Uwezeshaji wa Kidijitali

Somo 1: Utetezi na Kuleta Mabadiliko

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Utetezi Ni Nini?

Sehemu ya 1

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kuna sifa nyingi za jamii na mazingira yetu zinazotupendeza. Pengine tunafurahia marafiki zetu. Pengine tunafurahia kuichezea timu fulani ya michezo. Huenda tunapenda kupata fursa ya kusikiliza nyimbo mpya kutoka kwa wasanii tunaopenda.

Hata hivyo, wakati mwingine kuna sifa za jamii zetu ambazo hazitupendezi. Pengine shule imeweka sheria mpya ya mavazi, inayohitaji mavazi ya bei ghali ambayo hatuwezi kuyamudu. Labda mwanasiasa aliyechaguliwa anajaribu kutunga sheria ambazo hazizingatii mahitaji yetu. Pengine machaguo ya usafiri katika eneo tunaloishi hayana namna ya kutusafirisha hadi maeneo tunayotaka kwenda.

Tuseme kwamba mmeona kuwa mngelazimika kupanda mabasi kadhaa na kutembea umbali mrefu ili kufika kwenye supamaketi iliyo karibu zaidi nanyi.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mnaweza vipi kujaribu kulibadilisha hilo?
  • Je, kuna watu binafsi mnaoweza kuwasiliana nao ambao wanaweza kuwasaidia?
  • Pengine una marafiki wanaopitia baadhi ya matatizo ambayo wewe unapitia. Nyote mnawezaje kujipigania?
DONDOO ZA MWALIMU

Mfano ulio hapo juu unaweza kurekebishwa ili kuendana na mambo ambayo wanafunzi wako wanafahamu na pia muktadha wa eneo lenu. Lengo la mfano huu ni kuwasaidia wanafunzi kutambua maana ya utetezi na jinsi wanavyoweza kuutumia maishani mwao kwa kutambua tatizo katika eneo lao ambalo wanaweza kutatua.

Sehemu ya 2

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika hali za aina hii, mara nyingi tunahisi kwamba mambo huenda yatakuwa mazuri zaidi ikiwa tutaweza kubadilisha mambo yanayotukera. Ile hamu ya kupigania mambo unayoamini na kuleta mabadiliko ndiyo inakufanya kuitwa "mtetezi."

DONDOO KWA MWALIMU

Kwenye skrini ya maonesho iliyoko mbele ya darasa, pitia tovuti inayotumika kufanya shughuli za utetezi ambayo inaendana na eneo lenu. Angazia jinsi aina ya utetezi inayozungumziwa kwenye tovuti hiyo ilianza wakati watu, mara nyingi vijana, walipotambua kwamba kulikuwa na tatizo lililokuwa linaathiri jamii yao na wakataka kufanya jambo ili kujaribu kubadilisha hali hiyo. Mfano wa kimataifa ni kama Greta Thunberg. Mifano ya kawaida inaweza kujumuisha:

  • Ethiopia: Urithi wa Bluu
  • Kenya: Kuwapa Uwezo Watoto wa Kike
  • Zambia: Sistah Sistah Foundation

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Sasa tutatambulisha tatizo moja katika jamii yako ambalo linakugusa na hatua zinazofuata ambazo wewe na jamii yako mnaweza kuchukua ili kutatua tatizo.

ZOEZI

Wagawe wanafunzi katika makundi ya watu watatu. Lipe kila kundi muda katika kikao cha sasa angalau siku mbili;

  • Kufanya utafiti kuhusu tatizo linaloathiri jamii yao. Watafute angalau njia mbili kuhusu jinsi tatizo hilo linavyoathiri jamii na njia mbili zinazoweza kutumiwa ili kutatua tatizo hilo,
  • Kutengeneza bango linalotoa maelezo kuhusu tatizo lililotambuliwa na masuluhisho yanayoweza kutumika, ambalo litawasilishwa kwa kundi zima kama sehemu ya shughuli ya kuzunguka darasani na kutazama "maandishi na michoro iliyo darasani."
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika makundi yenu:

  • Fanyeni utafiti na mtambue tatizo moja la jamii yenu ("jamii" inaweza kuwa shule, mtaa au kikundi cha eneo lako ambacho wewe ni mwanachama) ambalo mngependa kubadilisha. Mnaweza kuzungumza na marafiki, walimu na/au familia zenu kuhusu mambo ambayo wangependa kubadilisha au kuhusu matatizo yanayowaathiri.
  • Tengeneza bango. Mabango yaliyotengenezwa na kila kundi yatabandikwa ukutani kisha "tutazunguka darasani" pamoja tukiyatazama huku kila kundi likijadili tatizo lililolitambua na jinsi ya kulitatua.

Kila kundi lazima litambue angalau njia mbili ambazo tatizo hilo linaathiri jamii zao na njia mbili zinazoweza kutumiwa ili kulitatua.

Kuweni wabunifu: Piga picha na mzibandike kwenye bango (ni vyema kuhakikisha kwamba wanafunzi watapata printa) ili kuonesha tatizo hilo na/au masuluhisho yake au mtumie chati za mitiririko ya hatua, grafu na chati za kuonesha ukubwa wa tatizo hilo na/au masuluhisho ya matatizo yake.

Kila bango linapaswa kuwa kamili — yaani, bango hilo linafaa kuwa na taarifa za kutosha ili mtu alitazame/alisome na aweze kuelewa tatizo lililopo na masuluhisho yanayoweza kutumiwa kulitatua bila kuhitaji kuelezwa na mwanachama wa kundi hilo.

ZOEZI

Lipe kila kundi muda wa kutosha kufanya utafiti na kutengeneza mabango. Hakikisha kwamba utakuwepo kujibu maswali na kutoa usaidizi wa kiufundi. Baada ya kundi zima kukusanyika tena, waombe wanafunzi wabandike mabango ukutani. Lipe kundi zima dakika 20 za kuzunguka darasani huku wanafunzi wakiangalia mabango ya wengine, kisha utoe takriban dakika 30 ili kila kundi dogo liwasilishe bango lake kwa kundi kubwa.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa
Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy