine walionesha heshima na utu

Wape wanafunzi dakika 30 ili wakamilishe zoezi hili.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Viwango/Miongozo ya Jumuiya ni mkusanyiko wa masharti ambayo kampuni ya Facebook iliweka ili kujua mambo yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa katika mitandao yake ya Facebook na Instagram.

Viwango/Miongozo hii ndiyo msingi wa jinsi Facebook na Instagram huchukulia masuala ya usalama.

Ili kutengeneza sera, Facebook na Instagram hutambua matatizo, kufanya kazi na wataalamu mbalimbali ili kupata suluhisho, kisha kutengeneza sera na mbinu za kutoa usaidizi ili kuhakikisha kwamba matatizo hayo yanatatuliwa.

Kuna njia mbalimbali ambazo huduma na mifumo ya Facebook na Instagram hutofautiana, lakini kwa masuala yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa katika mitandao hiyo miwili ya kijamii, sera ziko sawa.

Sehemu muhimu ambapo kuna tofauti kati ya Facebook na Instagram ni kwamba Instagram haihitaji utengeneze akaunti kwa kutumia jina lako halisi.

Instagram in mahali ambapo mtu yeyote anaweza kujieleza, iwe ni kwa niaba ya nungunungu anayemtunza kwake nyumbani au mtu asiye na hakika anapenda watu wa jinsi gani na hayuko tayari kuzungumzia suala hilo akitumia jina lake halisi.

Sera hujaribu kuleta uwiano kati ya uhuru wa kujieleza na usalama. Hata hivyo kuna changamoto ya kufanikisha suala hili katika jumuiya ya mabilioni ya watu kutoka pande zote za ulimwengu.

Kitufe cha ‘kuripoti’ humwezesha mtu yeyote kuripoti jambo lolote kwetu kama vile fulani — ikiwa mtu huyo anadhani anakiuka masharti yetu.

Watu halisi wanaofanya kazi saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki ambao hupitia ripoti na kuchukua hatua zinazostahiki, na teknolojia ya akili bandia iliyobuniwa kwa namna inayoiwezesha kutambua maudhui yanayokikua masharti yetu, na kujulisha timu za kampuni ya Facebook ili zichukue hatua zinazotakiwa.

Unapokiuka miongozo ya jumuiya huenda maudhui yako yakafutwa/yakaondolewa (au Facebook ikuombe ufanye hivyo)

Ikiwa hutayaondoa wewe mwenyewe, hilo huenda likaathiri upatikanaji wa akaunti yako.
Mtu anapogundua kwamba hawezi kutumia akaunti yake, huenda akaunti hiyo imeondolewa na Facebook kwa kuwa mtu huyo aliitumia vibaya.

Facebook inatathmini upya wakati ambapo akaunti inafaa kuondolewa katika Instagram.
Hivi sasa akaunti zinaondolewa baada ya matukio ya idadi fulani ya ukiukaji wa masharti vinavyotokea ndani ya muda fulani.

Tumezungumzia kuhusu baadhi ya mipaka unayofaa kuzingatia unapowasiliana na watu mtandaoni, lakini ni vyema kukumbuka kwamba pia kuna masharti na sera zilizowekwa na watu wengine katika ulimwengu wa kidijitali.

Sio wewe unayeweka masharti na sera hizo, lakini sharti uzifuate ikiwa unataka kutumia huduma au tovuti zingine.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy