Utangulizi wa Mafunzo ya Kidijitali

Somo 3: Upatikanaji wa Taarifa na Jamii za Mtandaoni

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Chagiza Somo [dakika 15]

Dondoo kwa Mwalimu

Uchagizaji wa somo huwapa walimu mwongozo kuhusu kiasi cha mambo ambayo wanafunzi wanayajua kabla ya kuanza maudhui ya somo.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Pamoja na mwenzako au kwenye kikundi chako kidogo tumia dakika mbili kuchagua moja ya kauli zifuatazo kisha uzungumzie kisa au jambo ulilopitia. Kila mtu atapewa dakika moja ya kuzungumza:

  • Nilitafuta kwenye intaneti kuhusu ...
  • Nilichati mtandaoni na mtu fulani kuhusu …
  • Nilipokea au kutuma ujumbe wa mtandaoni kwa ...
  • Nilisambaza jambo mtandaoni ambalo ...
Dondoo Kwa Mwalimu

Kila mwanafunzi azungumzie kisa cha mtu mwingine ambacho ameambiwa.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kuna njia nyingi ambazo tunatumia intaneti - kutafuta taarifa, kuwasiliana na watu wengine au kuwasiliana na watu. Kisha, tutajifunza kuhusu mbinu mahususi za kufanya mambo haya.

Mjadala wa Kundi Zima [dakika 10]

Wanafunzi watapata uelewa wa mchakato wa upatikanaji wa marafiki na taarifa.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Intaneti ni mtandao mkubwa wa kompyuta na vifaa, lakini siku hizi kuna aina nyingi tofauti za kompyuta. Pamoja na mwenzako au katika kikundi chako kidogo tumia dakika mbili kujadili ni zipi aina za kompyuta au vifaa vya kidijitali? Tutajadili majibu yenu mtakapokamilisha mjadala. Majibu ambayo huenda yatatolewa:

  • Kompyuta kubwa ambayo haisogezwi
  • Kompyuta mpakato
  • Kishikwambi
  • Simu janja
  • Saa janja

Baada ya kompyuta yako kuunganishwa kwenye intaneti, mara nyingi unatumia kivinjari ili kupata mtandao wa ulimwenguni kote.

Kwenye mtandao utapata tovuti na kurasa za wavuti. Mfano; Mitandao ya kijamii, blog na magazeti au maduka uyapendayo.

Moja ya sababu kubwa za watu kutumia intaneti ni kutafuta taarifa na hivyo hutumia injini ya utafutaji. Tutaangalia injini tofauti tofauti za utafutaji na jinsi zinavyotumiwa.

Kuna injini nyingi tofauti za utafutaji kote ulimwenguni mnazoweza kuchagua kutumia. Pamoja na mwenzako au katika kikundi chako kidogo tumia dakika mbili kuzijadili.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Ni injini gani za utafutaji mnazofahamu?
    • Majibu ambayo huenda yatatolewa:
      • Google
      • Yahoo
      • Bing
      • Baidu
      • YANDEX
      • DuckDuckGo
Dondoo za Mwalimu

Injini hizo za utafutaji zinaweza kuwa mifumo ambayo inatumika katika eneo unalofundisha.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Injini za utafutaji hutafuta katika tovuti nyingi tofauti na kutupatia orodha ya tovuti husika ambazo zinaweza kukupa taarifa zaidi kuhusu mada hiyo.

Dondoo za Mwalimu

Andika maswali yaliyo hapa chini kwenye ubao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tumieni dakika tano kujadili maswali haya pamoja na mwenzako au katika kikundi chako kidogo. Baadaye tutashirikishana majibu na kundi zima.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuitumia injini ya utafutaji hapo kabla?
  • Ni injini zipi za utafutaji umezitumia?
  • Umetafuta nini?
  • Ulikipata ulichokuwa unakitafuta?

Mazungumzo ya Darasani [dakika 10]

Wanafunzi watapata uelewa wa jinsi ya kutumia mitandao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Watu hutumia intaneti ili kuwasiliana na watu wengine. Pamoja na mwenzako au katika kikundi chako kidogo, tumieni dakika mbili kujadili maswali yafuatayo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Ni mitandao gani ya kijamii mnayoifahamu ambapo watu huwasiliana na watu wengine?
    • Majibu ambayo huenda yatatolewa:
      • Facebook
      • Snapchat
      • Twitter
      • LinkedIn
      • Instagram
      • YouTube
      • TikTok
Dondoo za Mwalimu

Mitandao ya kijamii inaweza kugeuzwa kuwa mifumo ambayo inatumika katika eneo ambalo unafundisha.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Unaweza kuipata mitandao hii kwenye tovuti katika kompyuta mpakato/kifaa au kupitia programu iliyo kwenye simu janja yako.
Mitandao ya kijamii hujenga dhana ya umoja kupitia njia ya mtandao. Mitandao mingine ya kijamii huwapa watumiaji uwezo wa kuchapisha picha, video au maneno ili kuonesha matukio yanayofanyika katika maisha yao.

Sababu nyingine ya kutumia intaneti ni kutuma meseji za papo hapo. Mifumo hii inajumuisha programu kama:

  • Facebook Messenger
  • WhatsApp
  • WeChat
  • LINE
  • Skype
  • Telegram
  • Signal

Mifumo hii hukuwezesha kuwasiliana moja kwa moja na mtu mwingine au kundi la watu kwa namna isiyo wazi sana kwa umma.

Dondoo Kwa Mwalimu

Mifumo ya kutuma meseji za papo hapo inaweza kugeuzwa na kuwa mifumo inayopatikana katika eneo unalofundisha.

Andika maswali yaliyo hapa chini kwenye ubao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tumia dakika tano kujadili maswali haya pamoja na mwenzako au katika kikundi chenu kidogo. Baadaye tutajadili majibu yenu na darasa zima.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Ni njia gani ambazo unaweza kuzitumia kuwasiliana na watu mtandaoni?
  • Je, hapo kabla umewahi kutumia yoyote kati ya mitandao hiyo ya kijamii au mifumo ya kutuma meseji za papo hapo?
  • Ni njia zipi unazipenda zaidi?

Mazungumzo ya Darasani [dakika 10]

Wanafunzi watazijua njia tofauti za kuwasiliana mtandaoni.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Watu hutumia intaneti kuwasiliana au kutuma barua za kieletroniki au barua pepe. Pamoja na mwenzako au katika kikundi chenu kidogo, tumia dakika mbili kujadili swali lifuatalo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Ni mifumo gani ya barua pepe iliyo maarufu?
    • Majibu ambayo huenda yatatolewa:
      • Gmail
      • Outlook
      • Yahoo
      • AOL
      • Yandex
      • GMX
      • Zoho
      • ProtonMail
Dondoo za Mwalimu

Mifumo ya barua pepe inaweza kugeuzwa ili iendane na mifumo ambayo inatumika katika eneo unalofundisha.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Mifumo hii ya barua pepe huwawezesha watu kutuma ujumbe wa kielektroniki na barua pepe kama njia ya kuwasiliana mtandaoni na watu au vikundi vya watu.

Mifumo mingi ya barua pepe huwapa watumiaji uwezo wa kutengeneza njia za anwani za mtandaoni na mbinu za uhifadhi ili kuainisha na kupanga barua pepe zao.

Mambo muhimu ya kukumbuka [dakika 5]

Pitia somo ukitumia hoja hizi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Unapoingia kwenye intaneti mara nyingi utatumia kivinjari ili kupata mtandao wa ulimwenguni kote. Kwenye mtandao utapata tovuti na kurasa za wavuti unazoweza kuzitumia kupata taarifa na marafiki wa mtandaoni.

Kuna injini nyingi tofauti za utafutaji zilizo na tovuti tofauti na zinakupa orodha ya tovuti husika unazoweza kutumia kupata taarifa zaidi kuhusu mada uliyotafuta.

Watu hutumia mitandao ya kijamii na tovuti kusambaza taarifa kuhusu maisha yao binafsi, kuwasiliana na jamaa na marafiki au kushiriki katika shughuli zingine za kijamii mtandaoni kama vile kusambaza muziki, picha, video au vichekesho.

Ingawa kuna njia nyingi za mawasiliano ya mtandaoni - yaliyo rasmi na yasiyo rasmi, ni muhimu kukumbuka kwamba mifumo mingine ya mtandaoni inafaa zaidi kwa mawasiliano rasmi. Mfano kama vile unapowasiliana na waajiri, na mingine inafaa zaidi kwa mawasiliano yasiyo rasmi, kama vile kuzungumza na marafiki na jamaa. Katika somo jingine tutaangalia umuhimu wa mfumo unaotumia kwa mtu unayewasiliana naye na usalama wa mfumo husika.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy