Ustawi wa Kidijitali

Somo 4: Mitazamo Tofauti

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Mtazamo ni Nini?

Sehemu ya 1

ONESHA PICHA YA MAZUNGUMZO YA DARASANI

Onesha picha ya Njozi ya Jagi la Maua ya Rubin kwenye skrini ya projekta. Huku ukiuliza maswali, waombe wanafunzi waje mbele na kuonesha ni picha gani wanayoona.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Mnaona nini mnapotazama picha hii?
  • Ni wangapi kati yenu wanaoona jagi la maua?
  • Ni wangapi kati yenu wanaoona hizo sehemu mbili?
  • Mnaweza kuziona sehemu hizo mbili kwa wakati mmoja?
  • Unachoona huenda kikategemea mtazamo wako.
  • Unadhani mtazamo ni nini?
MAZUNGUMZO YA DARASANI

Andika maelezo yanayotolewa na wanafunzi kwenye ubao.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Mtazamo ni namna maalum ya — unavyokitazama kitu.

Sehemu ya 2

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Huu hapa ni mfano mwingine. Tuseme kwamba rafiki yetu Abdul amefanikiwa kuingia katika timu ya mpira ya shule. Anapomwambia mama yake anasema, "Nimefanikiwa kuingia kwenye timu ya mpira!" Mama yake anafurahi na kumsifu. Wakati Abdul anapomwambia Raviv ambaye ndiye rafiki yake mkubwa kwamba amefanikiwa kuingia katika timu, Raviv anasema kwamba anafurahia sana mafanikio ya Abdul.

Abdul pia anamwambia rafiki yake Ahmed kwamba amefanikiwa kuingia katika timu ya mpira. Hata hivyo, Amed pia alikuwa amejaribu kuingia katika timu hiyo lakini Abdul akachukua nafasi yake. Kwa hiyo, Amed hajafurahia sana. Abdul pia ni mwanachama wa klabu ya sayansi na sasa atalazimika kutohudhuria mikutano ya sayansi ili afanye mazoezi ya mpira. Anapomwambia Amina, rais wa klabu ya sayansi, naye pia halifurahii sana.
Watu wote hawa walio maishani mwa Abdul walipata taarifa sawa: kwamba Abdul amefanikiwa kuingia katika timu ya mpira.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO

Kwa nini wote wanachukulia suala hili kwa namna tofauti?
Kwa nini mitazamo yao tofauti na mahusiano yao tofauti na Abdul ni muhimu?
Mnaweza kufikiria kuhusu mifano mingine inayoonesha jinsi watu tofauti wanavyoweza kuiona hali lilelile kwa mitazamo tofauti?

Umuhimu wa mitazamo ni nini?

Dondoo kwa Mwalimu

Mfano hapo juu unaweza kuboreshwa ili iendane na mazingira ya wanafunzi katika eneo unalofundisha. Kwa mfano:

  • Ethiopia: Tumia Tsehay (Mwanamke), Gebre (Mwanamume) Bisrat (Mwanamume) na Genet (Mwanamke) badala yake.
  • Ghana: Tumia majina kama Kofi (Mwanamume), Kojo (Mwanamume), Kweku (Mwanamume) Akua (Mwanamke) Afua (Mwanamke) Nana (Mwanamke)
  • Kenya: Tumia majina kama Luanda (Mwanamume), Charles (Mwanamume) Akinyi (Mwanamke) Muthoni (Mwanamke) badala yake.
  • Nigeria: Tumia majina kama Abdul (Mwanamume), Ade (Mwanamume), Chioma (Mwanamke), na Amina (Mwanamke) badala yake.
  • Zambia: Tumia majina kama Chanda (Mwanamume), Patrick (Mwanamume), Radhia (Mwanamke) na Valerie (Mwanamke) badala yake.

Sehemu ya 3

MAZUNGUMZO YA DARASANI

Wagawe wanafunzi katika makundi ya watu watatu au wanne. Lipe kila kundi karatasi na kalamu za wino au penseli.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Nitalipa kila kundi hati yenye wasifu wa kubuniwa wa Hiwot wa mitandao ya kijamii na karatasi ndogo. Kuna jina la mtu aliye maishani mwa Hiwot kwenye karatasi hiyo. Kama kundi, fikirieni kwamba mnatazama wasifu huu wa mitandao ya kijamii kupitia macho ya mtu aliye kwenye karatasi hiyo.

Mnadhani Hiwot ni nani? Ni mambo gani mnayoweza kudhania? Anapenda nini? Ni nini ambacho hapendi? Ametoa maoni kuhusu nini? Mnachukulia vipi Hiwot, kwa mujibu wa mtazamo wenu?

Mna dakika 10. Kuweni tayari kuwasilisha majibu yenu mwishoni!
Omba kila kundi liwasilishe majibu yaliyotolewa. Watu muhimu maishani mwa Hiwot/ambao huenda wakawa muhimu:

  • Mama yake Hiwot, ambaye ana wasiwasi kuhusu usalama wa binti yake
  • Rafiki mkubwa wa Hiwot, ambaye anamheshimu Hiwot
  • Msichana anayesomea katika shule ya karibu, ambaye hamjui Hiwot
  • Mwalimu wake Hiwot
  • Bosi ambaye anafikiria kumpa Hiwot kazi
Dondoo kwa Mwalimu

Mfano huu unalenga kuwaoyesha wanafunzi jinsi watu tofauti wanavyoweza kuuchukulia wasifu uleule katika mitandao ya kijamii ili kuwawezesha kufikiria kwa makini kuhusu taswira yao ya mtandaoni. Mfano huo unaweza kuboreshwa ili kuendana na mazingira ya wanafunzi katika eneo unalofundisha. Kwa mfano:

  • Ethiopia: Badala yake, tumia majina kama Msekerem au Hiwot.
  • Kenya: Badala yake, tumia majina kama Atieno au Lemanyanh.
  • Nigeria: Badala yake, tumia majina kama Abraham au Abdul.
  • Zambia: Badala yake, tumia majina kama Mulenga.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Kulikuwa na tofauti gani katika njia ambazo mlimtazama na kumtathmini Hiwot?
  • Mnadhani kwa nini kuna tofauti hizo?
  • Mnadhani kwamba tathmini hizo zote ni sahihi? Kwa nini/kwa nini siyo?
  • Mnaweza kufikiria kuhusu wakati hali kama hizi zilipotokea maishani mwenu —wakati taarifa zile zile zilichukuliwa kwa njia tofauti na watu tofauti?

Ni wangapi kati yenu wamekuwa na mabishano na wazazi/walezi wenu? Marafiki?
Ni wangapi kati yenu wanatumia mitandao ya kijamii? Mnafikiria kuhusu jinsi watu wengine wanavyochukulia wasifu wenu kwenye mitandao ya kijamii?
Mmewahi kufuta maudhui au kujiondoa katika maudhui mliyoshirikishwa katika mitandao ya kijamii (mfano, picha, video, machapisho ya maandishi)? Kwa nini?

Tafakuri Kuhusu Mitazamo

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Tafakari kuhusu namna tofauti tofauti ambavyo watu walio maishani mwako wanavyokuchukulia.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Je, unafanya mambo kwa njia tofauti ukiwa miongoni mwa watu tofauti?Je, wewe huzungumza na wazazi/walezi wako au walimu kwa namna sawa na unavyozungumza na marafiki zako? Kwa nini/kwa nini siyo?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Sote huenda tukawa watu tofauti kidogo kulingana na pahali tulipo na watu tulio nao.
Kama sehemu ya zoezi hili, tutajadili jinsi mnavyoweza kuonesha taswira zenu mtandaoni, hasa katika mitandao ya kijamii na jinsi watu wengine wanavyoweza kuwachukulia kwa namna tofauti kulingana na mitazamo yao.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Je, unaonesha taswira tofauti kwa watu tofauti mtandaoni?
    • Kwa mfano, katika mtandao mmoja (mfano, Facebook), huenda ukatumia jina lako halisi, lakini je, unatumia jina lako halisi katika shughuli zote unazoendesha kwenye Intaneti?
  • Ni katika mitandao ipi mingine ambapo sio kila wakati unatumia jina lako halisi au mitandao unayotumia bila kufichua utambulisho wako? Kwa nini?
  • Unadhani kwamba taarifa zako ambazo umesambaza mtandaoni zinaonesha taswira kamili kuhusu wewe?
  • Unadhani kwamba wasifu wa mitandao ya kijamii huonesha taswira kamili? Ungependa wasifu uoneshe taswira kamili?
  • Watu wanaweza kukuchukulia vipi ikiwa wanaweza kuzipata baadhi tu ya taarifa zako?
    • Kwa mfano, mtazamo wa wazazi/walezi wako utabadilika iwapo wataona kila kitu unachofanya katika mtandao mmoja wa kijamii lakini wasione shughuli zako kwenye mtandao mwingine?
  • Je, kile unachokichapisha unakifanya kuwa siri? Kwa nini?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Leo tumezungumza sana kuhusu mitazamo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
  • Kwa mujibu wa mazungumzo yetu, ni jambo gani moja ulilojifunza leo kuhusu mitazamo?
  • Kuna njia gani nyingine ambayo mitazamo huathiri namna ambavyo tunatathmini taarifa? Unaweza kutaja kisa cha hivi karibuni ambacho hali hii ilionekana?
  • Ni kwa vipi mitazamo ni muhimu na siyo tu kwenye maisha yetu binafsi bali pia katika mambo ya habari?

Zoezi

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Piga picha chapisho lolote katika mitandao ya kijamii (yaani picha, video, chapisho la maandishi) (sio lazima liwe chapisho lao wenyewe). Taja majukumu matatu ukizingatia chapisho la mtu huyo kwenye mitandao ya kijamii (mfano; rafiki, jamaa, mwalimu) kisha kwa kila jukumu, andika aya fupi ukieleza jinsi ambavyo mtu huyo atachulikulia chapisho hili.

DONDOO KWA MWALIMU

Katika dakika 10 za mwisho, wagawe wanafunzi katika makundi ya watu wawili wawili kisha wazungumze na wenzao kuhusu angalau namna mbili ambazo wanadhani mitazamo ni muhimu katika muktadha wa chapisho walilochagua.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy