Utangulizi wa Mafunzo ya Kidijitali

Somo 4: Utambulisho wa Kidijitali na Sifa ya Mtandaoni

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Mvuto wa Somo [dakika 10]

Dondoo za Mwalimu

Uchagizaji wa somo huwapa walimu mwongozo kuhusu kiasi cha mambo ambayo wanafunzi wanayajua kabla ya kuanza maudhui ya somo.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tunapozungumzia utambulisho, ni kuhusu wewe binafsi — sifa zako, imani na maadili, Ujuzi ulionao, mambo unayopenda na yale yanayokufurahisha zaidi. Lakini kumbuka kwamba pia tuna utambulisho wa mtandaoni — utambulisho wa kidijitali.

Tumia dakika mbili ili kutengeneza orodha ya mambo 10 makuu yanayowakilisha utambulisho wako. Fanya hatua hii peke yako. Hutakiwi kulishirikisha kundi kuhusu mambo hayo.

Sasa pamoja na mwenzako ni mambo mangapi kati ya yale mliyo yaorodhesha ambayo mngejisikia huru kuwaambia;
1. Marafiki zenu [weka alama ya herufi F mbele yake]
2. Mwalimu/mwajiri/bosi [weka herufi X mbele yake]
3. Mtu msiyemfahamu [weka herufi S mbele yake]

Taarifa zote unazoweka, kuchapisha na kusambaza unapokuwa kwenye intaneti huchangia kutengeneza utambulisho wako wa kidijitali. Ikiwa uliisambaza orodha hii ya mambo 10 mtandaoni, ni muhimu kukumbuka kwamba jambo lolote kati ya yale uliyo orodhesha kwenye orodha ya utambulisho wako linaweza kufika mtandaoni.

Kisha, tutajadili kuhusu jinsi taarifa zilizo wazi kwa umma huchangia maoni ya watu wengine kukuhusu.

Mjadala wa Kundi Zima [dakika 10]

Wanafunzi watafikiria kuhusu jinsi taarifa zinazopatikana kwa umma mtandaoni huchangia maoni ya watu wengine kuwahusu.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika vikundi vyenu vidogo tafuteni vitu vitatu ambavyo vinaweza kutengeneza utambulisho wako wa kidijitali kisha mviandike kwenye karatasi yenye mistari.

Hii inaweza kuwa ni pamoja na mambo ambayo unachapisha au kusambaza mtandaoni kama vile habari za matukio, picha za kuchekesha, meseji za picha, n.k Pia inaweza kuwa ni pamoja na taarifa unazochagua kusambaza mtandaoni kukuhusu wewe (mfano; wasifu wako wa mitandao ya kijamii, namba ya simu n.k.).

Dondoo za Mwalimu

Vipe vikundi dakika tano ili kutafakari kuhusu masuala haya na kuyajadili. Baadaye leta kundi zima pamoja ili kujadiliana kama darasa.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kila wakati unapoingia kwenye intaneti na kuchapisha kitu au kuweka taarifa fulani unaacha alama.

Ni sawa na unapotembea katika udongo au matope — unaweza kuona alama za miguu yako na unaacha alama nyuma yako. Wakati mwingine alama hizi haziwezi kufutwa.

Hii inamaanisha kwamba shughuli zote za mtandaoni huacha alama inategemea na jinsi unavyosimamia taarifa zako.

Kisha, tutajadili kuhusu ni taarifa gani ambazo ungependa zionekane wakati mtu anatafuta jina lako.

Majadiliano Darasani [dakika 15]

Wanafunzi watazingatia taarifa ambazo wangependa zionekane wakati mtu anatafuta majina yao.

Dondoo Kwa Mwalimu

Mtambulishe Angela kwa wanafunzi wako (mtu wa kubuni).

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Msalimieni Angela! Angela ameingia katika ulimwengu wa mtandao hivi majuzi. Lengo letu ni kumsaidia katika safari yake ya mtandaoni. Hebu tumfahamu Angela zaidi.

Dondoo za Mwalimu

Andika taarifa zilizo hapa chini kwenye ubao:

  • Ana miaka 19 na anasomea kozi ya uuguzi.
  • Anatoka katika jiji la Dodoma na anapenda kuimba karaoke
  • Alilelewa na familia yake yeye pamoja na kaka yake John. Wana uhusiano wa karibu sana kwa sababu amemzidi kaka yake umri kwa miaka 2 tu.
  • Anapokuwa na muda wa ziada, Angela anapenda kutazama filamu.

Majina na mifano hii inaweza kuwa ya kawaida ili yalete uhalisia wa majina ya watu yanayotumika sana na hali za kawaida katika eneo unalofundisha. Lengo la mfano huu ni kuwafundisha wanafunzi kuhusu mambo yanayotengeneza utambulisho wa kidijitali na kujua jinsi taarifa za kawaida za sifa ya mtu zinavyoweza kuingia katika ulimwengu wa kidijitali.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO

Pia Angela ana utambulisho kwenye mtandao — utambulisho wa kidijitali. Unadhani utambulisho huo unaweza kuwa upi? Kumbuka kwamba, yale atakayochagua kufanya mtandaoni (yaani kusambaza na kuchapisha) au chochote atakachoweka kwenye intaneti — kitakuwa sehemu ya utambulisho wake wa kidijitali.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Katika kikundi chenu kidogo tumieni dakika tano kutengeneza orodha ya mambo yote ambayo Angela huenda anafanya mtandaoni kulingana na taarifa mnayojua hadi sasa.

Andikeni majibu yenu kwenye karatasi. Tutayajadili kwa pamoja kama darasa.

  • Majibu Ambayo Huenda Yatatolewa:
    • Anatafuta Kazi za Uuguzi
    • Maeneo (Migahawa) ya Kuimba Karaoke
    • Zawadi za Kumpa Kaka yake Wakati wa Siku Yake ya Kuzaliwa au Wakati wa Sikukuu
    • Kumbi za Filamu au Saa za Maonyesho Katika Kumbi za Eneo Analoishi
    • Filamu Maarufu Sasa Hivi Katika Netflix
    • Matamasha ya Filamu
WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Kwa nini ni muhimu kudumisha usalama wa utambulisho wako wa kidijitali? Chukulia kwamba taarifa zote ambazo mmeorodhesha kuhusu Angela zitahifadhiwa katika faili la karatasi kisha mchukulie kwamba watu wengine watatazama faili hilo.
  • Je, ungefanya, maamuzi tofauti iwapo ungegundua kwamba habari kuhusu shughuli zako siyo za siri?
Dondoo Kwa Mwalimu

Wape wanafunzi muda wa kujibu.

Maingiliano ya ndani ya Darasa [dakika 15]

Wanafunzi watazingatia taarifa ambazo wangependa zionekane wakati mtu anatafuta majina yao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Ni mambo, gani binafsi ambayo mnaweza kusambaza mtandaoni na ni yapi ambayo mtayafanya kuwa ni siri? Hatua ya kwanza ni kutambua watu ambao una wasiliana nao mara kwa mara au wale ambao wanaweza kuzipata taarifa zako. Katika vikundi vyenu vidogo tumia dakika mbili kutafakari kuhusu yafuatayo:

  • Je, unaweza kuwaambia marafiki zako jina lako?
  • Je, unaweza kuwaambia marafiki zako mahali unapoishi?
  • Je, unaweza kuwaambia marafiki zako siri zako?

Sasa tutafakari kuhusu watu wengine mnao onana mara kwa mara kisha mjiulize maswali yafuatayo. Katika vikundi vyenu vidogo tumia dakika mbili kutafakari kuhusu yafuatayo:

  • Je, unaweza kusimama mbele ya darasa au ofisi — ambapo unawajua watu kadhaa, ila sio wote — kisha uwaambie jina lako?
  • Je, unaweza kuwaambia tarehe yako ya kuzaliwa?
  • Je, unaweza kuwaambia mahali unapoishi?

Hatimaye, tafakari kuhusu jinsi wewe mwenyewe unavyotumia intaneti. Katika vikundi vyenu vidogo, tafakarini kuhusu taarifa mnazosambaza na mtafakari iwapo machapisho yenu yanaweza kuwaumiza wengine, kueleweka ndivyo sivyo au kutia doa sifa yako — au ya mtu mwingine.

Dondoo Kwa Mwalimu

Wape wanafunzi dakika nane za kutafakari kuhusu masuala haya na kuyajadili. Baadaye leta kundi pamoja kwa majadiliano ya kundi zima kwa muda wa dakika mbili.

Mambo muhimu ya kukumbuka [dakika 10]

Pitia somo ukitumia hoja hizi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Unapofikiria kuhusu habari utakazosambaza, mtandaoni zingatia maadili yako na ya wale wanaopokea habari hizo. Hili linaweza kukusaidia kujua kwa urahisi taarifa ambazo unajisikia huru kuzisambaza na zile ambazo hufai kuzisambaza.

Huku kukiwa na teknolojia mpya siku hizi taarifa zilizo wazi kwa umma zinaweza kuenea haraka sana na kufikia wapokezi wapya na kuchangia maoni ya wengine kutuhusu.

Fikiria kuhusu taarifa binafsi ambazo ungependa zionekane mtandaoni wakati mtu anatafuta jina lako — hasa taarifa zenye kuaibisha. Mara baada ya taarifa hizi kuwekwa mtandaoni inaweza kuwa vigumu sana kudhibiti watu watakaoziona.

Kila unaposambaza taarifa mtandaoni (hata ikiwa unazisambaza moja kwa moja na mtu mmoja, kama vile kupitia meseji binafsi), kuwa tayari kwa uwezekano kwamba habari hizo zinaweza kuenea kwa watu wengine wa kando na watu uliowakusudia wafikiwe na habari hizo.

Sababu nyingine ya kutilia maanani utambulisho wako wa kidijitali ni kuwa baadhi ya taarifa unazochapisha mtandaoni zinaweza kupatikana kwa umma kupitia utafutaji wa mtandaoni. Hii inaweza kuwa ni pamoja na picha, akaunti za mitandao ya kijamii, shule yako, kazi na mwajiri wako, machapisho ya habari unazoshiriki pamoja na makundi yako ya kijamii.

Watu unaokutana nao wanaweza kutumia injini za utafutaji ili kupata taarifa zaidi kukuhusu. Habari watakazopata, ziwe nzuri au mbaya zitachangia maoni yao kuhusu wewe. Ikiwa unataka kudhibiti jinsi wanavyokuchukulia ni muhimu kwamba ufahamu taarifa ambazo huenda wataona.

Watu hawa ni pamoja na waajiri wako wa baadae na maafisa udahili wa shule, vyuo vya kati au vyuo vikuu. Maafisa udahili huenda wasiwaambie waombaji ikiwa walitafuta au hawakutafuta taarifa zao mtandaoni na/au walitumia taarifa hizo kufanya maamuzi yao.

Zoezi la Hiari

Ikiwa sio tatizo kwa wanafunzi, waombe watafute majina yao katika injini ya utafutaji ya mtandaoni au kama darasa mnaweza kuamua kuhusu mtu maarufu mtakayemtafuta kupitia injini ya utafutaji ya mtandaoni.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Umepata nini?
  • Umestaajabishwa na taarifa zilizoonekana?
  • Kuna watu wengine wengi wenye jina sawa na lako?
  • Mtu asiyekufahamu anaweza kukuchukulia vipi baada ya kuziona taarifa hizo?
Dondoo Kwa Mwalimu

Wape dakika 10-15 za kujadiliana kama darasa.


End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy