Fursa za Kidijitali

Somo 2: Kutambua Uwezo Wetu

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Ni Kitu Gani cha Kipekee Unachoweza Kuwapa Watu?

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Leo, tutajishughulisha na kuangalia mbinu na uwezo wetu na jinsi tunavyoweza kutumia mbinu hizi kufanya shughuli tulizo na ari nazo.

Wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kufahamu jinsi ya kubadili mambo uliyo na ari nayo na yale unayofurahia na kuyageuza ili yawe mbinu unazoweza kutumia kwa shughuli tofauti — pengine iwe kazi ya kujitolea, tarajali, mpango wa mustakabali wa masomo ya chuo kikuu au wa kazi. Hata hivyo, kwa kufanya mazoezi, tunaweza kufanikiwa kufanya hayo!

Katika hatua ya kwanza, ni muhimu kutambua mbinu ambazo umepata ukiwa nje na ndani ya shule.

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Sambaza kitini cha “Kutathmini Stadi Zako (Vitenzi, Nomino, na Vivumishi)!" kitini na kalamu za wino au penseli.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Kwenye kitini chako, kuna orodha za aina mbili tofauti za mbinu: 1) mbinu zinazoweza kutumika katika nyanja tofauti 2) mbinu za elimu au maarifa

Unaweza kuchukulia mbinu zinazoweza kutumika katika nyanja tofauti kama zile ambazo unaweza kutumia katika kazi moja na kuzitumia katika kazi nyingine kwa urahisi. Kwa mfano, kuweza kubadilika ili kuendana na hali mpya na kushirikiana na wengine kunaweza kukusaidia kusonga mbele bila kujali mahali ulipo — katika shule au kazi yoyote utakayoamua kufanya, kuanzia kuwa muuguzi hadi mwalimu wa shule au msanifu wa programu za kompyuta. Pia unaweza kuchukulia mbinu hizi kama vitenzi — kama vile "kutafiti," "kupanga," au "kujadiliana."

Mbinu za elimu au maarifa ni stadi ambazo hutumika tu katika taaluma fulani kama vile sanaa ya vitu vinavyoonekana (mfano, usanifu wa michoro) au sayansi (mfano, kemia). Baadhi ya mifano ya mbinu hizi ni kama kuweza kuunda ukurasa wa wavuti, kutengeneza michoro ya kuchekesha kwa ajili ya magazeti, au kufanya jaribio la kemia katika maabara. Huenda mmejifunza mbinu hizi shuleni, katika mpango wa masomo wa baada ya shule, kutoka kwenye vitabu, kutoka kwa mshauri au mkajifunza wenyewe tu. Unaweza kuchukulia mbinu hizi kama nomino, kama vile "biolojia," "tamthilia," au "takwimu."

Kitini hicho pia kina safu ya mbinu ambazo tunahisi kuwa zinaelezea jinsi tunavyofanya mambo katika maisha yetu ya kila siku. Mbinu hizi zinaitwa mbinu za tabia zetu na zinaweza kuchukuliwa kama vivumishi. Kwa mfano, unaweza kuwa mbunifu sana katika namna ambavyo unakabili suala fulani na unafurahia kuwa na mawazo yasiyo ya kawaida. Au huenda unawajali watu wengine sana na kila wakati unajitahidi sana ili kuhakikisha kuwa hali zilizopo zinawahusisha watu wote na zina usawa. Au huenda una akili nzuri sana, jambo ambalo linaweza kukusaidia kustahimili hata unapokumbana na vizuizi.

Kwa kuangalia kitini cha "Kutathmini Stadi Zako (Vitenzi, Nomino, na Vivumishi)!" kitini, ningependa utumie dakika 10 zijazo kwa kukadiria jinsi unavyodhani uko vizuri kwa kila mbinu unayoweza kuitumia katika nyanja mbalimbali na mbinu ya elimu/maarifa. Kwa sasa, msitilie maanani safu ya mwisho — mbinu za tabia binafsi.

Kwa baadhi ya mbinu za elimu/maarifa unaweza kutaka kutoa maelezo mahususi. Kwa mfano, chini ya "sanaa ya maonesho", huenda unacheza piano vizuri sana. Chini ya safu ya "kisehemu kidogo" unaweza kuandika sehemu mahususi ya taaluma fulani ambayo una ujuzi wake!

Pia kuna safu chache zilizo wazi hapo chini ya orodha ya mbinu za elimu/maarifa — ikiwa hutaona nyanja za mbinu ulizo na ari nazo katika orodha hiyo, unaweza kuziongeza!

DONDOO KWA MWALIMU

Mifano iliyoko hapo juu inaweza kurekebishwa ili kuendana na mambo ambayo wanafunzi wako wanafahamu na pia muktadha wa eneo lenu. Mifano iliyoko hapo juu inalenga kuwafundisha wanafunzi tofauti ya mbinu zinazoweza kutumika katika nyanja tofauti na mbinu za elimu/maarifa.

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wape washiriki dakika 10 ili wajaze ukadiriaji wa safu za "Mbinu Zinazoweza Kutumika Katika Nyanja Tofauti" na "Mbinu za Elimu/Maarifa" kwenye kitini.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Sasa chagua angalau mbinu tano (kutoka kwa zile zinazoweza kutumika katika nyanja tofauti na zile za elimu/maarifa) ambazo umepatia ukadiriaji wa juu (yaani, umezipa ukadiriaji wa nne au tano). Fikiria kuhusu jinsi unavyozitumia mbinu hizo. Pengine ni "kwa ukarimu," au "kwa ubunifu," au pengine "kwa njia nyumbufu" — mbinu za tabia binafsi. Ili kuzitambua mbinu hizi, unaweza kufikiria kuhusu, "Ni kwa vipi jamaa au marafiki zako wanavyokueleza?" na "Ni kwa vipi unayakabili majukumu na shughuli mpya?" Tumia dakika chache kuandika vivumishi chini ya safu ya "Mbinu za Tabia Binafsi/Vivumishi" kwenye kitini chako.

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wape washiriki dakika tano ili waandike mbinu chache za tabia binafsi kwenye kitini.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Natumai kwamba zoezi hili litawapa ufahamu wa uwezo wenu, ambao unaweza kuchukuliwa kama mchanganyiko wa nomino, vitenzi na vivumishi.

Kumbukeni kwamba mnapofikiria kuhusu fursa za siku zijazo ambazo mngependa kutekeleza, jambo linalokufanya mtu wa kipekee sio kuwa na nomino au vitenzi au vivumishi vingi pekee. La muhimu zaidi ni jinsi ambavyo utaleta vipengele hivi pamoja ili kukusaidia kuelewa jambo unalotoa kwa ulimwengu kwa namna ya kipekee!

Zoezi

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Baada ya kukamilisha kujaza karatasi ya zoezi, andika mbinu 10 ulizozipa ukadiriaji wa juu zaidi. Jaribu kuchagua mchanganyiko wa mbinu zinazoweza kutumika katika nyanja mbalimbali, elimu/maarifa (na mbinu chache za tabia binafsi mlizoandika) — yaani, mbinu za vitenzi, nomino, na vivumishi. Kwa kila moja ya mbinu hizo 10, toa mfano MAHUSUSI wa wakati ambapo ulitumia uwezo huo.

Mwisho, kutoka kwenye orodha yako, chagua angalau tano na ufikirie kuhusu jinsi unavyoweza kutumia mbinu hizo kwa pamoja ili kufanya na kufanikiwa katika shughuli ulizo na ari nazo. Eleza jinsi unavyoweza kuzitumia mbinu hizo kwa pamoja katika aya chini ya orodha yako.

Kwa mfano, tuseme kwamba mimi ni mwanafunzi anayetaka kuwa daktari siku moja. Ninafanya vizuri sana katika masomo yangu ya biolojia na kemia (yaani, mbinu za elimu/maarifa) na pia ninaweza kuwasiliana na watu wengine vizuri sana na kusuluhisha matatizo (yaani, mbinu zinazoweza kutumika katika nyanja mbalimbali).

Vilevile, ninahisi kwamba mimi hukabili miradi mipya kwa ustahimilivu na utaalamu (yaani, mbinu za tabia binafsi). Ninaweza kuzitumia mbinu hizi katika siku zijazo, baada ya kupata leseni yangu ya udaktari, ili kutibu wagonjwa, kuwasaidia kupona magonjwa yao na pia kuboresha hali ya maisha kwa kiasi kikubwa huku nikiwa na matumaini ya kuwa daktari mtaalamu wa uwanja fulani wa matibabu katika siku zijazo.

DONDOO KWA MWALIMU

Mifano iliyoko hapo juu inaweza kurekebishwa ili kuendana na mambo ambayo wanafunzi wako wanafahamu na pia muktadha wa eneo lenu. Mifano iliyoko hapo juu inalenga kuwafundisha wanafunzi tofauti ya mbinu zinazoweza kutumika katika nyanja tofauti na mbinu za elimu/maarifa.


End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy