Utangulizi wa Mafunzo ya Kidijitali

Somo 1: Intaneti ni nini na Tunajiungaje?

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Chagiza Somo kwa [dakika 10]

Wape wanafunzi wako picha iliyoko hapa chini kisha uongoze mjadala kuhusu mada hii:

 • "Kiasi cha data kinachokadiriwa kutengenezwa kwenye intaneti kwa dakika moja" [Chanzo: Dakika Moja Kwenye Intaneti Katika Mwaka 2020]. https://www.statista.com/chart/17518/data-created-in-an-internet-minute/
Dondoo Za Mwalimu

Mkufunzi utambue;
Uchagizaji wa somo huwapa walimu mwongozo kuhusu kiasi cha mambo ambayo wanafunzi wanayajua kabla ya kuanza maudhui ya somo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Mnatambua nembo au chapa zipi?
 • Je nembo hizo ni maarufu kwa sababu gani?
 • Zinatoa huduma gani?
  • Majibu yanayoweza kutolewa ni pamoja na:
   • Kuchati mtandaoni
   • Burudani - Muziki/Video/Filamu
   • Kuunganisha Watu
   • Manunuzi (Biashara ya Mtandaoni) na Usafirishaji
 • Kwa mujibu wa muktadha wenu (angalia msamiati) na uelewa wa intaneti, unadhani ni muda gani unaowakilishwa katika chati hii?
 • Hususani kuhusu YouTube, Je, watumiaji watatumia muda gani kupakia video zenye saa 500?
  • Jibu ni dakika moja.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO
Picha hii inaonesha, namna ambavyo baadhi ya makampuni hutoa huduma kwa watu wanaotumia intaneti.

Kulingana na data (zilizokusanywa na Visual Capitalist), dakika moja kwenye intaneti huwa na:

 • Zaidi ya saa 400,000 za video ambazo watu hutazama katika Netflix.
 • Saa 500 za video zilizopakiwa kwenye chaneli mbalimbali za YouTube.
 • Karibu meseji milioni 42 husambazwa kupitia WhatsApp.
 • Dakika hiyo moja kwenye intaneti pia ina zaidi ya vifurushi 6,500 vinavyotumwa na Amazon.
 • Dakika hiyo moja kwenye intaneti ina washiriki 208,333 walio kwenye mikutano inayofanyika kwa Zoom.

Mjadala wa Kundi [dakika 10]
Wanafunzi wataelewa jinsi intaneti inavyofanya kazi na jinsi inavyoweza kutumika kama nyenzo katika maisha yao ya kila siku.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO

 • Ingawa huenda una ufahamu fulani au ni mtumiaji mzuri wa mtandao, Je, umewahi kutulia na kujiuliza: "Intaneti ni nini?"
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kwa kushirikiana na mwenzako au kikundi kidogo, tumieni dakika mbili kujadili na kuandika mawazo yenu.

Endesha majadiliano ya kikundi kizima (dakika mbili) kisha uandike majibu yao ubaoni.

Dondoo Kwa Mwalimu

Baada ya kipindi hicho cha kutoa mawazo, andika maana hizi ubaoni:

 • Intaneti: Intaneti ni mtandao unaounganisha kompyuta pamoja na kuwezesha taarifa au data kusafiri kutoka kompyuta moja hadi nyingine.
 • Mtandao: Huunganisha kompyuta pamoja. Kwa mfano, nyaya za simu huunganisha simu yako ya nyumbani na simu zingine na kukuwezesha kuwasiliana na watu wengine walio kwenye mtandao huo wa simu.
 • Data: Uwezo wa kufahamu, kuunda, kukusanya, kuwakilisha, kutathmini, kutafsiri na kuchanganua data kutoka kwenye vyanzo vya kidijitali na visivyo vya kidijitali.

Wape wanafunzi fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maana hizo tatu.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Je, kuna ufanano au utofauti wa kile mnachofikiri kuhusu maana ya intaneti na maana zilizotolewa?
 • Je, maana hizi zina jukumu gani katika tovuti kama vile YouTube?
  • Mfano:
   • YouTube: Ni tovuti ya kupakia video kwenye intaneti inayotumia nywila/neno la siri kuingia na kuwaruhusu watu kuangalia data/maudhui yao.
   • Intaneti: Hukuunganisha moja kwa moja kwenye YouTube.
   • Mtandao: Watu hutumia kompyuta/vifaa vingine vya kidijitali ili kuunganishwa kwenye intaneti kupitia mitandao ya simu za mkononi au satelaiti.
   • Data: Ufikiaji wa maktaba ya video na taarifa katika YouTube.

Mazungumzo ya Darasani [dakika 10]

Wanafunzi watazijua njia tofauti ambazo kompyuta huunganishwa kwenye intaneti na jinsi taarifa zinavyosambazwa.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Hivi sasa kwa kuwa tuna uelewa wa msingi kuhusu intaneti. Je, watu hutumia vipi intaneti?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tumia dakika mbili kujadili suala hili na mwenzako. Tutazungumzia majibu yenu mtakapomaliza.

Dondoo Kwa Mwalimu

Baada ya takribani dakika mbili waombe wanafunzi watoe majibu yao. Andika majibu hayo kwenye ubao. Majibu yanayoweza kutolewa ni pamoja na:

 • Kuchati
 • Manunuzi
 • Barua pepe
 • Kutazama Tovuti za vichekesho
 • Kutengeneza na kutuma Video
 • Kutazama Filamu
 • Kukusanya Taarifa

Weka majibu kwenye makundi tofauti ubaoni. Majibu mengi yanaweza kuwa katika makundi haya:

 • Mawasiliano
 • Burudani
 • Kazi

Mazungumzo ya Darasani [dakika 20]

Wanafunzi watajifunza jinsi vifaa vinavyounganishwa kwenye intaneti.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Ni dhahiri kwamba intaneti imebadilisha jinsi watu wanavyo wasiliana pamoja na jinsi wanavyoishi maisha yao. Je, kuna mifano gani ya baadhi ya vifaa vinavyotumia intaneti hivi sasa?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tumieni dakika mbili kujadili suala hili na mwenzako. Tutazungumzia majibu yenu mtakapomaliza.

Dondoo Za Mwalimu

Baada ya takribani dakika mbili waombe wanafunzi watoe majibu yao. Andika majibu yao kwenye ubao. Majibu yanayoweza kutolewa ni pamoja na:

 • Simu
 • Kompyuta/Kishikwambi
 • Televisheni
 • Mifumo ya Michezo
 • Magari

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Sasa kwa kuwa tumetambua vifaa vinavyotumia Inteneti. Je, vifaa hivi vinaweza kuunganishwa vipi kwenye intaneti?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Intaneti bila waya ni namna inayotumika zaidi ya kuunganisha vifaa kwenye intaneti. Intaneti bila waya hutumia mawimbi ya redio kuunganisha vifaa hivibila kutumia nyaya halisi.

Dondoo Kwa Mwalimu

Waoneshe wanafunzi picha iliyo kwenye slaidi.
Tumia picha kuelezea jinsi ya kujiunga kwenye intaneti kwa kutumia kifaa.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Vifaa vya mkononi hutumia mtandao wa simu ili kuunganishwa kwenye intaneti, hususan vikiwa havipo kwenye mtandao wa shule, maktaba au wa nyumbani.

Mitandao ya simu ni aina ya mawimbi ya redio yasiyotumia waya ambayo hufika mbali ikilinganishwa na ile ya kutumia rauta. Mitandao ya simu hutumia transiva maalum zinazoitwa minara ya simu ili kuunganisha kifaa chako cha mkononi kwenye intaneti.

Mambo muhimu ya kukumbuka [dakika 10]

Dondoo Kwa Mwalimu

Pitia somo ukitumia hoja hizi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Intaneti ni mtandao mkubwa wa kompyuta zilizounganishwa pamoja kupitia mtandao ulimwengu mzima.

Intaneti imebadilisha na huenda itaendelea kubadilisha jinsi tunavyoishi katika jamii.

Watu hutumia intaneti kila siku katika maisha yao ili kuwasiliana, kufanya kazi, kufanya tafiti na kwa ajili ya burudani.

Watu huunganishwa kwenye intaneti kwa kutumia vifaa mbalimbali, kama vile kompyuta, simu za mkononi, televisheni, vifaa vya michezo na magari ili kusambaza na kupokea taarifa.

Kuna namna mbalimbali za kuunganishwa kwenye intaneti kwa kutumia waya au bila kutumia waya.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy