Ustawi wa Kidijitali

Somo 6: Muda Wangu Mimi tu

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Kabla ya kuanza zoezi hili, vuteni pumzi kwa nguvu kwa muda mchache. Wakumbushe wanafunzi kwamba wanahimizwa washiriki lakini hawatakiwi kufanya hivyo. (Wanakaribishwa kukaa na kubaki kimya ikiwa wataamua kutoshiriki.)

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tutasababisha usumbufu mdogo au kujiletea mawazo kwenye akili na miili yetu kimakusudi kwa kufikiria kuhusu hali ngumu, ili tujifunze jinsi ya kujifariji.

Wachezee wanafunzi wako sauti iliyorekodiwa au uwaongoze kwenye mazoezi haya ukitumia taarifa ifuatayo.

Fikiria kuhusu hali katika maisha yako inayokutatiza au kukupa mawazo mengi. Tafadhali chagua hali ambayo sio mbaya zaidi au ngumu zaidi maishani mwako, lakini iwe hali ambayo inakutatiza kidogo. Unapofikiria kuhusu hali hii, je, unaweza kupata hisia fulani katika mwili wako, pengine kero kama kubanwa kifuani au maumivu makali ya ghafla tumboni? Sasa, jiambie: "Katika wakati huu, kuna sehemu yangu inayopitia changamoto." Hii ndiyo maana ya kufahamu unachohisi. Pengine utasema, "Jamani, najihisi vibaya sana," au "Hali hii inakera," au labda, "Huu ni usumbufu mkubwa."

Sasa jiambie: "Changamoto ya aina hii ni sehemu ya maisha." Hii ni kawaida kwa binadamu wote. Kuna watu wengine wengi wanaopitia changamoto hii.
Pengine utaamua kusema, “Vijana wengine hujihisi hivi pia," au "Sio mimi peke yangu ninayejihisi hivi," au "Hii ni sehemu ya maisha ya kijana na vijana wengine wengi wanapitia changamoto kama mimi tu." Au "Vijana wote hujihisi hivi wakati mmoja au mwingine…!”

Sasa, jiguse kwa namna ya kujituliza na kujifariji — pengine kwa kuuelekeza mkono kwenye moyo wako au kitendo kingine unachopendelea. Hisi joto la mkono wako likiingia kwenye mwili wako. Sasa, jiambie: "Acha nijionyeshe fadhila." Kumbukeni kwamba kama vijana, mnapitia mabadiliko mengi mno — akili zenu zinabadilika, miili yenu inabadilika, pengine mko katika shule mpya au mnawaza kuhusu masomo ya chuo, kuna misukumo na mabadiliko mengi sana. Kwa hivyo jionyeshe fadhila.

Ili kuzingatia mahitaji yako binafsi zaidi, jiulize, "Ninafaa kusikia nini hivi sasa?" Au ikiwa unatatizika kupata maneno ya kusema, jiulize,"Ningemwambia nini rafiki wa karibu ambaye anapitia haya? Je, ninaweza kujiambia maneno hayo?"

  • Acha nijipe faraja ninayohitaji.
  • Acha nijikubali jinsi nilivyo.
  • Acha nijifunze kujikubali jinsi nilivyo.
  • Acha nijisamehe.
  • Acha niwe na ushupavu.
  • Acha niwe salama.
  • Acha niwe na amani.
  • Acha nifahamu kwamba ninastahili upendo.
  • Ikiwa unahisi kujizungumzia ni jambo geni kwako au ni kana kwamba unaomba ruhusa, wakati wowote unaweza kuruka kusema jambo hilo na kusema tu "Ninatumaini kwamba nitajikubali jinsi nilivyo," au "Shupavu," au "Nijikubali," tambua kile unachohisi tu.
WAULIZE WANAFUNZI WAKO

Waulize wanafunzi swali moja au zaidi kati haya yafuatayo:

  • Kuna hisia gani unapojiliwaza kwa njia hii? Unahisi vipi unapofikiria kwamba unaweza kuanza kutambua unapopitia changamoto na kuanza kujiambia maneno ya faraja?
  • Kulitokea mabadiliko yoyote wakati ulipoelekeza mkono wako kwenye moyo wako?
  • Unawezaje kufahamu kwamba unaweza kujiliwaza mwenyewe vizuri zaidi?
  • Je, unaweza kufikiria kuhusu hali ambayo ukifanya hivi kunaweza kukusaidia?
  • Zingatia vile vipengele vitatu vya kujifariji — ni vipengele gani vilivyokuwa na maana zaidi kwako na ambavyo ni muhimu kutambua?
    • Kutambua unachohisi ("Huu ni wakati wa kupitia changamoto.")
    • Hali ya kawaida kwa binadamu wote "(Sio mimi peke yangu ninayepitia changamoto.")
    • Kujifariji (kujigusa mwili au kujiambia maneno ya upole; "Acha nijifariji.")

Zoezi

Masuala ya kutafakari baada ya mazoezi haya:

  • Wakati ulipokuwa unawaongoza wanafunzi katika mazoezi haya, ni mambo gani yaliyokuwa na ufanisi na ni yapi hayakuwa na ufanisi? Wanafunzi waliyachukulia vipi mazoezi haya? Utabadilisha jambo lolote utakapofanya zoezi hili wakati mwingine?
  • Je, umegundua kama wanafunzi wanaangalia makosa yao au changamoto zao za maisha kwa mtazamo tofauti baada ya kushiriki katika mazoezi haya?
  • Ni marekebisho gani yaliyofanyiwa mazoezi haya kwa kuzingatia maoni ya wanafunzi na familia? Zoezi hilo lilikwendaje?
  • Je, wanafunzi walijadili jinsi mazoezi haya yanavyoweza kutumika au kuwa na manufaa au kutokuwa na manufaa katika maisha yao?

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Kituo cha The Greater Good Science Center hufanya utafiti wa saikolojia, sosiolojia, na sayansi ya nyurolojia na kufunza stadi zinazokuza ustawi, ustahimilivu na huruma katika jamii. Kituo cha GGSC kimejitolea kwa namna ya kipekee katika masuala ya sayansi na taaluma: Hatufadhili tu michakato bunifu ya utafiti wa kisayansi kuhusu ustawi wa kijamii na kihisia, bali pia tunawasaidia watu kutumia utafiti huu katika maisha yao binafsi na taaluma zao. Jifunze zaidi: https://greatergood.berkeley.edu/

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy