Muhtasari wa Somo
Washiriki wataweza kutambua na kutathmini uaminifu wa vyanzo vya kidijitali (ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuthibitisha vyanzo vya habari, kutambua upendeleo, habari potofu,taarifa iliyopikwa na kutathmini utafutaji).
Washiriki wataweza kutambua na kutathmini uaminifu wa vyanzo vya kidijitali (ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuthibitisha vyanzo vya habari, kutambua upendeleo, habari potofu,taarifa iliyopikwa na kutathmini utafutaji).
Tayari?
Anza Somo
Katika ulimwengu wetu wa kidijitali, watumiaji wana ufikiaji wa papo hapo wa habari, taarifa na rasilimali ili kujifunza zaidi karibu kuhusu kila kitu. Kuwa na kiwango hiki cha upatikanaji wa habari ni faida kubwa, lakini pia kunaweza kutatanisha na kulemea. Kabla ya kufanyia kazi habari au kushiriki na wengine, unapaswa kuhakikisha kuwa unajua ni taarifa za kuaminika na sahihi.
Chanzo cha habari kinachoaminika ni kile ambacho hutoa habari sahihi kulingana na uthibitisho mzuri. Vyanzo vinavyoaminika kwa kawaida huwa na utaalamu katika eneo husika la habari hiyo. Kuaminika hakupo wazi wakati wote, na vyanzo vyake huwa na nguvu na udhaifu wake. Hii ndiyo sababu ni muhimu kujifunza mbinu mbalimbali za kutathmini taarifa, hasa taarifa za mtandaoni zinazopatikana kupitia mitandao ya kijamii na utafutaji kwenye tovuti. Ujuzi wa vyombo vya habari vya dijitali unaweza kukusaidia kujua jinsi ya kutathmini kwa kina taarifa na vyanzo vyenye uwezekano wa upendeleo au taarifa potofu.
Watu hutumia aina mbalimbali za injini za utafutaji na mitandao ya kijamii ili kupata taarifa kwenye mtandao. Kila mtandao hutumia kanuni—seti ya maagizo yaliyoratibiwa na kompyuta ili kukamilisha kazi—ili kurudisha matokeo ya kipekee kulingana na mambo kama vile eneo lako la kijiografia, utafutaji mwingine kuhusu mada zinazofanana, utafutaji wako wa awali na kiwango cha maelezo katika swali lako la utafutaji.
Ni muhimu kutambua kwamba hata matokeo ya juu katika utafutaji wa tovuti yanapaswa kupimwa ukweli wake.
Kwa mfano, baadhi ya matokeo bora ya utafutaji ni matangazo yanayolipiwa na makampuni au mashirika mengine ili kutangaza bidhaa au huduma zao. Haya yanaweza kutambuliwa kwa maneno kama vile ‘Tangazo’ au ‘Matokeo Yanayofadhiliwa’ na kwa kawaida huonekana sehemu ya juu au kwenye ukurasa.
Hata kama sehemu ya maudhui inaonekana na kuonekana kuwa ni ya kweli, hiyo haimaanishi kuwa ni ya kuaminika au sahihi. Wakati mwingine, vyanzo vya habari vinajaribu kueneza taarifa potofu au habari potofu, ambazo utajifunza kuzihusu baadaye katika somo hili. Unapokuwa na shaka, tafuta vyanzo vingine vya kuthibitisha habari kabla ya kuisambaza.
Kiasi cha habari mtandaoni kwa hakika hakina kikomo. Ili kuepuka kuelemewa wakati wa kutathmini vyanzo, tumia mkakati rahisi wa STTF, ambao ni kifupi kilichoundwa na Michael Caufield, mtaalamu wa kujuzi wa vyombo vya habari vya kidijitali katika Chuo Kikuu cha Washington State Vancouver.
STTF ni kifupi kinachosimama kwa:
SUBIRI
TAFITI CHANZO
1.Wakati wa kuamua uaminifu wake, tafakari Je, chanzo kina utaalamu na nia gani?
Kwenye utaalamu wa chanzo: tafuta chanzo kinajua nini kuhusu mada na jinsi walivyoipata habari hiyo wao wenyewe.
Kwenye nia ya chanzo: tafuta chanzo kinataka uamini nini kuhusu mada na kwa nini wanataka uamini habari hiyo
2. Unapaswa pia kuzingatia ni nani anayeweza kufaidika kutokana na (au anaweza kuumizwa) na chanzo cha habari
3.Uchunguzi mfupi wa chanzo cha habari unaweza kukusaidia kuelewa vyema kama ni chanzo kinachoaminika ambacho kinafaa kusoma au kusambazwa?
4.Kwa utafiti wa kina, unaweza kutaka kukagua madai binafsi ndani ya habari yenyewe.
TAFUTA CHANZO BORA ZAIDI
FUATILIA MADAI, NUKUU, PICHA NA VIDEO HADI KWENYE CHANZO ASILI
Viashiria 8 vya Uaminifu ni pamoja na:
Ikiwa unatathmini taarifa inayoonekana, zingatia nguzo hizi tano za uthibitishaji wa kuona kutoka First Draft:
Taarifa zinazoonekana zinaweza kujumuisha chati na grafu, meme, picha, video au taarifa yoyote inayowasilishwa kwa njia ya kuona.
Kuna viwango tofauti vya udanganyifu ndani ya picha na video zilizobadilishwa:
Unawezaje kujua kama unatazama Feki ya kina?
Angalia kwa karibu utofauti wa kuona:
Taarifa bandia ni maudhui ambayo ni ya uwongo au ya kupotosha.
Taarifa potofu ni habari ya uwongo au ya kupotosha iliyoundwa au kusambazwa kwa nia mbaya ya kusababisha madhara, kudanganya au kupotosha mtu binafsi, kikundi au shirika.
Aina za habari za udanganyifu
First Draft ni shirika lenye dhamira ya "kuwezesha jamii kwa maarifa, ufahamu na zana zinazohitajika ili kuzishinda taarifa za uwongo na za kupotosha."Wanatambua aina saba za kawaida za habari ya mtandaoni ya udanganyifu kuanzia habari bandia hadi habari potofu:
1.Kejeli: Kejeli inatumia mfumo wa kuchekesha kutoa maoni kuhusu matukio ya sasa, asili ya binadamu au mada nyinginezo za kijamii. Kejeli inaweza kuwa sehemu nzuri ya mawasiliano, lakini nje ya muktadha, inaweza kutumika kupotosha.
2.Muunganisho wa uwongo: Pia inajulikana kama mtego bofya, aina hii ya taarifa ya udanganyifu hutumia picha au lugha ya kusisimua kuwashawishi watu kubofya Makala au video ambazo haziendani na maudhui yaliyomo ndani.
3.Maudhui yanayopotosha: Maudhui ambayo ni ya kweli lakini yanayotumiwa kwa njia ya kupotosha.
4.Maudhui ya kilaghai: Maudhui ya uwongo au yanayopotosha ambayo yameundwa kuonekana kana kwamba yanatoka kwenye shirika au chanzo kinachotambulika, lakini sivyo.
5.Muktadha wa uwongo: Maudhui ya kweli ambayo yanasambazwa yakiambatana na maelezo ya uongo ya muktadha.
6.Maudhui yaliyobadilishwa: Maudhui ya kweli, ikiwa ni pamoja na taswira, ambayo yamebadilishwa kuwa ya kupotosha.
7.Maudhui yaliyotungwa: Maudhui ambayo ni 100% ni ya uwongo. Katika sehemu inayofuata, utajifunza juu ya feki za kina.
Utangazaji wa mtandaoni hutumia mikakati mbalimbali ili kuwafanya watu kubofya matangazo au kuchangamana na bidhaa na huduma. Baadhi ya mikakati hii ni pamoja na mtego bofya, Uidhinishaji na Maudhui yanayofadhiliwa. Unaweza kudhibiti matangazo unayoona kwa kurekebisha mapendeleo yako ya tangazo.
Mtego bofya hutumia vichwa vya habari na picha za kusisimua ili kuvutia umakini wako na kukushawishi kubofya makala.
Unawezaje kujua ikiwa kitu ni Mtego Bofya?
Hapa kuna vidokezo:
Matangazo mengi ni rahisi kutambulika, wakati mwingine watangazaji hutumia Uidhinishaji na maudhui yaliyofadhiliwa ili kufanya tangazo lichanganywe na maudhui ya uandishi wa habari. Uidhinishaji ni wakati kampuni hulipa watu kutangaza bidhaa zao kwenye wasifu wao wa mitandao ya kijamii kupitia machapisho yaliyofadhiliwa.
Maudhui yanayofadhiliwa ni tangazo ambalo hufanywa ili kuonekana kama chanzo cha habari kisichopendelea au makala ya habari. Tovuti za habari za mtandaoni huchapisha maudhui yaliyofadhiliwa, na pia yanapatikana kwenye mitandao ya kijamii na kwenye akaunti za waraghabishi unaowapenda.
Unaweza kutambua mapendekezo na maudhui yaliyofadhiliwa kwa kutumia mikakati hii:
Hongera!
Umekamilisha Somo
Wanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama Ukurasa