Utangulizi wa Mafunzo ya Kidijitali

Somo 5: Uraia wa Kidijitali na Umuhimu Wake

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Chagiza Somo [dakika 10]

Dondoo za Mwalimu

Uchagizaji wa somo huwapa walimu mwongozo kuhusu kiasi cha mambo ambayo wanafunzi wanayajua kabla ya kuanza maudhui ya somo.
Kabla ya somo kuanza, andika maana ya Uraia wa Kidijitali na Ustawi kwenye ubao (tazama misamiati muhimu).

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Uraia wa kidijitali una maana gani kwako?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika vikundi vidogo, tumieni dakika mbili kusoma maana yake kisha mchague neno moja kutoka kwenye maana iliyotolewa ambalo mnahisi linaeleza vizuri zaidi maana ya kuwa raia wa kidijitali na pia mtoe sababu ya kuchagua neno hilo.

Kwa mfano: Kutilia maanani hisia za wengine - Hii ndiyo maana nzuri zaidi ya raia wa kidijitali kwa sababu sharti uingiliane na watu wengi mtandaoni na uelewe wao ni akina nani pamoja na hisia zao ili uweze kuwa raia wa kidijitali.

Dondoo Kwa Mwalimu

Vipe vikundi dakika mbili ili kutafakari kuhusu masuala haya na kuyajadili. Baadaye leta kundi zima pamoja ili kujadiliana kama darasa.

Kwa kuzingatia mjadala huo na maana iliyotolewa, waombe wanafunzi wafikirie maana zao wenyewe wakizingatia maana ya uraia wa kidijitali kwao.

Toa mfano mmoja au miwili kwa darasa zima.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kisha, tutaangalia manufaa na majukumu ya kuwa mwanachama wa jamii ya mtandaoni.

Mjadala wa Kundi [dakika 15]

Wanafunzi watafahamu manufaa na majukumu yanayotokana na kuwa mwanachama wa jamii ya mtandaoni.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Kwa kuzingatia mjadala wetu na maana iliyotolewa ya uraia wa kidijitali ni manufaa na majukumu gani yanayotokana na kuwa mwanachama wa jamii ya mtandaoni?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kwa Mfano: Manufaa ni kwamba unaweza kuwa na maiwasiliano chanya na watu kutoka ulimwenguni kote na kwa hivyo una wajibu wa kuheshimu mitazamo ya wengine.

Dondoo Kwa Mwalimu

Vipe vikundi dakika tano ili kutafakari kuhusu masuala haya na kuyajadili. Baadaye leta kundi zima pamoja ili kujadiliana kama darasa.

  • Majibu yanayoweza kutolewa ni pamoja na:
    • Ukuzaji endelevu wa ujuzi.
    • Kuwezeshwa kutumia teknolojia kuleta manufaa.
    • Kutofautisha ukweli na uongo.
    • Kujenga mahusiano mazuri.
    • Kukaa salama.
    • Uwe na usawa kwa muda unaotumia na usiotumia kwenye vifaa vya kidijitali.
    • Ongoza wengine kwa kutilia maanani matakwa yao na uwasiliane na watu wa tamaduni mbalimbali.
    • Heshimu mitazamo iliyo tofauti na yako.
    • Tafakari kwa makini kuhusu jinsi wewe na wengine mnavyochangia katika jamii na kushirikiana ili kuleta maendeleo chanya ndani na nje ya mtandao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kisha, tutajadili kwa nini manufaa na majukumu haya ni muhimu.

Maingiliano ya ndani ya Darasa [dakika 15]

Wanafunzi watapata uelewa kuhusu maana ya uraia wa kidijitali na umuhimu wake katika mtandao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika vikundi vyenu vidogo, andikeni sababu 2-3 za umuhimu na majukumu ya uraia wa kidijitali.

Kwa mfano: Uraia wa Kidijitali ni muhimu kwa sababu jamii ya mtandaoni haina tofauti na jamii halisi kwa hivyo sharti ichukuliwe kwa heshima na hadhi sawa.

  • Majibu yanayoweza kutolewa ni pamoja na:
    • Jamii za mitandaoni ni mahali pa kuimarisha uraia hai.
    • Jamii za mitandaoni ni mahali pa kuchunguza maadili binafsi.
    • Jamii za mitandaoni ni mahali pa kujenga mahusiano.
    • Jamii za mitandaoni ni mahali pa kufanya utetezi na uhamasishaji.
    • Jamii za mitandaoni ni mahali pa kutafiti na kutafuta taarifa za kweli.

Mambo muhimu ya kukumbuka [dakika 5]

Pitia somo ukitumia hoja hizi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Uraia wa kidijitali ni muhimu katika kudumisha usalama na heshima katika jamii za mtandaoni.

Raia wa kidijitali wanaendelea kukuza na kupata uelewa kuhusu maana ya uraia wa kidijitali na sababu za umuhimu wake katika mtandao.

Manufaa na majukumu ya kuwa raia mwema wa kidijitali ni pamoja na ukuzaji endelevu wa elimu ya matumizi yanayofaa na yenye kuwezeshwa na utumiaji wa teknolojia. Elimu hii ni pamoja na kusaidia watu kutofautisha ukweli na uongo, kujenga mahusiano, yanayofaa, kukaa salama, kupata ustawi, kuwa thabiti na kuwaongoza wengine kwa kutilia maanani matakwa yao. Nyingine ni kufikisha habari kati ya watu wenye tamaduni tofauti, kuheshimu mitazamo iliyo tofauti na yao, kufikiria kwa makini kuhusu jinsi wanavyochangia katika jamii na kushirikiana ili kuleta maendeleo chanya ndani na nje ya mtandao.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy