Ustawi wa Kidijitali

Somo 3: Uwepo Katika Mtandao

Kabla ya kuanza somo, hakikisha umesoma muhtasari wa somo na matayarisho ya somo. Mwongozo wa Muwezeshaji unaweza pia kukusaidia kujitayarisha.

Muhtasari wa Somo


Matayarisho ya Somo


Begin Lesson

Tayari?
Anza Somo

Wasifu wa Mtandaoni na Kusimulia Visa

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Taarifa zinazokuhusu ambazo zinapatikana kwa umma mtandaoni hutoka katika vyanzo mbalimbali. Unaweza kuwa na udhibiti juu ya baadhi ya vyanzo hivyo, kama maudhui unayochapisha (mfano, picha, video, machapisho ya maandishi) kwenye wasifu wako wa mitandao ya kijamii.

DONDOO KWA MWALIMU

Kupitia skrini onesha maoni mabaya ya kubuniwa kuhusu Nelson Mandela yaliyotolewa mtandaoni. Tafadhali hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kwamba maudhui ya maoni hayo na akaunti hizo ni za kubuniwa tu. Zimebuniwa kwa ajili ya zoezi hili tu.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Mna maoni gani kuhusu ukurasa wa Facebook wa Nelson Mandela?
 • Vipi kuhusu maoni mabaya ya kubuniwa kuhusu Mandela?
 • Mnadhani maoni haya yangemfanya Mandela ajihisi vipi (mfano, kuudhika, kustaajabika)?
 • Yanaweza kuwafanya watu wengine kuhisi vipi, kutokana na jinsi wanavyompenda/wanavyomchukia Mandela?
DONDOO KWA MWALIMU

Mfano huu unalenga kuwawezesha wanafunzi kujua jinsi maoni mabaya yanayotolewa mtandaoni yanavyoweza kumuathiri mtu anayelengwa. Mfano huo unaweza kuboreshwa ili kuendana na mazingira ya wanafunzi katika eneo unalofundisha. Tunapendekeza msitumie wanasiasa wowote, na badala yake mtumie watu maarufu katika historia katika mfano huu.

WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Sasa fikiria kuhusu wasifu wako mwenyewe katika mitandao ya kijamii.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Watu watapata taswira gani baada ya kusoma wasifu wako?
 • Ni nani aliyetengeneza taswira hiyo?
 • Unaweza kuzithibiti vipi taarifa hizo?
 • Unaweza kuwa na udhibiti gani juu ya maudhui yanayokuhusu yaliyo mtandaoni? Ni nini ambacho huwezi kukidhibiti?
WAAMBIE WANAFUNZI WAKO

Angalia mojawapo ya wasifu wako wa mitandao ya kijamii (Facebook, Instagram, Snapchat, Twitter, WeChat, n.k.) au wasifu wa mitandao ya kijamii wa mtu mashuhuri (mfano; mtu aliye katika tasnia ya muziki, filamu, televisheni, mwanasiasa, kiongozi wa kibiashara). Zingatia maudhui mengi (mfano, picha, video, machapisho ya maandishi) yanayoonekana kwenye wasifu huo.

WAULIZE WANAFUNZI WAKO
 • Ni nani aliyetunga machapisho hayo? Kwa nini?
 • Baadhi ya maoni yaliyotolewa ni yapi?
 • Ni watu gani waliolengwa kwa kila chapisho?
 • Ni taarifa gani ambazo hazikuwekwa?
ZOEZI

Waombe wanafunzi waandike kwa ufupi wakizingatia machapisho waliyopitia katika zoezi la hapo nyuma kisha wajibu maswali yafuatayo:

 • Ni aina gani ya maudhui ambayo wewe/mmiliki wa akaunti UNAYADHIBITI/ANAYADHIBITI mwenyewe?
  • Majibu yanayopendekezwa: Jina unalotumia mtandaoni, machapisho ya matukio ya sasa, machapisho, picha au video unazopakia, maoni unayotoa kuhusu maudhui ambayo watu wengine wanasambaza katika mitandao ya kijamii.
 • Ni aina gani ya maudhui ambayo wewe/mmiliki wa akaunti HUWEZI kuyadhibiti mwenyewe?
  • Majibu yanayopendekezwa: Maoni ambayo watu wengine wanatoa kuhusu maudhui unayosambaza kwenye mitandao ya kijamii (mfano; machapisho yanayodumu kwa muda, machapisho ya matukio ya sasa, machapisho katika Twitter), maudhui ambayo wengine wanasambaza kwenye mitandao ya kijamii, jinsi marafiki/wafuasi/watu ulio na mahusiano nao mtandaoni husambaza maudhui uliyopakia.
 • Ni jambo gani moja unaloweza kufanya kuhusu taarifa ambayo mtu ameandika kuhusu wewe ambayo hupendi kwa sababu fulani (yaani HUNA udhibiti wa moja kwa moja wa taarifa hii)?
  • Majibu yanayopendekezwa: Kujiondoa katika chapisho uliloshirikishwa; kuwasiliana na mtu aliyechapisha taarifa hiyo na kumuomba aitoe; kumzuia mtu huyo; ikiwa unahisi uko hatarini mwambie mtu mzima unayemwamini; kwa kutegemea tovuti husika, unaweza kuripoti chapisho hilo na/au mtumiaji huyo ikiwa anakunyanyasa au kukudhulumu.

End Lesson

Hongera!
Umekamilisha Somo


Chanzo:
Maudhui haya yanahifadhiwa na Meta na hivi sasa yanajumuisha mafunzo yaliyotolewa kwa shirika la Youth and Media katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard chini ya leseni ya Kimataifa ya Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0. Unaweza kuyatumia maudhui hayo, ikiwa ni pamoja na kuyanakili na kuandaa kazi zinazotokana na maudhui hayo, kwa madhumuni ya kibiashara au la, ilimradi utataja mradi wa Youth and Media kama chanzo cha asili na kufuata masharti mengine ya leseni hiyo, kushirikisha kazi zingine zozote za ziada chini ya masharti hayo.

To help personalize content, tailor and measure ads and provide a safer experience, we use cookies. By clicking or navigating the site, you agree to allow our collection of information on and off Facebook through cookies. Learn more, including about available controls: Cookie Policy