Muhtasari wa Somo
Washiriki wataelewa kuwa wanaweza kukuza na kudhibiti sifa na utambulisho wao mtandaoni kwa kuchukua hatua muhimu za faragha.
Washiriki wataelewa kuwa wanaweza kukuza na kudhibiti sifa na utambulisho wao mtandaoni kwa kuchukua hatua muhimu za faragha.
Tayari?
Anza Somo
Alama za kidijitali ni taarifa zote kuhusu mtu binafsi zilizopo mtandaoni au katika kikoa cha umma. Hii inaweza kujumuisha taarifa ibinafsi zilizowekwa na mtu binafsi lakini pia inaweza kujumuisha mafaili ya sauti, picha, machapisho kwenye mitandao ya kijamii, maandishi na video.
Alama za kidijitali zinaweza hata kujumuisha mwingiliano na familia, marafiki, vikundi na mashirika kupitia maoni na vitu walivyopenda. Jkama unavyoacha alama za Alama za miguu unapotembea,vivyo hivyo unaacha alama za kidijitali unapovinjari na kuwasiliana mtandaoni.
Utambulisho wa mtu binafsi unaweza kujumuisha imani yake, sifa, anachopenda na tabia zake. Inaweza pia kujumuisha uanachama na ushiriki wake katika vikundi vya jumuiya kulingana na sifa zinazomtambulisha au vitu anavyopenda.
Utambulisho wako mtandaoni ni jinsi unavyojionyesha katika mpangilio wa mtandaoni. Watu hutengeneza utambulisho wao wenyewe mtandaoni.
Uthibiti uko mikononi mwako
Unaweza kudhibiti utambulisho wako mtandaoni kwa njia na hali tofauti tofauti katika mipangilio. Unaweza kuwa na utambulisho tofauti mtandaoni kulingana na jumuiya, kikundi au jukwaa la mitandao ya kijamii unalotumia na watu unaowasiliana nao katika nafasi hiyo.
Utambulisho kwenye majukwaa
Jukwaa huwezesha mawasiliano na kuchangamana kati yako na watu wengine. Utambulisho wako wa mtandaoni unaweza kuwa sawa katika majukwaa yote ya mitandao ya kijamii au unaweza kutengeneza utambulisho tofauti tofauti kwa kila jukwaa.
Ni taarifa gani binafsi unayochagua kuiweka mtandaoni na ni nani uliyemchagua aione huunda utambulisho wako mtandaoni.
Kuchagua hadhira
Unaweza kuchagua kuposti baadhi ya maudhui na kuchagua kundi dogo la watu watakaoona posti hiyo. Ni muhimu kujua jinsi ya kufanya marekebisho hayo.
Sifa ya mtu binafsi inajumuisha imani au maoni ambayo watu wengine wanayo kuhusu mtu huyo.
Sifa yako ya mtandaoni ni jinsi wengine wanavyokuona katika mpangilio wa mtandaoni.
Utambulisho wako mtandaoni huchangia sifa yako mtandaoni, lakini huna udhibiti kamili wa sifa yako mtandaoni. Watu wengine watatafsiri Zoezi zako mtandaoni kulingana na imani, uzoefu na maoni yao binafsi.
Sifa yako mtandaoni inaweza kutofautiana kutoka kundi la watu moja hadi jingine.
Uwakilishi ni maudhui (picha, video), alama (emoji, GIF, meme) au maandishi yanayoonesha au kuwakilisha mtu au kitu fulani.
Fikiri kabla ya kushiriki;
Kwa maneno mengine, kitu ambacho watu huchapisha mtandaoni ni uwakilishi wao wenyewe na jinsi wanavyohisi kuhusu kitu au mtu fulani. Wakati mwingine, watu huchapisha maudhui wakiwa na nia au ujumbe ulio wazi kabisa. Wakati mwingine, chapisho lililowekwa linaweza kuwa sio wazi. Mara nyingi, chapisho lolote mtandaoni hutafsiriwa tofauti na watu tofauti. Ndio maana ni muhimu kufikiria juu ya ujumbe wa nyongeza chapisho lako linaweza kutuma, kabla ya kuposti.
Hongera!
Umekamilisha Somo
Wanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.

Tazama Ukurasa