Muhtasari wa Somo
Wanafunzi watafanya yafuatayo:
- Kutoa maana ya shukrani na kutoa mfano wa wakati waliposhukuru.
- Kuelewa kwamba kuna aina nyingi za mambo ambayo tunaweza kuonesha shukrani.
Wanafunzi watafanya yafuatayo:
Masuala ya kutafakari kabla ya zoezi hili:
Tayari?
Anza Somo
Wanafunzi watatengeneza makundi ya watu wawili wawili.
Baada ya makundi ya watu wawili wawili kumaliza kuzungumza, uliza:
Eleza kwamba "shukrani" ni hisia tunayokuwa nayo tunapoonesha tunathamini watu wengine kwa kutuonesha fadhila au kutufanyia matendo ya kutujali. Toa mfano wa maisha yako mwenyewe, kama vile: "Nilijihisi kushukuru wakati mtu fulani aliposhikilia mlango ili niweze kupita asubuhi ya leo kwa sababu nilikuwa nimebeba mifuko mizito."
Jadili jinsi tunavyoweza pia kuwa na shukrani tunapothamini vitu halisi tulivyo navyo, vitu ambavyo tulipewa na mtu mwingine au vitu tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku ambavyo wakati mwingine hatuvitilii maanani sana. Toa mfano wa maisha yako mwenyewe, kama vile: "Nilijihisi kushukuru kwa sababu ya chakula changu cha jioni jana, kwa sababu nilikuwa na njaa sana na kilikuwa kitamu."
Onesha jinsi watu wengi pia wanavyohisi kushukuru kwa sababu ya vitu vilivyo katika mazingira ya asili. Toa mifano kuhusu hili, kama vile: "Ninahisi kushukuru kwa sababu ya mvua inayotupa maji ya kunywa na kusaidia mimea kukua."
Jadili jinsi wakati mwingine tunavyohisi kushukuru kwa sababu ya mambo ambayo hatuwezi kugusa au kuona, lakini ni mambo muhimu hata hivyo, kama vile afya nzuri, utamaduni au desturi zetu, usawa, mawazo yanayotupa msukumo au kuwa hai tu. Toa mfano mwingine wa maisha yako mwenyewe, kama vile: "Ninahisi kushukuru wakati ninapojifunza jambo jipya, kwa kuwa mafunzo hufanya akili yangu kukua."
Eleza kwamba mara nyingi tunatoa shukrani kwa kumwambia mtu "Asante".
(Kumbuka: Wanafunzi wengine huenda wanatoka katika familia au tamaduni ambapo sio kawaida kusema asante kwa maneno. Wahimize wanafunzi wazungumzie namna zingine ambazo jamaa zao au watu wa jamii wanazotoka huenda wanazitumia kuonesha shukrani. Katika tamaduni nyingine, watu hutoa shukrani baada ya kupata mlo mzuri kwa kusugua miguu na mikono yao kwa mikono yao yenye unyevu punde tu baada ya kumaliza kula.
Tunapohisi kushukuru, kwa kawaida tunasema "asante" au "tunashukuru."
Mpe kila mwanafunzi kikaratasi kinachoweza kubandikwa. Waambie waandike muhtasari mfupi kuhusu wakati ambao walijihisi kutoa shukrani na walitaka kutoa shukrani kwa sababu gani au kwa nani (wanaweza kutumia lile wazo walilozungumzia hapo kabla au lingine jipya). Waoneshe vile vibao vinne katika kona nne za chumba.
Angalieni vikaratasi vyenu na mfikirie kuhusu ni kibao kipi kati ya vile vinne vya, "Vitu Tunavyomiliki," "Matendo ya Fadhila," "Mazingira ya Asili," na "Mambo Mengine Muhimu," kinaelezea vizuri zaidi yale mambo mliyoandika. Tembea kimyakimya na usimame kando ya alama inayoeleza wazo lako. Ikiwa wazo lako haliendani na kibao chochote, simama katikati ya chumba. Mwanafunzi yeyote aliye katikati ya chumba anaweza kubuni kategoria mpya. Zungumzia ulichoandika katika kikundi chako.
Ikiwa kuna mwanafunzi mmoja tu katikati ya chumba, mwambie aseme alichoandika pamoja na kategoria mpya aliyobuni. Jadili kategoria hiyo mpya ya shukrani na darasa zima. Omba mwanafunzi mmoja au wawili kutoka kwenye kila kikundi wajitolee kutoa mfano wa aina ya shukrani inayoashiriwa na kibao walichochagua au ile kategoria mpya.
Baada ya mifano kutoka kwenye kila kundi kutolewa, yaambie makundi yote yazunguke kisha yasimame karibu na alama mpya. Waombe wanafunzi wajadiliane tena kuhusu mambo wanayohizi kutoa shukrani kuhusu ambayo yanaelezewa na hii alama mpya (hawahitaji kuandika mambo haya). Omba mfano mmoja au miwili kutoka kwenye kila kundi.
Ikiwa kutakuwa na muda, endeleeni katika mtindo wa mzunguko hadi wakati ambapo kila mtu atakuwa amepitia katika vituo vyote vinne (au vitano).
Waombe wanafunzi wafikirie kuhusu jinsi walivyohisi walipofikiria kuhusu mambo au watu walio na shukrani juu yao.
Wanawezaje kuwahimiza wengine waoneshe shukrani?
Waambie wanafunzi waandike aya moja au wachore michoro inayoonesha mambo ambayo wanataka kutoa shukrani.
Weka aya au michoro hiyo kwenye ubao. Wahimize wanafunzi waangalie "vitu" halisi ambavyo vilizungumziwa.
Walipewa vitu hivyo na nani? Fikiria kuhusu watu waliosaidia kutengeneza vitu hivyo. Ongeza watu hao kwenye mambo unayotakata kutoa shukran!
Hongera!
Umekamilisha Somo
Wanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu maana ya uthibitishaji wa taarifa na kwa nini ni muhimu kwa wapokezi wa habari kuthibitisha habari wanazosoma au kutazama.
Tazama UkurasaWanafunzi watafikiria na kuandika kuhusu jinsi maisha yao yatakavyokuwa miaka 40 kutoka sasa.
Tazama UkurasaWashiriki watajifunza jinsi metadata zinavyotumika katika mchakato wa kuthibitisha habari kwa kutazama metadata za picha katika vitazamaji vitatu tofauti vya metadata.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza kuhusu na kutambua njia ambazo aina tofauti za vyombo vya habari zinaweza kutumiwa ili kuwahamasisha watu kuhusu suala fulani.
Tazama UkurasaWanafunzi watajifunza jinsi ya kubuni mpango wa awali wa kampeni zao wenyewe za utetezi.
Tazama UkurasaWanafunzi watafanya kuorodhesha maadili kulingana na umuhimu wake.
Tazama Ukurasa