Somo 2: Kujenga Mtandao Wako wa Utetezi
Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.
Muhtasari wa Somo
Wanafunzi watajifunza jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kutumika vizuri ili kukuza jitihada za utetezi. Wanafunzi pia watajifunza jinsi ya kutengeneza maudhui ya mtandaoni ili kusambaza taarifa kuhusu lengo wanalotaka kutekeleza.
Matayarisho ya Somo
MUDA UNAOKADIRIWA
SWALI MUHIMU
- Mitandao ina uwezo gani katika jitihada za utetezi?
VIFAA
MATAYARISHO
- ambua video itakayotumika kuonesha mahusiano ya watu yanayotambulika katika jamii yako.
- Wanafunzi wanahitaji intaneti ili kukamilisha somo hili.
- Kuna fursa za kubadilisha maudhui yako ili yaendane na mambo ambayo wanafunzi wako wanafahamu na pia muktadha wa eneo lenu. Fursa hizi zimebainishwa kama "Dondoo za Mwalimu" katika hati nzima. Tunapendekeza kwamba ulipitie somo mapema na uandae mifano kabla ya kuanza kwa somo.
HIARI: USTADI WA ISTE DIGCITCOMMIT
- KUSHIRIKISHWA - Ninatumia teknolojia na mifumo ya kidijitali ili kushiriki katika masuala ya kiraia, kutatua shida na kuleta mabadiliko chanya katika jamii halisi na za mtandaoni.
Kutumia Mitandao ya Wanajamii Katika Shughuli za Utetezi
Sehemu ya 1
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO
Kuna msemo maarufu unaosema, "Cha muhimu sio kitu unachojua. Ni mtu unayejua." Ingawa msemo huu sio sahihi kwa 100% (unachojua pia ni muhimu sana!), unatukumbusha kuhusu umuhimu wa mitandao ya watu.
Haijalishi kama unatafuta kazi au unajaribu kucheza mchezo fulani katika kiwango cha juu, lakini kuwa na mtandao mzuri kunaweza kukuwezesha kupata wawasiliani wanaoweza kukusaidia kutimiza malengo yako. Juhudi za utetezi haziko tofauti na hilo. Kadiri tunavyokuwa na mtandao mkubwa na bora wa watu tunaowafahamu, ndipo inapokuwa rahisi zaidi kuleta mabadiliko katika jamii zetu.
Kuanzia familia na marafiki hadi walimu wetu na viongozi wa jamii, tayari tunafahamu watu wengi kushinda tunavyofikiria, hasa tunapojumuisha marafiki za marafiki na kuwa na watu zaidi katika mtandao wetu mbali na wale wenye mahusiano ya karibu nasi. Watu hawa wanaweza kuwa rasilimali muhimu katika kutusaidia kutimiza malengo yetu.
Kuna watu wengi ambao huenda hatuwafahamu hivi sasa ambao wanaweza kutusaidia kutimiza malengo yetu. Mitandao ya kijamii na intaneti kwa jumla hutupatia njia nyingine za kukutana na aina za watu wanaoweza kuchangia stadi au nyenzo zao katika jitihada zetu za utetezi.
Sehemu ya 2
DONDOO KWA MWALIMU
Kwenye skrini ya projekta mbele ya darasa, onesha mfano wa video inayoendana na maudhui ya eneo/mkoa wa wanafunzi wako ili kuonesha jinsi watu wanavyounganishwa kupitia mitandao ya watu na jinsi tunavyoweza kunufaika kutokana na mitandao hiyo.
WAULIZE WANAFUNZI WAKO
- Taarifa zinaweza kuenezwa vipi kwa njia nzuri kupitia mitandao yako ya watu uliyo nayo hivi sasa? Tunaweza kuitumia mitandao hii vipi ili kukuza jitihada za utetezi?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO
Katika zoezi linalofuata, mtatengeneza maudhui ya mtandaoni yanayoweza kusambazwa, yanayoeleza kuhusu mambo yanayowagusa.
Kwa kusambaza taarifa kuhusu jitihada zenu za utetezi mtandaoni, mnaweza kuwaambia watu wengine kuhusu mambo mnayojali na huenda mkakutana na watu wanaoweza kuwasaidia katika jitihada zenu!
Zoezi
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO
Tengeneza nyenzo za mtandaoni inayoweza kusambazwa (mfano; kwa kutumia Canva, Google Docs, mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook au Instagram, blogu ya WordPress, tovuti katika mfumo wa Neocities, wasilisho la slaidi kwa kutumia Scratch, Microsoft PowerPoint au Google Slides) kuhusu suala mnalojali, ambapo mtafanya yafuatayo: Andika utangulizi unaoeleza sababu na kwa nini mnadhani ni muhimu.
- Toa viunganishi vya tovuti kadhaa (mfano; makala ya mtandaoni) zinazoangazia tatizo hilo.
- Orodhesha watu watatu wanaoandika makala, mabloga, wanaochapisha katika Twitter au kutengeneza maudhui ya kidijitali yanayohusiana na suala hili. (Hiari: Ikiwa unaweza, mwandikie kila mmoja chapisho la Twitter na uwajulishe kuhusu jitihada unayopanga kutekeleza pamoja na malengo unayotaka kutimiza.)
MAZUNGUMZO YA DARASANI
Wape wanafunzi dakika 30 ili kukamilisha zoezi hili. Kulingana na muda uliotolewa, katika kundi la sasa au la pili litakaloundwa, waombe wanafunzi watoe nyenzo zao kwa kundi zima na wachukue dakika 15 wakijadili mikakati mizuri inayoweza kutumika.
DONDOO KWA MWALIMU
Mnapojadili mikakati mizuri na darasa lako, hakikisha kwamba wanafunzi wanazingatia mambo yafuatayo:
- Ni upi ujumbe mkuu wa utetezi/kampeni hii?
- Ni jukwaa gani linalofaa zaidi kwa kampeni hii?
- Ni akina nani mnaowalenga? Kampeni iliwafikia watu mliowalenga?
Hongera!
Umekamilisha Somo
Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa
Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.