Utangulizi wa Mafunzo ya Kidijitali

Somo 2: Taarifa za Kidijitali na Kusambaza

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Chagiza Somo kwa [dakika 10]

Dondoo Za Mwalimu

Uchagizaji wa somo huwapa walimu mwongozo kuhusu kiasi cha mambo ambayo wanafunzi wanayajua kabla ya kuanza maudhui ya somo.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Mwambie mwenzako mambo mawili: 1) Chakula au jambo unalolipenda zaidi 2) Tarehe yako ya kuzaliwa.

Kisha, jadiliana kuhusu ni lipi kati ya mambo hayo mawili linaweza kuchukuliwa kama taarifa ya jumla na lipi linaweza kuchukuliwa kama taarifa ya kidijitali.

Dondoo Za Mwalimu

Baada ya kujadili masuala haya kwa dakika mbili katika vikundi vya watu wawili, omba kundi lieleze kuhusu ni majibu yaliyotolewa. Pia katika majibu hayo, yapi wanadhani ni taarifa za kawaida na yapi yanaweza kuchukuliwa kama taarifa za kidijitali.

  • Jibu: Chakula au jambo ulipendalo, zaidi ni taarifa ya jumla na tarehe yako ya kuzaliwa itachukuliwa kama taarifa ya kidijitali.

Baada ya wanafunzi kumaliza kutoa maoni yao andika maana hizi ubaoni.

  • Taarifa: Ukweli au taarifa kuhusu mtu au kitu.
  • Taarifa za kidijitali: Taarifa ambazo kompyuta inaweza kuchakata. Zinaweza kuwa namba, maneno, picha, video au sauti. Mfano; barua pepe, picha kwenye mtandao wa kijamii au hata video.

Mjadala wa Kundi [dakika 5]

Wanafunzi watapata uelewa wa kina kuhusu kiasi kikubwa cha data zinazosambazwa kwenye intaneti.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mnadhani ni watu wangapi wanatumia intaneti?
Dondoo Za Mwalimu

Wape wanafunzi fursa ya kutoa maoni na kuyaandika kwenye ubao.

Baada ya kuandika maoni yao machache wape jibu.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Karibu watu bilioni 4.57 au asilimia 59 ya watu wote walioko ulimwenguni hutumia intaneti na idadi hii inaendelea kuongezeka.

Hali hii husababisha kutengenezwa kwa data NYINGI SANA za kompyuta. Data za kompyuta ni taarifa zote zinazotumwa, kuonekana, kusambazwa, kuhifadhiwa na kuchakatwa katika kompyuta.

Kisha, tutakwenda kuangalia namna ambavyo data hizi zinavyosambazwa na namna ya kujilinda na kuziweka data zako katika usalama.

Mazungumzo ya Darasani [dakika 20]

Wanafunzi watapata uelewa wa kina kuhusu aina za data zinazosambazwa kwenye intaneti.

Dondoo Kwa Mwalimu

Ligawe darasa katika vikundi vidogo.

Wape wanafunzi wako picha 5-10 zinazoonyesha njia za kusambaza taarifa.

Mifano inaweza kuwa ni pamoja na picha ya watu wawili wakizungumza, video, mtu akisoma kitabu, mtu akimtumia ujumbe n.k.

Ukumbusho: Ikiwa huna picha za aina hii unaweza kuzichora mwenyewe au uwaombe wanafunzi wachore namna ambavyo watu wanasambaziana taarifa ili kuliboresha zoezi hili na kuongeza ushiriki wa wanafunzi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Jadilianeni kuhusu picha zilizo kwenye skrini katika vikundi vidogo kwa takriban dakika moja kwa kila picha. Kisha tafakarini ikiwa picha hiyo inaashiria kusambaziana taarifa za kidijitali au la.

Dondoo Za Mwalimu

Wape muda wa kujadili ikiwa vikundi vina maoni tofauti.

Mazungumzo ya Darasani [dakika 20]

Wanafunzi watapata uelewa kuhusu namna ya kuweka taarifa zao za kidijitali salama wanapotumia intaneti.

Dondoo Kwa Mwalimu

Waombe wanafunzi wako wabaki katika vikundi vyao vidogo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Je, taarifa zenu ziko salama kwenye intaneti?
  • Elezeni ni kwa nini au kwa nini haziko salama?
Dondoo Za Mwalimu

Wape dakika mbili na uwaruhusu wanafunzi kutoa maoni yao katika kundi zima.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kisha, tutazijadili njia nne za kuhakikisha usalama wako na wa taarifa zako kwenye intaneti.

Wakati mwingine, unapewa fursa ya kuchagua mtandao wa WiFi ambao ungependa kutumia. Ni muhimu kukumbuka kwamba kuna hatari kubwa iwapo utajiunga na mtandao wa WiFi usiofaa.

DONDOO KWA MWALIMU

Soma taarifa zilizo katika kila slaidi.

Mitandao ya Umma (Isiyo Salama, Isiyoaminika)

  • Mitandao isiyohitaji nywila ili kuingia.
  • Watu wengine walio kwenye mtandao huo wanaweza kuziona taarifa zako. Wanaweza kuiba taarifa unazotuma, kupitia mtandao huo au kufuatilia mambo unayofanya.
  • Kwa mfano, ikiwa uko kwenye ukumbi wa sinema kisha uone jina la mtandao wa shule yako kwenye simu yako wakati unapotafuta mtandao wa umma unatakiwa kujua kwamba mtandao, huo unajaribu kuiga au kuonekana kama mtandao wa shule yako ili kukusanya nywila kutoka kwa wanafunzi wasio na habari.

Mtandao binafsi (Salama, Unaoaminika)

  • Unahitaji nywila, uwekaji wa kodi umewezeshwa na unakuhakikishia kwamba mtandao unaojiunga nao ndio unaowakilishwa na jina la mtandao huo.
  • Mitandao salama na inayoaminika hutoa ulinzi zaidi. Zingatia muktadha na eneo la mtandao huo.

Mtandao Unaolindwa na Nywila

  • Unapo tengeneza mtandao unaolindwa na nywila, sharti mmiliki wa mtandao huo awashe rauta.
  • Uwekaji wa kodi wa kawaida mara nyingi ni Wired Equivalent Privacy, (WEP), Wireless Internet Protected Access (WPA) au WPA2.
  • Vifaa hivyo hufanya taarifa zinazotumwa, kwa njia isiyokuwa ya waya kwenye mtandao, ziharibiwe (au kuvurugwa). Uwekaji wa kodi ulibuniwa ili kufanya iwe vigumu kwa wadukuzi kuona unachotuma.

Tovuti

  • HTTPS ni kiwango kinachotumiwa na tovuti ili kusimba data inayopitishwa kwenye intaneti.
  • Uwekaji wa kodi unaweza kuzuia mhusika yeyote asiyehusika kutazama data zilizo kwenye mtandao wako kwa urahisi. Mfumo huu unatoa usalama wa ziada na unaweza kutumika katika kuperuzi chochote kwa kuongeza “https://” kabla ya URL unayotumia (mfano https://www.mysite.com). Hata hivyo, si tovuti zote zinazoweza kutumia HTTPS.
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kwa kutumia chati na kuzingatia mazungumzo yetu ya leo kuhusu taarifa zilizo mtandaoni na jinsi ya kuzipata, tumieni dakika chache kujibu maswali matatu yafuatayo katika vikundi vyenu vidogo na muwe tayari kutoa majibu yenu ya kundi zima.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Kuna manufaa kujiunga na intaneti?
  • Kuna matatizo au changamoto zipi zinazotokana na kujiunga kwenye intaneti?
  • Kuna masuala gani kuhusu usalama yanayoweza kuibua wasiwasi wakati wa kutumia njia isiyotumia waya tofauti na kutumia njia ya kujiunga na intaneti kwa njia ya waya?

Mambo muhimu ya kukumbuka [dakika 5]

Dondoo Kwa Mwalimu

Pitia somo ukitumia hoja hizi.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Intaneti ni mtandao mkubwa wa data na hutumiwa na asilimia 59 ya watu wote ulimwenguni (idadi hii inaongezeka!)

Taarifa za kidijitali ni taarifa ambazo husambazwa kwa njia ya intaneti katika mfumo wa namba, maneno, picha, video au sauti.

Intaneti inaweza kupatikana kupitia njia ya kuunganisha kwa waya au bila waya na unatakiwa uweze kuleta uwiano wa madhara na manufaa ya kutumia mitandao ya umma.

Intaneti ni njia muhimu ya watu kushiriki kwenye masuala ya kijamii, katika ngazi za kawaida, kitaifa na kimataifa.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy